04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhimiza Kusoma Suwrah na Ayah Maalumu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الحث عَلَى سور وآيات مخصوصة

04-Mlango Wa Kuhimiza Kusoma Suwrah na Ayah Maalumu

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أَبي سَعِيدٍ رَافِعِ بن الْمُعَلَّى رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : ((  أَلاَ أُعَلِّمُكَ أَعْظَمَ سُورَةٍ في القُرْآن قَبْلَ أنْ تَخْرُجَ مِنَ الْمَسْجِدِ ؟ )) فَأخَذَ بِيَدِي ، فَلَمَّا أرَدْنَا أنْ نَخْرُجَ ، قُلْتُ : يَا رَسُولَ اللهِ ، إنَّكَ قُلْتَ : لأُعَلِّمَنَّكَ أعْظَمَ سُورَةٍ في القُرْآنِ ؟ قَالَ : ((  الحَمْدُ للهِ رَبِّ العَالَمِينَ ، هِيَ السَّبْعُ المَثَانِي وَالقُرْآنُ العَظِيمُ الَّذِي أُوتِيتُهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Raafi' bin Al-Mu'allaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Je, nisikufundishe Suwrah tukufu katika Qur-aan kabla hujatoka Msikitini?" Akashika mkono wangu, tulipotaka kutoka nilimwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Uliniambia utanifundisha Suwrah tukufu katika Qur-aan." Akasema: "الحَمْدُ للهِ رَبِّ العَالَمِينَ", hiyo ni Suwrah yenye Ayah saba zinazokaririwa, na Qur-aan Tukufu ambayo nimepewa." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخدري رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ في : ( قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ ) : ((  وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ القُرْآنِ )) .

وفي روايةٍ : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ لأَصْحَابِهِ : ((  أَيَعْجِزُ أحَدُكُمْ أنْ يَقْرَأَ بِثُلُثِ القُرْآنِ فِي لَيْلَةٍ )) فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَيْهِمْ ، وَقَالُوا : أيُّنَا يُطِيقُ ذَلِكَ يَا رسولَ الله ؟ فَقَالَ : ((  ( قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ اللهُ الصَّمَدُ ) : ثُلُثُ الْقُرْآنِ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusu ( قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ ) : "Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, hakika hiyo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan." 

Na katika riwaayah nyingine: "Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Swahaaba wake: 'Je, anashindwa mmoja wenu kusoma thuluthi ya Qur-aan kwa usiku mmoja?" Jambo hilo likawa gumu kwao, na wakasema: "Nani anayeweza kufanya hivyo, Ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "( قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ اللهُ الصَّمَدُ ) , ni thuluthi ya Qur-aan." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد الخدري رضي اللهُ عنه : أنَّ رَجُلاً سَمِعَ رَجُلاً يَقْرَأُ : ((  قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ )) يُرَدِّدُهَا فَلَمَّا أصْبَحَ جَاءَ إِلَى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ وَكَانَ الرَّجُلُ يَتَقَالُّهَا ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، إنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ القُرْآنِ )) رواه البخاري .

Na kutoka kwake Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu); "Mtu alimsikia mtu mwingine anasoma: ( قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ ) , anairudiarudia, kulipopambazuka akaja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamueleza hilo, na huyu mtu alikuwa analiona dogo sana. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, hakika Suwrah hiyo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هُرَيْرَةَ رضي اللهُ عنه : أَنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ في :  (قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ ) ((  إنَّهَا تَعْدِلُ ثُلُثَ الْقُرْآنِ )) رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kuhusu ( قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ ) : Hakika hiyo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan." [Muslim] 

 

Hadiyth – 5

وعن أنس رضي اللهُ عنه : أنَّ رَجُلاً قَالَ : يَا رَسُولَ اللهِ ، إني أُحِبُّ هذِهِ السُّورَةَ : ( قُلْ هُوَ اللهُ أحَدٌ ) قَالَ : ((  إنَّ حُبَّهَا أدْخَلَكَ الجَنَّةَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) . ورواه البخاري في صَحِيحِهِ تعليقاً .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): kuwa Mtu mmoja aliuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi naipenda Suwrah hii: ( قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ ) . Akasema: "Hakika kuipenda hiyo (Suwrah) kutakuingiza Peponi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan na ameipokea Al-Bukhaariy katika Swahiyh yake]

