17-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kujuzu Kunywa Kutoka Katika Vyombo Vyote Vilivyo Tohara Isipokuwa Vya Dhahabu na Fedha, Kujuzu Al-Kar'i (Nayo ni kunywa Kwa Kutumia Mdomo Moja Kwa Moja Mtoni Bila ya Chombo Chochote au Mkono

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب جواز الشرب من جميع الأواني الطاهرة غير الذهب والفضة

وجواز الكرع – وَهُوَ الشرب بالفم من النهر وغيره بغير إناء ولا يد –وتحريم استعمال إناء الذهب والفضة في الشرب والأكل والطهارة وسائر وجوه الاستعمال

17-Mlango Wa Kujuzu Kunywa Kutoka Katika Vyombo Vyote Vilivyo Tohara Isipokuwa Vya Dhahabu na Fedha, Kujuzu Al-Kar'i (Nayo ni kunywa Kwa Kutumia Mdomo Moja Kwa Moja Mtoni Bila ya Chombo Chochote au Mkono

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : حَضَرَتِ الصَّلاَةُ فقامَ مَن كَانَ قَريبَ الدَّارِ إِلَى أهْلِهِ ، وبَقِيَ قَوْمٌ ، فأُتِيَ رسول الله صلى الله عليه وسلم بِمَخْضَبٍ مِنْ حِجَارَةٍ ، فَصَغُرَ المخْضَبُ أنْ يَبْسُطَ فِيهِ كَفَّهُ ، فَتَوَضَّأَ القَوْمُ كُلُّهُمْ . قالوا : كَمْ كُنْتُمْ ؟ قَالَ : ثَمَانِينَ وزيادة . متفق عَلَيْهِ ، هذه رواية البخاري .

وفي رواية لَهُ ولمسلم : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم دَعَا بإناءٍ مِنْ ماءٍ ، فَأُتِيَ بقَدَحٍ رَحْرَاحٍ  فِيهِ شَيْءٌ مِنْ ماءٍ ، فَوَضَعَ أصابعَهُ فِيهِ . قَالَ أنسٌ : فَجَعلْتُ أنْظُرُ إِلَى الماءِ يَنْبُعُ مِنْ بَيْن أصَابِعِهِ ، فَحَزَرْتُ مَنْ تَوضَّأ مَا بَيْنَ السَّبْعِينَ إِلَى الثَّمَانينَ .

Amesema Anas (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba wakati wa Swalaah ulifika, hivyo wale ambao nyumba zao zilikuwa karibu walikwenda kushika wudhu na wengine wakabakia na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Aliletewa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) chombo kilichotengenezwa kwa mawe kilichokuwa na maji ndani yake. Kilikuwa ni chombo kidogo sana kinachoweza kufunikwa na kitanga cha mkono. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alishika wudhu na watu wote waliokuwa pamoja nae pia walishika wudhu. Tukasema: "Mlikuwa wangapi?" Akasema: "Themanini au na ziada kidogo." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni riwaayah ya Al-Bukhaariy]

Na katika riwaayah ya Muslim: Hakika Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliitisha chombo cha maji. Akaletewa chombo kikubwa lakini chembamba kilichokuwa na maji kidogo. Alitia vidole vyake ndani yake. Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Niliona maji yakitoka baina ya vidole vyake. Makisio ya idadi ya watu walioshika wudhu kwa kutumia maji hayo ni baina ya sabini na themanini." 

 

 

Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن زيد رضي الله عنه ، قَالَ : أتَانَا النبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَخْرَجْنَا لَهُ مَاءً في تَوْرٍ مِنْ صُفْر فَتَوَضَّأَ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alikuja kwetu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nasi tukamletea maji katika chombo cha shaba, naye akashika wudhu (kutumia maji hayo). [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 3

وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَى رَجُلٍ مِن الأَنْصَارِ ، وَمَعَهُ صَاحِبٌ لَهُ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  إنْ كَانَ عِنْدَكَ مَاءٌ باتَ هذِهِ اللَّيْلَةَ في شَنَّةٍ وَإلاَّ كَرَعْنَا )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa Answaar akiwa pamoja na sahibu yake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ikiwa una maji kidogo yaliyobakia kutoka jana usiku katika kigudulia chako (cha ngozi) tupatie tunywe na ikiwa huna basi tutakunywa moja kwa moja kwa midomo yetu kutoka kwa kijito." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 4

وعن حذيفة رضي الله عنه ، قَالَ : إنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَانَا عَن الحَرِير ، وَالدِّيباجِ ، والشُّربِ في آنِيَة الذَّهَب والفِضَّةِ ، وقال : ((  هي لَهُمْ في الدُّنْيَا ، وهِيَ لَكُمْ في الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza kuvaa hariri na dibaji na kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha na akasema: "Vitu hivyo ni vyao hapa duniani na ni vyenu Aakhirah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أُمِّ سلمة رضي الله عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : ((  الَّذِي يَشْرَبُ في آنِيَةِ الفِضَّةِ ، إنَّمَا يُجَرْجِرُ في بَطْنِهِ نَارَ جَهَنَّمَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية لمسلم : ((  إنَّ الَّذِي يَأكُلُ أَوْ يَشْرَبُ في آنِيَةِ الفِضَّةِ وَالذَّهَبِ )) .

وفي رواية لَهُ : ((  مَنْ شَرِبَ في إناءٍ مِنْ ذَهَبٍ أَوْ فِضَّةٍ ، فَإنَّمَا يُجَرْجِرُ في بَطْنِهِ نَارَاً مِنْ جَهَنَّم )) .

Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayekunywa katika chombo cha fedha anaangushia moto tumboni mwake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad].

Na katika riwaayah ya Muslim: "Hakika anayekula au kunywa katika chombo cha fedha na dhahabu." 

Na katika riwaayah yake: "Mwenye kunywa katika chombo cha dhahabu au fedha, hakika anaangushia tumboni mwake moto kutoka Jahanam." 

 

 

 

 

Share