09-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miujiza Yake: Nuru Yake Kuwaongoza Swahaba Njia Katika Kiza
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
09-Miujiza Yake: Nuru Yake Kuwaongoza Swahaba Njia Katika Kiza
Swahaba wawili walikwenda nyumbani kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) usiku mmoja wa kiza, pindi walipoondoka, Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Alijaaliwa Nuru ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) iwaandame kama taa mbili zikiwaangazia njia. Basi kila mmoja wao alikwenda nyumbani kwake kwa nuru ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) iliyomwongoza njia kizani.
حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، حَدَّثَنَا مُعَاذٌ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ قَتَادَةَ، حَدَّثَنَا أَنَسٌ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَجُلَيْنِ، مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَا مِنْ عِنْدِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي لَيْلَةٍ مُظْلِمَةٍ وَمَعَهُمَا مِثْلُ الْمِصْبَاحَيْنِ، يُضِيآنِ بَيْنَ أَيْدِيهِمَا، فَلَمَّا افْتَرَقَا صَارَ مَعَ كُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا وَاحِدٌ حَتَّى أَتَى أَهْلَهُ.
Amesimulia Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Mara moja watu wawili miongoni mwa Swahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) walitoka katika nyumba ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) usiku wa kiza totoro. Walifuatwa na vitu viwili vinavyofanana na kandili mbili kuwaonyesha njia kwa mwangaza wake, na walipoachana, kila mmoja wao aliandamwa na moja kati ya hivyo vitu viwili mpaka wakafika nyumbani kwao. [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]
Na katika Riwaayah nyengine:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، قَالَ حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ هِشَامٍ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ حَدَّثَنَا أَنَسٌ، أَنَّ رَجُلَيْنِ، مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَا مِنْ عِنْدِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي لَيْلَةٍ مُظْلِمَةٍ، وَمَعَهُمَا مِثْلُ الْمِصْبَاحَيْنِ يُضِيآنِ بَيْنَ أَيْدِيهِمَا، فَلَمَّا افْتَرَقَا صَارَ مَعَ كُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا وَاحِدٌ حَتَّى أَتَى أَهْلَهُ.
Amesimulia Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ):
Swahaba wawili wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) waliondoka na kiza kilikuwa kimeingia, waliongozwa na mianga miwili mithili ya taa (kukiwatangulia kutokana na miujiza ya Allaah) ukiwamulikia njia mbele yao, na walipoachana, kila mmoja alimulikiwa na moja ya mianga hiyo mpaka walipofika majumbani mwao. [Al-Bukhaariy Kitaab Asw-Swalaah]