06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Msafiri Anatakiwa Kutoa Takbira Anapopanda na Kutoa Tasbihi Anaposhuka na Kubwa na Mfano Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تكبير المسافر إِذَا صعد الثنايا وشبهها وتسبيحه إِذَا هبط الأودية ونحوها

والنهي عن المبالغة برفع الصوتِ بالتكبير ونحوه

06-Mlango Wa Msafiri Anatakiwa Kutoa Takbira Anapopanda na Kutoa Tasbihi Anaposhuka na Kubwa na Mfano Wake

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن جابر رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كُنَّا إِذَا صَعِدْنَا كَبَّرْنَا ، وَإِذَا نَزَلْنَا سَبَّحْنَا . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) Amesema: Tulipokuwa tunapanda tulikuwa tunapiga Takbira na tunaposhuka tunatoa Tasbihi (Subhana Allaah). [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمرَ رضي اللهُ عنهما ، قَالَ : كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم وجيُوشُهُ إِذَا عَلَوا الثَّنَايَا كَبَّرُوا ، وَإِذَا هَبَطُوا سَبَّحُوا . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na jeshi lake walikuwa wakipanda kilima wanaleta Takbira na waliposhuka wakitoa Tasbihi. [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمرَ رضي اللهُ عنهما ، قَالَ : كَانَ النَّبي صلى الله عليه وسلم إِذَا قَفَلَ مِنَ الحَجِّ أَوْ العُمْرَةِ ، كُلَّمَا أوْفَى عَلَى ثَنِيَّةٍ أَوْ فَدْفَدٍ كَبَّرَ ثَلاثَاً ، ثُمَّ قَالَ : ((  لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ . آيِبُونَ ، تَائِبُونَ ، عَابِدُونَ ، سَاجِدُونَ ، لِرَبِّنَا حَامِدُونَ ، صَدَقَ اللهُ وَعْدَهُ ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ ، وَهَزَمَ الأحْزَابَ وَحْدَهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية لمسلم : إِذَا قَفَلَ مِنَ الجيُوشِ أَو السَّرَايَا أَو الحَجِّ أَو العُمْرَةِ .

Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anaporudi Hijjah au 'Umrah alikuwa kila anapopanda kilima au mwinuko anapiga Takbira mara tatu, kisha anasema: "Hapana Mola ila Allaah tu hana mshirika. sisi ni wenye kurejea wenye kutubia wenye kumwabudu wenye kumsujudia Rabb wetu wenye kumsifu. Allaah ametimiza Ahadi Yake na kumsaidia mja Wake na akayashinda majeshi ya adui peke Yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Muslim: Alipokuwa anarudi kutoka katika vita au kikosi kidogo au Hijjah au 'Umrah.

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رجلاً قَالَ : يَا رسول الله ، إنّي أُريدُ أنْ أُسَافِرَ فَأوْصِني ، قَالَ : ((  عَلَيْكَ بِتَقْوَى اللهِ ، وَالتَّكْبِيرِ عَلَى كلِّ شَرَفٍ )) فَلَمَّا وَلَّى الرَّجُلُ ، قَالَ : (( اللَّهُمَّ اطْوِ لَهُ البُعْدَ ، وَهَوِّنْ عَلَيْهِ السَّفَرَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mtu mmoja alisema: 'Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi ninataka kusafiri, nakuomba uniusiye." Akasema: "Jilazimishe kumcha Allaah na kutoa Takbira juu ya kila mahali penye mwinuko." Yule mtu alipoanza safari, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuombea: "Ee Rabb! Mfupishie umbali (wa safari yake) na mfanyie sahali safari yake." [At-Tirmidhiy, na akasrema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي موسى الأشعريِّ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كنّا مَعَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم في سَفَرٍ ، فَكُنَّا إِذَا أشْرَفْنَا عَلَى وَادٍ هَلَّلْنَا وَكَبَّرْنَا وَارتَفَعَتْ أصْوَاتُنَا ، فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : ((  يَا أيُّهَا النَّاسُ ، ارْبَعُوا عَلَى أنْفُسِكُمْ ، فَإنَّكُمْ لاَ تَدْعُونَ أصَمَّ وَلاَ غَائِباً ، إنَّهُ مَعَكُمْ ، إنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu Muwsaa Al-Ash'ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Tulikuwa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika safari, tukawa kila tunapopanda mlima tukitoa Tahlil (Laa ILLaaha Illa Allaah) na Takbir kwa sauti kubwa. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Enyi watu! Musizikalifishe nafsi zenu kwani nyinyi hamumuombi aliye kiziwi wala asiyekuwepo. Hakika Yeye yu pamoja nanyi, hakika Yeye Anasikia na yu karibu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share