04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Anachosema Mwenye Kukata Tamaa ya Maisha Yake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقوله مَن أيس من حياته
04-Mlango Wa Anachosema Mwenye Kukata Tamaa ya Maisha Yake
Hadiyth – 1
عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : سَمِعْتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ مُسْتَنِدٌ إلَيَّ ، يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وارْحَمْنِي ، وأَلْحِقْنِي بالرَّفِيقِ الأَعْلَى )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipokuwa amejipumzisha juu yake (kabla ya kuaga kwake dunia) akisema: "Ee Mola wangu! Nisamehe na unirehemu na unikutanishe na Rafiki yangu (Mtukufu) Aliye juu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : رَأيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ بِالمَوْتِ ، عِنْدَهُ قَدَحٌ فِيهِ مَاءٌ ، وَهُوَ يُدْخِلُ يَدَهُ في القَدَحِ ، ثُمَّ يَمْسَحُ وَجْهَهُ بالماءِ ، ثُمَّ يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ أعِنِّي عَلَى غَمَرَاتِ المَوْتِ أَوْ سَكَرَاتِ المَوْتِ )) رواه الترمذي .
Na amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa katika hali ya mauti. Alikuwa na kikombe cha maji anatia mkono wake ndani yake, kisha anapangusa uso wake na maji. Kisha anasema: "Ee Mola wangu! Nipunguzie ulevi wa mauti, na uchungu kwani mauti yana ulevi." [At-Tirmidhiy]