 

Hadiyth – 6

وعن عقبة بن عامِر رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  ألَمْ تَرَ آيَاتٍ أُنْزِلَتْ هذِهِ اللَّيْلَةَ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ ؟ ( قُلْ أَعْوذُ بِرَبِّ الفَلَقِ ) وَ( قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ) )) رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kwani hukuona aya zilizoteremshwa usiku huu ambazo hazijaonekana mfano wake kabisa? ( قُلْ أَعْوذُ بِرَبِّ الفَلَقِ ) na ( قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ) ." [Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي سَعِيدٍ الخُدريِّ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يَتَعَوَّذُ مِنَ الجَانِّ ، وَعَيْنِ الإنْسَانِ ، حَتَّى نَزَلَتْ المُعَوِّذَتَانِ ، فَلَمَّا نَزَلَتَا ، أخَذَ بِهِمَا وَتَرَكَ مَا سِوَاهُمَا . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Na Abu Sa'iyd al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitaka hifadhi kwa Allaah kutokana na majini na macho mabaya ya wanadamu mpaka alipoteremka al-Mu'wwidhatayn (Suwrah mbili za kujikinga kwa Allaah yaani suwratul Falaq na An-Naas). Zilipoteremka alizichukua na akawa anazisoma na kuacha vyengine vyote." [At-Trmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan].

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مِنَ القُرْآنِ سُورَةٌ ثَلاثُونَ آيَةً شَفَعَتْ لِرَجُلٍ حَتَّى غُفِرَ لَهُ ، وَهِيَ : ( تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ المُلْكُ ) )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

وفي رواية أَبي داود : ((  تَشْفَعُ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ndani ya Qur-aan ipo Suwrah yenye ayah thelethini ambayo itamuombea mtu mpaka asamehewe na Allaah; nayo ni ( تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ المُلْكُ ) (Suwratul Mulk-Suwrah ya:67) [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي مسعودٍ البَدْرِيِّ رضي اللهُ عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَنْ قَرَأَ بِالآيَتَيْنِ مِنْ آخر سُورَةِ البَقَرَةِ في لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Mas'uud Al-Badriy (Radhwiya Allaahu 'anhu): kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusoma ayah mbili za mwisho wa Suwratul Baqarah usiku zitamtosha." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 10

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  لاَ تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ ، إنَّ الشَّيْطَانَ يَنْفِرُ مِنَ البَيْتِ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ سُورَةُ البَقرَةِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msifanye nyumba zenu kuwa makaburi, kwa hakika shetani anakimbia kutoka kwa nyumba ambayo husomwa ndani yake Suwratul Baqarah." [Muslim]

 

Hadiyth – 11

وعن أُبَيِّ بنِ كَعبٍ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  يَا أَبَا الْمُنْذِرِ ، أَتَدْري أيُّ آيَةٍ مِنْ كِتَابِ الله مَعَكَ أعْظَمُ ؟ )) قُلْتُ : ( اللهُ لاَ إلَهَ إِلاَّ هُوَ الحَيُّ القَيُّومُ ) فَضَرَبَ فِي صَدْرِي ، وقال : ((  لِيَهْنِكَ العِلْمُ أَبَا الْمُنْذِرِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ubayy bin Ka'ab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniuliza: "Ee Abul Mundhir! je, unajua ni ayah gani kwako ndio tukufu kabisa katika Kitabu cha Allaah?" Nikasema: "( اللهُ لاَ إلَهَ إِلاَّ هُوَ الحَيُّ القَيُّومُ ) Al-Baqarah: 255). Alinishika kifua changu, akasema: "Hongera kwa ilimu yako (ya Qur-aan), ee Abul Mundhir." [Muslim]

 

