05-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Unachosema Unapopanda Mnyama kwa Ajili ya Safari
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقول إذا ركب دَابَّة للسفر
05-Mlango Wa Unachosema Unapopanda Mnyama kwa Ajili ya Safari
قَالَ الله تَعَالَى :
وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْفُلْكِ وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ﴿١٢﴾
Na Akakufanyieni katika merikebu na wanyama mnaowapanda.
لِتَسْتَوُوا عَلَىٰ ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ﴿١٣﴾
Ili mlingamane sawasawa juu ya mgongo wake, kisha mkumbuke neema ya Rabb wenu mtakapolingamana sawasawa juu yao, na mseme: Utakasifu ni wa (Allaah) Ambaye Ametutiishia haya, na tusingeliweza wenyewe kumdhibiti.
وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ﴿١٤﴾
Na hakika kwa Rabb wetu, bila shaka tutarejea. [Az-Zukhruf: 12-14]
Hadiyth – 1
وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا اسْتَوَى عَلَى بَعِيرِهِ خَارِجاً إِلَى سَفَرٍ ، كَبَّرَ ثَلاثاً ، ثُمَّ قَالَ : (( سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلبُونَ . اللّهُمَّ إنا نسألكَ في سفرنا هذا البرّ والتَّقوى ، ومنَ العملِ ما ترضى ، اللَّهُمَّ هَوِّن عَلَيْنَا سَفَرَنَا هَذَا ، وَاطْوِ عَنَّا بُعْدَهُ . اللَّهُمَّ أنْتَ الصَّاحِبُ في السَّفَرِ ، والخَلِيفَةُ في الأهْلِ . اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنْ وَعْثَاءِ السَّفَرِ ، وَكَآبَةِ المَنْظَرِ ، وَسُوءِ المُنْقَلَبِ في المالِ وَالأَهْلِ وَالوَلَدِ )) وَإِذَا رَجَعَ قَالَهُنَّ وَزَادَ فِيهِنَّ : (( آيِبُونَ ، تَائِبُونَ ، عَابِدُونَ ، لِرَبِّنَا حَامِدُونَ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapokaa sawa juu ya ngamia wake akiwa anaenda safari hupiga Takbira mara tatu, kisha anasema Utukufu ni wa ambaye ametudhalilishia hiki na hatukuwa wenye kukipanda, na hakika sisi kwa Rabb wetu ni wenye kurudi. Ee Rabb wetu hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na ucha-Mungu, na katika matendo unayoyaridhia, Ee Rabb turahisishie safari yetu hii, na tukunjie umbali wake. Ee Rabb Wewe ni rafiki safarini, na Mwangalizi katika familia, Ee Rabb mimi nataka hifadhi Kwako ya mashaka ya safari, na mandhari yenye huzuni, na ubaya wa kurejea katika mali na mke na watoto." Alipokuwa anarudi safarini aliyasema na kuongeza ndani yake: "Aayibuuna Taa'ibuna 'Aabiduuna LiRabbina Haamiduuna - Sisi ni wenye kurejea kwenye kutubia wenye kumuabudu Rabb wenye kumsifu." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عبد الله بن سَرجِسَ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا سَافَرَ يَتَعَوَّذُ مِنْ وَعْثَاءِ السَّفَرِ ، وَكَآبَةِ المُنْقَلَبِ ، وَالْحَوْرِ بَعْدَ الكَوْنِ ، وَدَعْوَةِ المَظْلُومِ ، وَسُوءِ المَنْظَرِ في الأَهْلِ وَالمَالِ . رواه مسلم .
'Abdillaah bin Sarjis (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisafiri huomba hifadhi kutokana na mashaka ya safari, huzuni ya kurejea, na hasara baada ya faida, na maombi ya mwenye kudhulumiwa, na ubaya wa mandhari katika mke na mali. [Muslim]
Hadiyth – 3
عن عَلِي بن ربيعة ، قَالَ : شهدت عليَّ بن أَبي طالب رضي الله عنه ، أُتِيَ بِدَابَّةٍ لِيَرْكَبَهَا ، فَلَمَّا وَضَعَ رِجْلَهُ في الرِّكَابِ ، قَالَ : بِسْمِ اللهِ ، فَلَمَّا اسْتَوَى عَلَى ظَهْرِهَا ، قَالَ : الحَمْدُ للهِ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ ، ثُمَّ قَالَ : الحمْدُ للهِ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، ثُمَّ قَالَ : اللهُ أكْبَرُ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، ثُمَّ قَالَ : سُبْحَانَكَ إنّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي إنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ ، ثُمَّ ضَحِكَ ، فَقيلَ : يَا أمِيرَ المُؤمِنِينَ ، مِنْ أيِّ شَيْءٍ ضَحِكْتَ ؟ قَالَ : رَأيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم فَعَلَ كَمَا فَعَلْتُ ثُمَّ ضَحِكَ ، فقُلْتُ : يَا رسول اللهِ ، مِنْ أيِّ شَيْءٍ ضَحِكْتَ ؟ قَالَ : (( إنَّ رَبَّكَ تَعَالَى يَعْجَبُ مِنْ عَبدِهِ إِذَا قَالَ : اغْفِرْ لِي ذُنُوبِي ، يَعْلَمُ أنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ غَيْرِي )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن ))، وفي بعض النسخ: (( حسن صحيح )) . وهذا لفظ أَبي داود .
'Aliy bin Rabiy’ah (رضي الله عنه) amesema: Nimemshuhudia 'Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه) akiletewa mnyama ampande. Alipoweka mguu wake kwenye kipando alisema:
بِسْمِ اللهِ
Alipolingana juu ya mgongo wake alisema:
الحَمْدُ للهِ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ
Kisha akasema:
الحمْدُ للهِ
AlhamduliLlaah (Himdi Anastahiki Allaah) mara tatu.
Kisha akasema:
اللهُ أكْبَرُ
Allaahu Akbar (Allaah Ni Mkubwa) mara tatu.
Kisha akasema:
سُبْحَانَكَ إنّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي إنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ
Subhaanak inniy dhwalamtu nafsiy Faghfirliy, innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta.
Kutakasika ni Kwako, hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu, basi Nighufurie, kwani hakuna mwenye kughufuria dhambi ila Wewe.
Kisha akacheka. Akaulizwa: Ee Amiri wa Waumini! Unacheka nini?
Akasema: Nilimuona Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya kama nilivyofanya, kisha akacheka. Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Unacheka nini? Akasema: “Hakika Rabb wako Anamridhia mja Wake anaposema: Nighufurie dhambi zangu, anajua kuwa hakuna anayeghufuria dhambi isipokuwa Yeye (Allaah).”
[Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, amesema ni Hadiyth Hasan. Na katika baadhi ya mapokezi ni Hadiyth Hasan Swahiyh, na hii ni lafdhi ya Abuu Daawuwd]