03-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendekezwa Kusoma Qur-aan kwa Sauti Nzuri na Kutaka Isomwe na Mtu Mwenye Sauti Nzuri na Kumsikiliza

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب استحباب تحسين الصوت بالقرآن

وطلب القراءة من حسن الصوت والاستماع لها

03-Mlango Wa Kupendekezwa Kusoma Qur-aan kwa Sauti Nzuri na Kutaka Isomwe na Mtu Mwenye Sauti Nzuri na Kumsikiliza

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  مَا أَذِنَ اللهُ لِشَيءٍ مَا أَذِنَ لِنَبِيٍّ حَسَنِ الصَّوْتِ يَتَغَنَّى بِالقُرْآنِ يَجْهَرُ بِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Allaah hakuruhusu kitu kizuri zaidi kama alivyomruhusu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuitumia sauti nzuri kughania Qur-aan na kuisoma kwa sauti." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nasaai]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي موسى الأَشعري رضي اللهُ عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ لَهُ :((  لَقدْ أُوتِيتَ مِزْمَاراً مِنْ مَزَامِيرِ  آلِ دَاوُدَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية لمسلمٍ : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ لَهُ : ((  لَوْ رَأيْتَنِي وَأنَا أسْتَمِعُ لِقِراءتِكَ الْبَارِحَةَ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Kwa hakika umepewa kinanda miongoni mwa vinanda vya watu wa Daawuwd mwenyewe." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Muslim: Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia yeye: "Lau kama ungeniona mimi jana nikisikiliza kisomo chako kizuri cha Qur-aan."

 

Hadiyth – 3

وعن البَراءِ بنِ عازِبٍ رضي اللهُ عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم قَرَأَ فِي الْعِشَاءِ بالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ، فَمَا سَمِعْتُ أحَداً أحْسَنَ صَوْتاً مِنْهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa alimsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisoma katika Swalaah ya 'Ishaa Suwrah At-Tiyn. Hakika ni kuwa sijawahi kumsikia yeyote mwenye sauti nzuri kuliko yeye." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي لُبَابَةَ بشير بن عبد المنذر رضي اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَنْ لَمْ يَتَغَنَّ بِالقُرْآنِ فَلَيْسَ مِنَّا )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيدٍ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Lubaabah Bashiyr bin 'Abdil Mundhir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote asiyeghani (yaani kusoma Qur-aan kwa sauti nzuri) katika kuisoma Qur-aan si katika sisi." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Jayd]

 

Hadiyth – 5

وعن ابن مسعودٍ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ لِي النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : ((  اقْرَأْ عَلَيَّ القُرْآنَ )) ، فقلتُ : يَا رسولَ الله ، أَقْرَأُ عَلَيْكَ ، وَعَلَيْكَ أُنْزِلَ ؟! قَالَ : ((  إنِّي أُحِبُّ أنْ أسْمَعَهُ مِنْ غَيْرِي )) فَقَرَأْتُ عَلَيْهِ سُورَةَ النِّسَاءِ ، حَتَّى جِئْتُ إِلَى هذِهِ الآية: [ فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَؤُلاَءِ شَهِيداً ] [النِّسَاءِ: ٤١] قَالَ :((  حَسْبُكَ الآنَ )) فَالْتَفَتُّ إِلَيْهِ ، فَإذَا عَيْنَاهُ تَذْرِفَانِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Na Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Aliniambia: "Nisome Qur-aan." Nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Nikusomee wewe na imeteremshwa kwako?", Akasema: "Mimi napenda kuisika kwa mwengine." Ibn Mas'uwd akasema: "Nikamsomea Suwrah An-Nisaa' hadi nikafika ayah hii, "Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila Ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?" [An-Nisaa: 41]. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Inatosha sasa." Nikamgeukia nikaona macho yake yanabubujika machozi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

 

 

Share