03-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Sifa ya Urefu wa Kanzu, Mikono Yake, Kikoi na Ncha ya Kilemba na Uharamu wa Kuburuza Chochote Katika Hizo Kwa Njia ya Kiburi na Karaha kwa Kufanya Hivyo Bila Kiburi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب صفة طول القميص والكُم والإزار وطرف العمامة وتحريم إسبال شيء من ذلك على سبيل الخيلاء وكراهته من غير خيلاء

03-Mlango Wa Sifa ya Urefu wa Kanzu, Mikono Yake, Kikoi na Ncha ya Kilemba na Uharamu wa Kuburuza Chochote Katika Hizo Kwa Njia ya Kiburi na Karaha kwa Kufanya Hivyo Bila Kiburi

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن أسماءَ بنتِ يزيد الأنصاريَّةِ رَضِيَ الله عنها ، قالت : كَانَ كُمُّ قَمِيص رسول الله صلى الله عليه وسلم إِلَى الرُّسْغِ . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Amesema Asmaa' bint Yaziyd Al-Ansaariyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Ilikuwa urefu wa mikono ya kanzu ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ikifika kwenye vifundo vya vitanga." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاءَ لَمْ يَنْظُرِ اللهُ إِلَيْهِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) فَقَالَ أَبُو بكر : يَا رسول الله ، إنَّ إزاري يَسْتَرْخِي إِلاَّ أنْ أَتَعَاهَدَهُ ، فَقَالَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  إنَّكَ لَسْتَ مِمَّنْ يَفْعَلُهُ خُيَلاءَ )) رواه البخاري وروى مسلم بعضه .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi, Hatamuangalia Allaah mtu huyo Siku ya Qiyaamah." Akasema Abu Bakr: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika kikoi changu kinanivuka bila kukusudia mpaka ninapokipandisha." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika wewe si katika wale wanaofanya hivyo kwa kiburi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  لا يَنْظُرُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ إِلَى مَنْ جَرَّ إزاره بَطَراً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Hamuangalii mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi." [Al-Bukhaariy, Muslim na Maalik]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَا أسْفَل مِنَ الكَعْبَيْنِ مِنَ الإزْارِ فَفِي النار )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kilicho chini ya fundo mbili katika kikoi kitakuwa motoni." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي ذر رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  ثلاثةٌ لا يُكَلِّمُهُمُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ ، وَلاَ يَنْظُرُ إلَيْهِمْ ، وَلاَ يُزَكِّيهِمْ ، وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ )) قَالَ : فقَرأها رسول الله صلى الله عليه وسلم ثلاثَ مِرار ، قَالَ أَبُو ذرٍّ : خَابُوا وَخَسِرُوا ! مَنْ هُمْ يَا رسول الله ؟ قَالَ : ((  المُسْبِلُ ، وَالمنَّانُ ، وَالمُنْفِقُ سِلْعَتَهُ بِالحَلِفِ الكاذِبِ )) رواه مسلم .

وفي رواية لَهُ : ((  المُسْبِلُ إزَارَهُ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Hatazungumza na watu aina tatu Siku ya Qiyaamah wala Hatawaangalia na wala Hatawatakasa na watakuwa na adhabu iumizayo." Akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliikariri kauli hii mara tatu." Akasema Abu Dharr: "Watu hao wamehasirika, ni kina nani ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Mwenye kuburuza nguo kwa kiburi; na mwenye kujionyesha kwa fadhila aliomfanyia mtu mwengine; na mwenye kuuza mali duni kwa kiapo cha uongo." [Muslim]

Na katika riwaayah nyingine: "Mwenye kuburuza kikoi chake kwa kiburi." 

 

 

