10-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendekezwa Kurudi Haraka Msafiri kwa Familia Yake Anapomaliza Haja Yake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب تعجيل المسافرالرجوع إِلَى أهله إِذَا قضى حاجته
10-Mlango Wa Kupendekezwa Kurudi Haraka Msafiri kwa Familia Yake Anapomaliza Haja Yake
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( السَّفَرُ قِطْعَةٌ مِنَ العَذَابِ، يَمْنَعُ أحَدَكُمْ طَعَامَهُ وَشَرابَهُ وَنَوْمَهُ، فَإذَا قَضَى أحَدُكُمْ نَهْمَتَهُ مِنْ سَفَرِهِ ، فَلْيُعَجِّلْ إِلَى أهْلِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Safari ni kipande cha adhabu, inamzuia mmoja wenu chakula chake, kinywaji chake na usingizi wake. Hivyo, mmoja wenu atakapomaliza haja yake katika safari yake, na arudi haraka kwa watu wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]