08-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Duaa Atakayoomba Mtu Pindi Akiwaogopa Watu au Wengineo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يدعو بِهِ إِذَا خاف ناساً أَوْ غيرهم
08-Mlango Wa Duaa Atakayoomba Mtu Pindi Akiwaogopa Watu au Wengineo
عن أَبي موسى الأشعريِّ رضي اللهُ عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا خَافَ قَوْماً، قَالَ : (( اللَّهُمَّ إنَّا نَجْعَلُكَ في نُحُورِهِمْ ، وَنَعُوذُ بِكَ مِنْ شُرُورِهِمْ )) رواه أَبُو داود والنسائي بإسنادٍ صحيحٍ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwaogopa watu anasema: "Ee Rabb wangu wa haki hakika sisi tunakuweka shingoni mwao na tunataka hifadhi Kwako na shari zao." [Abu Daawuwd na An-Nasaaiy kwa Isnaad iliyo Swahiyh]