Hadiyth – 6

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  الإسْبَالُ في الإزار ، وَالقَمِيصِ ، وَالعِمَامةِ ، مَنْ جَرَّ شَيْئاً خُيَلاءَ لَمْ ينْظُرِ الله إِلَيْهِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه أَبُو داود والنسائي بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Hatawaangalia wale watu walioburuza nguo zao kama kikoi na kanzu na kilemba kwa kiburi." [Abu Daawuwd na An-Nasaaii kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي جُرَيٍّ جابر بن سُلَيْم رضي الله عنه ، قَالَ : رَأَيْتُ رَجُلاً يَصْدُرُ النَّاسُ عَنْ رَأْيهِ ، لا يَقُولُ شَيْئاً إِلاَّ صَدَرُوا عَنْهُ ، قُلْتُ : مَنْ هَذَا ؟ قالوا : رسولُ الله صلى الله عليه وسلم . قُلْتُ : عَلَيْكَ السَّلامُ يَا رسول الله – مرّتين – قَالَ : ((  لاَ تَقُلْ : عَلَيْكَ السَّلامُ ، عَلَيْكَ السَّلامُ تَحِيَّةُ المَوْتَى ، قُلْ : السَّلامُ عَلَيْكَ )) قَالَ : قُلْتُ : أنْتَ رسول اللهِ ؟ قَالَ : ((  أنَا رسول الله الَّذِي إِذَا أصَابَكَ ضُرٌّ فَدَعَوْتَهُ كَشَفَه عَنْكَ ، وَإِذَا أصَابَكَ عَامُ سَنَةٍ فَدَعَوْتَهُ أَنْبَتَهَا لَكَ ، وَإِذَا كُنْتَ بِأَرْضٍ قَفْرٍ أَوْ فَلاَةٍ فَضَلَّتْ رَاحِلَتُكَ ، فَدَعَوْتَهُ رَدَّهَا عَلَيْكَ )) قَالَ : قُلْتُ : اعْهَدْ إِلَيَّ . قَالَ : ((  لاَ تَسُبَّنَ أحَداً )) قَالَ : فَمَا سَبَبْتُ بَعْدَهُ حُرّاً ، وَلاَ عَبْداً ، وَلاَ بَعِيراً ، وَلاَ شَاةً ، ((  ولاَ تَحْقِرَنَّ مِنَ المَعْرُوفِ شَيْئاً ، وأَنْ تُكَلِّمَ أخَاكَ وَأنْتَ مُنْبَسِطٌ إِلَيْهِ وَجْهُكَ ، إنَّ ذَلِكَ مِنَ المَعْرُوفِ ، وَارْفَعْ إزَارَكَ إِلَى نِصْفِ السَّاقِ ، فَإنْ أبَيْتَ فَإلَى الكَعْبَينِ ، وَإيَّاكَ وَإسْبَالَ الإزَار فَإنَّهَا مِنَ المخِيلَةِ . وَإنَّ اللهَ لاَ يُحِبُّ المَخِيلَةَ ؛ وَإن امْرُؤٌ شَتَمَكَ وعَيَّرَكَ بِمَا يَعْلَمُ فِيكَ فَلاَ تُعَيِّرْهُ بِمَا تَعْلَمُ فِيهِ ، فَإنَّمَا وَبَالُ ذَلِكَ عَلَيْهِ )) رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح ، وقال الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Jurayy Jaabir bin Sulaym (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimuona mtu ambaye rai zake zilikuwa zikikubaliwa na watu wote, alichokuwa akisema kilikuwa kikikubaliwa na watu. Niliuliza: "Ni nani huyu?" Nikaambiwa: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Nikasema: "Amani iwe juu yako ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) - 'Alaykas Salaamu Yaa Rasuulallahi." Nikasema hilo mara mbili. akasema: "Usiseme 'Alaykas Salaamu, kwani 'Alaykas Salaamu ni salamu kwa wafu bali sema: 'As-Salaamu 'Alayka (Amani iwe juu yako)." Akasema (Abu Jurayy): Nikasema: Wewe ni Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Mimi ni Rasuli wa Allaah, ambaye ikiwa umepatikana na dhara aina yoyote nami nikakuombea basi utaondoshewa. Na ikiwa utapatikana katika ardhi yenye ukame (na hakuna kinachomea katika ardhi) nami nikaomba basi mimea itaanza kumea. Na lau utakuwa katika jangwa (lisilokuwa na binadamu wala maji) na kipando chako kikakutoroka, nami nikamuomba Yeye basi Atakurudishia." Nikasema: "Niusie mimi." Akasema: "Usimtusi yeyote." Akasema: "Sikuwahi kumtusi yeyote baada ya hapo, si muungwana wala mtumwa wala ngamia wala mbuzi." Akasema tena: "Usichukie kufanya wema aina yeyote; na unapozungumza na nduguyo basi zungumza naye kwa uso wa bashasha, hakika hilo ni katika wema. Na inyanyue izari (kikoi) yako mpaka katika muundi, ikiwa hutaweza basi juu ya fundo mbili (za miguu). Na nakuonya wewe usiwe ni mwenye kuburuza izari yako kwani hiyo ni ishara ya kiburi. Na hakika Allaah hampendi mwenye kiburi. Na ikiwa mtu atakutukana na kukulaumu na kukupakazia na makosa, kwa anayoyajua lakini wewe usimlaumu kwa makosa aliyo nayo kwa sababu yeye ndiye atakaye chukuliwa hatua kwa makosa yake hapa duniani na kesho Aakhera." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : بينما رَجُلٌ يُصَلَّي مسبلٌ إزَارَهُ ، قَالَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  اذْهَبْ فَتَوَضَّأ )) فَذَهَبَ فَتَوَضّأَ ، ثُمَّ جَاءَ ، فَقَالَ : ((  اذْهَبْ فَتَوَضّأ )) فَقَالَ لَهُ رجُلٌ : يَا رسولَ اللهِ ، مَا لَكَ أمَرْتَهُ أنْ يَتَوَضّأَ ثُمَّ سَكَتَّ عَنْهُ ؟ قَالَ : ((  إنّهُ كَانَ يُصَلِّي وَهُوَ مُسْبِلٌ إزَارَهُ ، وَإنَّ اللهَ لاَ يَقْبَلُ صَلاَةَ رَجُلٍ مُسْبلٍ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح عَلَى شرط مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Alipokuwa mtu mmoja anaswali na huku kikoi chake kinaburuza, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Nenda ukashike wudhu." Yule mtu alikwenda akatawadha, kisha akarudi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Nenda ukatawadhe." Mtu mmoja aliyekuwepo akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Kuna nini, kwani umemuamrisha akatawadhe kisha umenyamaza?" Akasema: "Hakika yeye alikuwa anaswali na kikoi chake kinaburuza. Na kwa hakika Allaah haikubali Swalaah ya mtu anayeburuza nguo yake." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh kulingana na sharti ya Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

