03-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Adabu za Safari na Kuteremka na Kupumzika Usiku Kuwahurumia Wanyama na Kuchunga Maslahi Yao na Haki Zao na Kufaa Kulala Juu ya Mnyama Ikiwa Anaweza Jambo Hilo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب آداب السير والنـزول والمبيت
والنوم في السفر واستحباب السُّرَى والرفق بالدواب
ومراعاة مصلحتها وأمر من قصّر في حقها بالقيام بحقها
وجواز الإرداف عَلَى الدابة إِذَا كانت تطيق ذلك
03-Mlango Wa Adabu za Safari na Kuteremka na Kupumzika Usiku Kuwahurumia Wanyama na Kuchunga Maslahi Yao na Haki Zao na Kufaa Kulala Juu ya Mnyama Ikiwa Anaweza Jambo Hilo
Hadiyth – 1
عن أَبي هُريرةَ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا سَافَرْتُمْ فِي الخِصْبِ ، فَأعْطُوا الإبلَ حَظَّهَا مِنَ الأَرْضِ ، وَإِذَا سَافَرْتُمْ في الجدْبِ ، فَأسْرِعُوا عَلَيْهَا السَّيْرَ ، وَبَادِرُوا بِهَا نِقْيَهَا ، وَإِذَا عَرَّسْتُمْ ، فَاجْتَنِبُوا الطَّرِيقَ ؛ فَإنَّهَا طُرُقُ الدَّوَابِّ ، وَمَأوَى الهَوَامِّ بِاللَّيْلِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mnapo safiri katika ardhi yenye rutuba wapatieni ngamia wenu haki yao kutoka katika ardhi na mnapo safiri kwenye jangwa nendeni nao haraka sana harakisheni kuhifadhi nguvu zao. Na mnapo simama usiku kwa ajili ya kupumzika, jiepusheni na barabara kwani hiyo ni njia ya wanyama na mapumziko ya wadudu wengine usiku." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي قتادة رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا كَانَ فِي سَفَرٍ ، فَعَرَّسَ بِلَيْلٍ اضْطَجَعَ عَلَى يَمِينهِ ، وَإِذَا عَرَّسَ قُبَيلَ الصُّبْحِ نَصَبَ ذِرَاعَهُ ، وَوَضَعَ رَأسَهُ عَلَى كَفِّهِ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa safarini, akalala usiku hulalia ubavu wake wa kulia. Na akilala karibu na asubuhi, anasimamisha dhiraa yake, na anaweka kichwa chake katika kiganja chake. [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( عَلَيْكُمْ بِالدُّلْجَةِ ، فَإنَّ الأرْضَ تُطْوَى بِاللَّيْلِ )) رواه أَبُو داود بإسناد حسن .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Safirini usiku kwani ardhi (masafa) hufupishwa usiku." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]
Hadiyth – 4
وعن أَبي ثَعْلَبَةَ الخُشَنِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ النَّاسُ إِذَا نَزَلُوا مَنْزِلاً تَفَرَّقُوا في الشِّعَابِ وَالأوْدِيَةِ . فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ تَفَرُّقكُمْ فِي هذِهِ الشِّعَابِ وَالأوْدِيَةِ إنَّمَا ذلِكُمْ مِنَ الشَّيْطَانِ ! )) فَلَمْ يَنْزِلُوا بَعْدَ ذَلِكَ مَنْزِلاً إِلاَّ انْضَمَّ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ . رواه أَبُو داود بإسناد حسن .