Hadiyth – 12

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : وَكَّلَنِي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بِحِفْظِ زَكَاةِ رَمَضَانَ، فَأتَانِي آتٍ فَجَعَلَ يَحْثُو مِنَ الطَّعَام، فَأخَذْتُهُ فقُلتُ: لأَرْفَعَنَّكَ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : إنِّي مُحْتَاجٌ ، وَعَليَّ عِيَالٌ ، وَبِي حَاجَةٌ شَدِيدَةٌ ، فَخَلَّيْتُ عَنْهُ ، فَأصْبَحْتُ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  يَا أَبَا هُريرة ، مَا فَعَلَ أَسِيرُكَ البَارِحَةَ ؟ )) قُلْتُ : يَا رسول الله ، شَكَا حَاجَةً وَعِيَالاً ، فَرحِمْتُهُ فَخَلَّيْتُ سَبيلَهُ . فَقَالَ : ((  أمَا إنَّهُ قَدْ كَذَبَكَ وَسَيَعُودُ )) فَعَرَفْتُ أنَّهُ سَيَعُودُ ، لقولِ رسول الله صلى الله عليه وسلم فَرَصَدْتُهُ ، فَجاء يَحْثُو مِنَ الطَّعَامِ ، فَقُلتُ : لأَرْفَعَنَّكَ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : دَعْنِي فَإنِّي مُحْتَاجٌ ، وَعَلَيَّ عِيَالٌ لاَ أعُودُ ، فَرحِمْتُهُ فَخَلَّيْتُ سَبيلَهُ ، فَأصْبَحْتُ فَقَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  يَا أَبَا هُريرة ، مَا فَعَلَ أَسِيرُكَ البَارِحَةَ ؟ )) قُلْتُ : يَا رسول الله ، شَكَا حَاجَةً وَعِيَالاً ، فَرحِمْتُهُ فَخَلَّيْتُ سَبيلَهُ . فَقَالَ : ((  إنَّهُ قَدْ كَذَبَكَ وَسَيَعُودُ )) فَرَصَدْتُهُ   الثَّالثَة ، فَجاء يَحْثُو مِنَ الطَّعَامِ فَأخَذْتُهُ ، فَقُلتُ : لأَرْفَعَنَّكَ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، وهذا آخِرُ ثلاثِ مَرَّاتٍ أنَّكَ تَزْعُمُ أنَّكَ لاَ تَعُودُ ! فَقَالَ : دَعْنِي فَإنِّي أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ يَنْفَعُكَ اللهُ بِهَا ، قُلْتُ : مَا هُنَّ ؟ قَالَ : إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَاقْرَأْ آيَةَ الكُرْسِيِّ ، فَإنَّهُ لَنْ يَزَالَ عَلَيْكَ مِنَ الله حَافِظٌ ، وَلاَ يَقْرَبُكَ شَيْطَانٌ حَتَّى تُصْبِحَ ، فَخَلَّيْتُ    سَبِيلَهُ ، فَأصْبَحْتُ ، فَقَالَ لي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَا فَعَلَ أسِيرُكَ البَارِحَةَ ؟ )) قُلْتُ : يَا رسول الله ، زَعَمَ أنَّهُ يُعَلِّمُنِي كَلِمَاتٍ يَنْفَعُنِي اللهُ بِهَا ، فَخَلَّيْتُ سَبيلَهُ ، قَالَ :     (( مَا هِيَ ؟ )) قُلْتُ : قَالَ لي : إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَاقْرَأْ آيَة الكُرْسِيِّ مِنْ أوَّلِهَا حَتَّى تَخْتِمَ الآية : ( اللهُ لاَ إلَهَ إِلاَّ هُوَ الحَيُّ القَيُّومُ ) وقال لِي : لاَ يَزَالُ عَلَيْكَ مِنَ اللهِ حَافِظٌ ، وَلَنْ يَقْرَبَكَ شَيْطَانٌ حَتَّى تُصْبِحَ . فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : ((  أمَا إنَّهُ قَدْ صَدَقَكَ وَهُوَ كَذُوبٌ ، تَعْلَمُ مَنْ تُخَاطِبُ مُنْذُ ثَلاَثٍ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ ؟ )) قُلْتُ : لاَ . قَالَ : ((  ذَاكَ شَيْطَانٌ )) رواه البخاري .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alinichagua kuhifadhi Zakaah ya Ramadhwaan, - Zakatul Fitr - Akaja mwenye kuja, akawa anachukua chakula, Nikamshika nikamwambia: "Nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam)." Akasema: "Mimi ni muhitaji, nina familia, nina haja nyingi." Nikamuachia. Nilipoamka; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Ee Abu Huraiyrah! Alifanya nini mateka wako jana?" Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Alinilalamikia haja na familia, Nilimhurumia nikamuacha." Akasema: "Ama hakika, amekudanganya na atarudi tena." Nilijua kwa hakika atarudi kwa kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo nilimvizia. Alikuja na kuchukua chakula. Nilimkamata nikamwambia: "Nitampeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Akasema: "Niache kwani mimi ni mhitaji na nina familia wala sitarudi." Nilimhurumia na kumuacha njia yake. Nikaamka, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Ee Abu Huraiyrah! mateka wako jana?" Nilimwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Alinilalamikia kuwa ana haja kubwa na familia, hivyo nilimhurumia na kumuachia aende." Akasema: "Hakika amekudanganya na atarudi." Nilimvizia mara ya tatu, Alikuja na kuchukua chakula, nikamshika. Nikamwambia: "Nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na hii ni mara ya tatu ya mwisho ambayo unadai hutarudi, kisha unarudi." Akasema: "Niachie, hakika mimi nitakufundisha maneno Allaah atakunufaisha nayo." Nikasema: "Ni yapi hayo?" Akasema: "Unapokwenda kitandani kwako soma Ayatul Kursiy (2:255) hadi umalizie ayah, kwani mlinzi wa Allaah hataacha kuwa juu yako, (akuhifadhi) wala hatakukaribia shetani mpaka unapambazuka, Nilimuachia njia yake." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Ee Abu Huraiyrah! Alifanya nini mateka wako jana?" Nilimwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Alidai kuwa atanifundisha maneno ambayo Allaah ataninufaisha nayo, hivyo nikamwachia." Akasema: "Ni yapi hayo?" Nikasema: "Aliniambia: Unapokwenda kitandani kwako soma Ayatul Kursiy, kuanzia mwanzo mpaka umalize ayah ( اللهُ لاَ إلَهَ إِلاَّ هُوَ الحَيُّ القَيُّومُ ) (Al-Baqarah: 255). Na akaniambia: "Mlinzi wa Allaah hataacha kuwa juu yako, wala hatakukaribia shetani mpaka asubuhi." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)akasema: "Kwa hakika yeye amekuambia kweli na yeye ni muongo. Unajua unazungumza na nani muda wa siku tatu, ee Abu Huraiyrah?" Nikasema: "La." Akasema: "Huyo alikuwa ni shetani." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 13