وعن قيس بن بشر التَّغْلِبيِّ ، قَالَ : أخْبَرَني أَبي - وكان جَلِيساً لأَبِي الدرداء - قَالَ : كَانَ بِدمَشْق رَجُلٌ مِنْ أصْحَابِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم يقال لَهُ سهل بن الْحَنْظَلِيَّةِ ، وَكَانَ رَجُلاً مُتَوَحِّداً قَلَّمَا يُجَالِسُ النَّاسَ ، إنَّمَا هُوَ صَلاَةٌ ، فإذا فَرَغَ فَإنَّمَا هُوَ تَسْبِيحٌ وَتَكْبيرٌ حَتَّى يَأتي أهْلَهُ ، فَمَرَّ بنا وَنَحْنُ عِنْدَ أَبي الدَّرداء ، فَقَالَ لَهُ أَبُو الدرداءِ : كَلِمَةً تَنْفَعُنَا وَلاَ تَضُرُّكَ . قَالَ : بَعَثَ رسول الله صلى الله عليه وسلم سَرِيَّةً فَقَدِمَتْ ، فَجَاءَ رَجُلٌ مِنْهُمْ فَجَلَسَ في المَجْلِسِ الَّذِي يَجْلِسُ فِيهِ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ لِرَجُلٍ إِلَى جَنْبِهِ : لَوْ رَأيْتَنَا حِيْنَ التَقَيْنَا نَحْنُ وَالعَدُوُّ ، فَحَمَلَ فُلانٌ وَطَعَنَ ، فَقَالَ : خُذْهَا مِنِّي ، وَأنَا الغُلاَمُ الغِفَاريُّ ، كَيْفَ تَرَى في قَوْلِهِ ؟ قَالَ : مَا أرَاهُ إِلاَّ قَدْ بَطَلَ أجْرُهُ . فَسَمِعَ بِذلِكَ آخَرُ ، فَقَالَ : مَا أرَى بِذلِكَ بَأساً ، فَتَنَازَعَا حَتَّى سَمِعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ: (( سُبْحَانَ الله ؟ لاَ بَأسَ أنْ يُؤجَرَ وَيُحْمَدَ )) فَرَأَيْتُ أَبَا الدَّرْدَاء سُرَّ بِذلِكَ ، وَجَعَلَ يَرْفَعُ رَأسَهُ إِلَيْهِ ، وَيَقُولُ : أأنْتَ سَمِعْتَ ذَلِكَ مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ؟ فيقول : نَعَمْ ، فما زال يُعِيدُ عَلَيْهِ حَتَّى إنّي لأَقُولُ لَيَبْرُكَنَّ عَلَى رُكْبَتَيْهِ ، قَالَ : فَمَرَّ بِنَا يَوْماً آخَرَ ، فَقَالَ لَهُ أَبُو الدَّرْداء : كَلِمَةً تَنْفَعُنَا وَلاَ تَضُرُّكَ ، قَالَ : قَالَ لنا رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( المُنْفِقُ عَلَى الخَيْلِ ، كَالبَاسِطِ يَدَهُ بالصَّدَقَةِ لاَ يَقْبضُهَا )) ، ثُمَّ مَرَّ بِنَا يَوماً آخَرَ ، فَقَالَ لَهُ أَبُو الدَّرْداء : كَلِمَةً تَنْفَعنَا وَلاَ تَضُرُّكَ ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( نِعْمَ الرَّجُلُ خُرَيمٌ الأسَديُّ ! لولا طُولُ جُمَّتِهِ وَإسْبَالُ إزَارِهِ! )) فَبَلَغَ ذَلِكَ خُرَيْماً فَعَجَّلَ، فَأَخَذَ شَفْرَةً فَقَطَعَ بِهَا جُمَّتَهُ إِلَى أُذُنَيْهِ ، وَرَفَعَ إزارَهُ إِلَى أنْصَافِ سَاقَيْهِ . ثُمَّ مَرَّ بِنَا يَوْماً آخَرَ فَقَالَ لَهُ أَبُو الدَّرْداء : كَلِمَةً تَنْفَعُنَا وَلاَ تَضُرُّكَ ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  إنَّكُمْ قَادِمُونَ عَلَى إخْوانِكُمْ ، فَأصْلِحُوا رِحَالكُمْ ، وَأصْلِحُوا لِبَاسَكُمْ حَتَّى تَكُونُوا كَأنَّكُمْ شَامَةٌ في النَّاسِ ؛ فإِنَّ الله لاَ يُحِبُّ الفُحْشَ وَلاَ التَّفَحُّش )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ حسنٍ ، إِلاَّ قيس بن بشر فاختلفوا في توثِيقِهِ وَتَضْعِيفِهِ ، وَقَدْ روى لَهُ مسلم .