Imepokewa kwake Abu Tha'labah Al-Khushaniy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Watu walikuwa wanaposhuka mahali (sehemu) wanatawanyika, katika vichaka na mabonde. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Hakika kutawanyika kwenu kwenye vichaka na mabonde ni jambo kutoka kwa shetani." Kwa hiyo hakushuka mahali baada ya hapo, isipokuwa watapoungana baadhi yao na wengine. [Abu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]
Hadiyth – 5
وعن سهل بن عمرو – وقيل : سهل بن الربيع بن عمرو الأنصاري المعروف بابن الحنظلِيَّة ، وَهُوَ من أهل بيعة الرِّضْوَانِ رضي الله عنه ، قَالَ : مَرَّ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بِبَعِيرٍ قَدْ لَحِقَ ظَهْرُهُ بِبَطْنِهِ ، فَقَالَ : (( اتَّقُوا الله في هذِهِ البَهَائِمِ المُعجَمَةِ ، فَارْكَبُوهَا صَالِحَةً ، وَكُلُوهَا صَالِحَةً )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwake Sahl bin 'Amruw - na inasemwa Sahl bin A-Rabii' bin 'Amruw Al-Answaariy maarufu Ibnil Handhaliyyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) naye ni katika watu wa ba'iah Ridhwaan (kabla ya Hudaybiyah) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita kwenye ngamia ambaye tumbo lake limeshikana na mgongo wake (amekondeana). Akasema: "Mcheni Allaah katika hawa wanyama wasiozungumza. Wapandeni wakiwa wazima, na kuleni nyama zake wakiwa wazima." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 6
وعن أَبي جعفر عبد الله بن جعفر رضي الله عنهما ، قَالَ : أردفني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ خَلْفَهُ ، وَأسَرَّ إليَّ حَدِيثاً لا أُحَدِّثُ بِهِ أحَداً مِنَ النَّاسِ ، وَكَانَ أحَبَّ مَا اسْتَتَرَ بِهِ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم لِحاجَتِهِ هَدَفٌ أَوْ حَائِشُ نَخْلٍ . يَعنِي : حَائِطَ نَخْلٍ . رواه مسلم هكَذَا مُختصراً .
وزادَ فِيهِ البَرْقاني بإسناد مسلم - بعد قَوْله : حَائِشُ نَخْلٍ - فَدَخَلَ حَائِطاً لِرَجُلٍ مِنَ الأنْصَارِ ، فَإذا فِيهِ جَمَلٌ ، فَلَمَّا رَأى رَسولَ الله صلى الله عليه وسلم جَرْجَرَ وذَرَفَتْ عَيْنَاهُ ، فَأتَاهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَمَسَحَ سَرَاتَهُ - أيْ : سِنَامَهُ - وَذِفْرَاهُ فَسَكَنَ ، فَقَالَ : (( مَنْ رَبُّ هَذَا الجَمَلِ ؟ لِمَنْ هَذَا الجَمَلُ ؟ )) فَجَاءَ فَتَىً مِنَ الأنْصَارِ ، فَقَالَ : هَذَا لِي يَا رسولَ الله . قَالَ : (( أفَلاَ تَتَّقِي اللهَ في هذِهِ البَهِيمَةِ الَّتي مَلَّكَكَ اللهُ إيَّاهَا ؟ فَإنَّهُ يَشْكُو إلَيَّ أنَّكَ تُجِيعُهُ وتُدْئِبُهُ )) رواه أَبُو داود كرواية البرقاني .
Abu Ja'far 'Abdillaah bin Ja'far (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinikalisha siku moja nyuma yake akaninog'oneza maneno sitamueleza yoyote katika watu. Na alichopenda zaidi kujisitiri nacho Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa haja zake ilikuwa ni nyuma ya ukuta au ukuta wa mtende. [Muslim]
Na ameongeza Al-Barqaaniy ameongeza katika Isnaad ya Muslim baada ya kauli yake: Ukuta wa mtende, akaingia katika bustani la mtu miongoni mwa Answari kupitia katika ukuta wake, hapo akakuta ngamia. Ngamia huyo alipomuona Rasuli wa Allaah (Swalla allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akagumia na kububujikwa machozi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuendea akampapasa nundu yake, Ngamia akatulia. akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni nani bwana wa ngamia huyu?, Ngamia huyu ni wa nani?" Akaja kijana wa Ki-Answaar akasema: "Ni wangu, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Humuogopi Allaah katika hawa wanyama ambao Allaah amekumilikisha? Kwani yeye amenishtakia kuwa wewe unakalisha njaa na unamtabisha." [Abu Daawuwd ameipokea kama riwaayah ya Al-Barqaaniy]
Hadiyth – 7
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : كُنَّا إِذَا نَزَلْنَا مَنْزِلاً ، لاَ نُسَبِّحُ حَتَّى نَحُلَّ الرِّحَال . رواه أَبُو داود بإسناد عَلَى شرط مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa tulikuwa tunashuka mahali hatuswali hadi kwanza tufungue vipando." [Abu Daawuwd kwa Isnaad kwa sharti ya Muslim]