05-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwausia Watu wa Familia Yenye Mgonjwa na Wanaomuangalia Kumfanyia Wema na Kumfanyia Hisani Aliye katika Uchungu wa Mauti au Aliyehukumiwa Kunyongwa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب وصية أهل المريض
ومن يخدمه بالإحسان إليه واحتماله والصبر عَلَى مَا يشق من أمره
وكذا الوصية بمن قرب سبب موته بحد أَوْ قصاص ونحوهما
05-Mlango Wa Kuwausia Watu wa Familia Yenye Mgonjwa na Wanaomuangalia Kumfanyia Wema na Kumfanyia Hisani Aliye katika Uchungu wa Mauti au Aliyehukumiwa Kunyongwa
عن عِمْران بن الحُصَيْنِ رضي الله عنهما : أنَّ أمْرَأَةً مِنْ جُهَيْنَةَ أتَت النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَهِيَ حُبْلَى مِنَ الزِّنَا ، فَقَالَتْ : يَا رسول الله ، أصَبْتُ حَدّاً فَأقِمْهُ عَلَيَّ ، فَدَعَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَلِيَّهَا ، فَقَالَ : (( أحْسِنْ إِلَيْهَا ، فَإذَا وَضَعَتْ فَأتِنِي بِهَا )) فَفَعَلَ ، فَأمَرَ بِهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ، فَشُدَّتْ عَلَيْهَا ثِيَابُهَا ، ثُمَّ أمَرَ بِهَا فَرُجِمَت ، ثُمَّ صَلَّى عَلَيْهَا . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba mwanamke wa kabila la Juhaynah alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na mimba ya zinaa, akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! MImi nimezini hivyo nisimamishie adhabu." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwita walii wake akamwambia: "Mtendee wema, atakapozaa mlete kwangu' Akafanya hivyo. Nabiy aliamuru afungwe kwa nguo zake, kisha akaamuru apigwe mawe. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamswalia (Swala ya Jeneza)." [Muslim]