09-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Anachosema Anayeshukia Mahali

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب مَا يقول إِذَا نزل منْزلاً

09-Mlango Wa Anachosema Anayeshukia Mahali

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن خولة بنتِ حَكِيمٍ رضي الله عنها، قالت: سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يَقُولُ : ((  مَنْ نَزَلَ مَنْزِلاً ثُمَّ قَالَ : أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ ، لَمْ يَضُرَّهُ شَيْءٌ حَتَّى يَرْتَحِلَ مِنْ مَنْزِلِهِ ذَلِكَ )) رواه مسلم .

Amesema Khawlah bint Haakim (Radhwiya Allaahu 'anha) kuwa: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Yeyote anayeshuka mashukio yoyote kisha akasema: 'A'udhu Bikalimati Llaahit Taammaati min sharri maa Khalaq - Ninajikinga kwa maneno ya Allaah yaliyokamilika kutokana na shari ya kila alichokiumba', hatodhuriwa na kitu chochote mpaka aondoke sehemu hiyo." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا سَافَرَ فَأقْبَلَ اللَّيْلُ، قَالَ: ((  يَا أرْضُ، رَبِّي وَرَبُّكِ اللهُ ، أعُوذُ بِاللهِ مِنْ شَرِّكِ وَشَرِّ مَا فِيكِ ، وَشَرِّ مَا خُلِقَ فِيكِ ، وَشَرِّ مَا يَدِبُّ عَلَيْكِ ، وَأعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ أسَدٍ وَأسْوَدٍ ، وَمِنَ الحَيَّةِ وَالعَقْرَبِ ، وَمِنْ سَاكِنِ البَلَدِ ، وَمِنْ وَالِدٍ وَمَا وَلَدَ )) رواه أَبُو داود .

Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposafiri utakapoingia usiku anasema: "Ee ardhi, Rabb wangu na Rabb wako ni Allaah najilinda kwa Allaah dhidi ya shari yako, na shari iliyo ndani yako, na shari ya vilivyoumbwa ndani yako, na dhidi ya shari vinavyotambaa juu yako, na ninajilinda kwa Allaah dhidi ya shari ya simba, na weusi, (Al Aswad), na dhidi ya nyoka na nge, na dhidi ya wakazi wa mji, na dhidi ya mzazi na alichokizaa." [Abu Daawuwd]

 

 

 

Share