16-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kuwa Mwandazi Awe wa Mwisho Kunywa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب كون ساقي القوم آخرهم شرباً
16-Mlango Wa Kupendeza Kuwa Mwandazi Awe wa Mwisho Kunywa
عن أَبي قتادة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( ساقي القوم آخِرُهُمْ شُرْباً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mnyweshaji wa watu ndiye wa mwisho wao kunywa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]