06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuruhusiwa Mgonjwa Kusema: Ninaumwa au Ninaumwa Sana, Lakini ni Karaha Kusema Hivyo kwa Kukata Tamaa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب جواز قول المريض : أنَا وجع ، أَوْ شديد الوجع
أَوْ مَوْعُوكٌ أَوْ وارأساه ونحو ذلك . وبيان أنَّه لا كراهة في ذلك
إِذَا لَمْ يكن عَلَى سبيل التسخط وإظهار الجزع
06-Mlango Wa Kuruhusiwa Mgonjwa Kusema: Ninaumwa au Ninaumwa Sana, Lakini ni Karaha Kusema Hivyo kwa Kukata Tamaa
Hadiyth – 1
عن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : دَخَلْتُ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُوعَكُ ، فَمَسسْتُهُ ، فَقلتُ : إنَّكَ لَتُوعَكُ وَعَكاً شَديداً ، فَقَالَ : (( أجَلْ ، إنِّي أُوعَكُ كَمَا يُوعَكُ رَجُلانِ مِنْكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba, nilimzuru Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipokuwa na homa, nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wewe una homa kali." Akasema: "Ndio, mimi huumwa kwa maumivu yaliyo sawa na watu wawili miongoni mwenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن سعدِ بن أَبي وقاصٍ رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يَعُودُنِي مِنْ وَجَعٍ اشْتَدَّ بِي ، فقلتُ: بَلَغَ بِي مَا تَرَى ، وَأنَا ذُو مَالٍ ، وَلاَ يَرِثُنِي إِلاَّ ابْنَتِي .. وذَكر الحديث . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Waqqaas amesema kwamba: "Alikuja kunizuru mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikiwa mgonjwa sana." Nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Umenifikia mimi ugonjwa huu kama unavyoniona na mimi ni tajiri na hakuna anayenirithi isipokuwa binti yangu mmoja"... Na akaitaja Hadiyth. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن القاسم بن محمد، قَالَ : قالت عائشةُ رضي الله عنها : وَارَأسَاهُ ! فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( بَلْ أنَا ، وَارَأسَاهُ ! )) ... وذكر الحديث . رواه البخاري .
Na imepokewa kutoka kwa Al-Qaasim bin Muhammad kwamba 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alisema: "Ah, kichwa changu." Hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Bali, ni kichwa changu"... Na akaitaja Hadiyth. [Al-Bukhaariy]