04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kumsaidia Rafiki

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب إعانة الرفيق

04-Mlango Wa Kumsaidia Rafiki

 

Alhidaaya.com

 

 

Katika Safari Zipo Hadiyth nyingi katika mlango huu ambazo tumetangulia kuzitaja, kama: "Na Allaah anamsaidia mja maadamu mja yu katika kumsaidia nduguye." Na Hadiyth: "Kila jema ni swadaqa", na mfano wake.

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي سعيد الخدري رضي اللهُ عنه ، قَالَ : بَيْنَمَا نَحْنُ في سَفَرٍ إذْ جَاءَ رَجُلٌ عَلَى رَاحِلَةٍ لَهُ ، فَجَعَلَ يَصْرِفُ بَصَرَهُ يَمِيناً وَشِمَالاً ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ كَانَ مَعَهُ فَضْلُ ظَهْرٍ فَلْيَعُدْ بِهِ عَلَى مَنْ لاَ ظَهْرَ لَهُ ، وَمَنْ كَانَ لَهُ فَضْلُ زَادٍ فَلْيَعُدْ بِهِ عَلَى مَنْ لاَ زَادَ لَهُ )) ، فَذَكَرَ مِنْ أصْنَافِ المَالِ مَا ذَكَرَهُ ، حَتَّى رَأيْنَا ، أنَّهُ لاَ حَقَّ لأَحَدٍ مِنَّا فِي فَضْلٍ . رواه مسلم .

Imepokewa kwa Abu Sa'iid Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa safarini pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja mtu juu ya kipando chake, akawa anageuza jicho lake kulia na kushoto. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mwenye kipando cha zaidi ampe asiyekuwa nacho." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akataja aina za mali mpaka tukadhani kuwa hakuna haki kwa mmoja wetu kuwa na ziada katika chochote." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن جابر رضي اللهُ عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم : أنَّهُ أرَادَ أنْ يَغْزُوَ ، فَقَالَ : ((  يَا مَعْشَرَ المُهَاجِرِينَ وَالأَنْصَارِ ، إن مِنْ إخْوَانِكُمْ قَوْماً لَيْسَ لَهُمْ مَالٌ ، وَلاَ عَشِيرةٌ ، فَلْيَضُمَّ أحَدكُمْ إِلَيْهِ الرَّجُلَيْنِ أَو الثَّلاَثَةَ ، فَمَا لأَحَدِنَا مِنْ ظَهْرٍ يَحْمِلُهُ إِلاَّ عُقْبةٌ كَعُقْبَةٍ )) يَعْني أحَدهِمْ ، قَالَ : فَضَمَمْتُ إلَيَّ اثْنَيْنِ أَوْ ثَلاَثَةً مَا لِي إِلاَّ عُقْبَةٌ كَعقبة أحَدِهِمْ مِنْ جَمَلِي . رواه أَبُو داود .

Imepokewa kutoka kwake Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipotaka kwenda katika vita alikuwa anatuambia: "Enyi kongamano la Muhajirina na Answaar! Hakika wapo miongoni mwenu ndugu zenu kaumu ambao hawana mali wala familia, hivyo kila mmoja wenu achukue watu wawili au watatu kwa sababu ya upungufu wa vipandio (wanyama wa kupanda), na kila mmoja apande kwa zamu. Nami niliunganisha watu wawili au watatu miongoni mwao na kushirikiana kwa zamu sawasawa katika kumpanda ngamia wangu." [Abu Daawuwd]

 

 

Hadiyth – 3

وعن جابر رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَتَخَلَّفُ في المَسير ، فَيُزْجِي الضَّعِيف ، وَيُرْدِفُ وَيَدْعُو لَهُ . رواه أَبُو داود بإسناد حسن .

Kutoka kwake Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa nyuma ya msafara, akisaidia wanyonge, na kubeba wanaotembea kwa miguu, na kuwaombea. [Abu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]

 

 

 

 

Share