Qays bin Bishr At-Taghlibiy amesema: Amenipasha habari mimi baba yangu ambaye alikuwa ni sahibu wa Abu Dardaa' (Radhwiya Allaahu 'anhu). Alisema: Kulikuwa na mtu Damascus aliyekuwa Swahaaba wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akijulikana kwa jina la Sahl bin Al-Handhaliyyah (Radhwiya Allaahu 'anhu). Na alikuwa ni mtu mwenye kupenda upweke na kujitenga na watu na hivyo hakukaa sana nao. Hakika alitumia muda wake mwingi katika Swalaah na alipomaliza kuswali basi alikuwa akijishughulisha katika kumtaja Allaah kwa kuleta Tasbihi (kusema Subhaana Allaah) na Takbira (Allaahu Akbar) mpaka familia yake wanapokuja kwa mahitaji yao. tulikuwa na Abu Dardaa' siku moja naye akawa anapita tukiwa tumekaa. Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) Akasema: "Tuambie neno ambalo litatufaa sisi wala halitakudhuru wewe." Akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma kikosi cha Mujahidina nacho baada ya muda kikarudi (baada ya kumaliza shughuli waliyotmwa nayo). Akaja mtu mmoja miongoni mwao na kukaa katika baraza ambayo anakaa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Huyu mtu alimwambia mwenziwe aliyekuwa ubavuni mwake: 'Lau ungetuona sisi tulipopambana na maadui. Mmoja wao (kafiri) alichukua fumo (mkuki) na kumchoma nao Muislamu, Na ambaye alisema na hakika mimi ni kijan wa Ghifari. Je, waonaje katika kauli yake hiyo?' Akasema: 'Nadhani kuwa amekosa ujira wake kwa ajili wa kujisifu.' Akasikia hayo mtu mwengine, naye akasema: 'sioni tatizo lolote katika hilo.' Walianza kubishana katika hilo mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasikia, ambaye alisema: 'Ametakasika Allaah! Hakuna madhara yoyote kwa yeye kupatiwa ujira Kesho Aakherah na kumsifu hapa duniani.' Nikamuona Abu Dardaa' amefurahia kusikia hayo. Akawa anayanyua kichwa chake kwake na kusema: 'Wewe umesikia hayo kutoka kwa Rasuli wa Allaah?' Akasema: 'Ndio.' Akawa anaendelea kulikariri hilo swali mpaka nikamwambia kwa nini unamchagiza sana. Akasema (Bishr): Akapita tena siku nyengine, naye Abu Dardaa' akamuuliza: "Twambie neno ambalo litatufaa sisi wala halitakudhuru wewe." Akasema: "Alituambia Rausli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 'Mwenye kutoa ili kumlisha chakula farasi (anayeandaliwa kwa jihadi katika njia ya Allaah) ni kama aliyeuacha wazi mkono wake kwa kutoa swadaqah na wala hakuufunga (anatoa bila ya kubana)." Kisha akapita tena siku nyengine, Abu Dardaa' akamuuliza tena: "Twambie neno ambalo litatufaa sisi wala halitakudhuru wewe." Akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 'Khuraym Al-Asadiy ni mtu bora na mzuri lau si kwa nywele zake ndefu na kuburuza kikoi chake.' Habari hizo zilipomfikia khuraym, hapo hapo alizikata nywele zake na kufika masikioni na akakinyanyua kikoi chake mpaka kikafika nusu ya muundi." Kisha akapita mara nyingine tena na Abu Dardaa' akamwambia: "Twambie neno ambalo litatufaa sisi wala halitakudhuru wewe." Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika nyinyi munarudi kwa ndugu zenu, hivyo tengenezeni vipando vyenu na nguo zenu mpaka muwe katika hali ya ustahifu miongoni mwa watu. Hakika Allaah hapendi ujuvi wala uchakavu." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan isipokuwa Qays bin Bishr, ambaye wametofautiana katika kumwamini na kumdhoofisha. Na hakika Muslim amepokea kutoka kwake]. 

 

 

Hadiyth – 10

وعن أَبي سعيد الخدريِّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  إزْرَةُ المُسْلِمِ إِلَى نِصْفِ السَّاقِ ، وَلاَ حَرَجَ – أَوْ لاَ جُنَاحَ – فِيمَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الكَعْبَيْنِ ، فمَا كَانَ أسْفَلَ مِنَ الكَعْبَيْنِ فَهُوَ في النَّارِ ، وَمَنْ جَرَّ إزَارَهُ بَطَراً لَمْ يَنْظُرِ اللهُ إِلَيْهِ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيحٍ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iid Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kikoi cha Muislamu kinatakiwa kifike nusu muundi wala hapana tatizo lolote urefu wake ukiwa baina ya nusu muundi na nguyu zake mbili. Chochote kitakachokuwa chini ya nguyu mbili kitakuwa motoni. Allaah Hatamuangali kabisa mwenye kuburuza kikoi chake kwa kiburi." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]

 

 

Hadiyth – 11

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : مررتُ عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم وفي إزَارِي استرخاءٌ ، فَقَالَ : ((  يَا عَبدَ اللهِ ، ارْفَعْ إزَارَكَ )) فَرَفَعْتُهُ ثُمَّ قَالَ : ((  زِدْ )) فَزِدْتُ ، فَمَا زِلْتُ أتَحَرَّاهَا بَعْدُ . فَقَالَ بَعْضُ القَوْم : إِلَى أينَ ؟ فَقَالَ : إِلَى أنْصَافِ السَّاقَيْنِ . رواه مسلم .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Nilipita mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kikoi changu kinaning'inia. Akasema: "Ee 'Abdallaah! Kipandishe Kikoi chako." Nami nikakipandisha. Kisha akasema: "Zidisha." Nami nikakipandisha tena na kuanzia wakati huo nikawa navaa kikiwa juu. Wakasema baadhi ya watu: "Juu mpaka wapi?" Akasema: "Mpaka nusu muundi." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 12

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاءَ لَمْ يَنْظُرِ اللهُ إِلَيْهِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) فَقَالَتْ أُمُّ سَلَمَةَ : فَكَيْفَ تَصْنَعُ النِّسَاءُ بذُيُولِهِنَّ ؟ قَالَ : ((  يُرْخِينَ شِبْراً )) قالت : إِذَاً تَنْكَشِفُ أقْدَامُهُنَّ . قَالَ : ((  فَيرخِينَهُ ذِرَاعاً لاَ يَزِدْنَ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi, Allaah hatamuangalia siku ya Qiyaamah." Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) akauliza: "Hivyo watafanyaje wanawake kwa marinda (sketi) yao?" Akasema: "Waziteremshe shibiri." (Ummu Salamah) akauliza: "Hivyo, miguu yao itaonekana." Akasema: "Waziteremshe dhiraa na wala wasizidishe zaidi ya hapo." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

 

 

Share