وعن أَبي الدرداءِ رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَنْ حَفِظَ عَشْرَ آيَاتٍ مِنْ أَوَّلِ سُورَةِ الكَهْفِ ، عُصِمَ مِنَ الدَّجَّالِ )) .

وفي رواية : ((  مِنْ آخِرِ سُورَةِ الكَهْفِ )) رواهما مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuhifadhi ayah kumi mwanzo wa Suwrah Al-Kahf (Suwrah: 18) ataepushwa na Dajjal.

Na katika riwaayah nyengine: "Mwisho wa Suwrah Al-Kahf. [Muslim]. Riwaayah ya kwanza ndiyo iliyohifadhiwa.

 

Hadiyth – 14

وعن ابنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما : بَيْنَمَا جِبْريلُ (عَلَيْهِ السَّلام) قَاعِدٌ عِنْدَ النبي صلى الله عليه وسلم سَمِعَ نَقيضاً مِنْ فَوقِهِ ، فَرَفَعَ رَأسَهُ ، فَقَالَ : هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ اليَوْمَ وَلَمْ يُفْتَحْ قَطٌّ إِلاَّ اليَوْمَ ، فنَزلَ منهُ مَلكٌ ، فقالَ : هذا مَلكٌ نَزلَ إلى الأرضِ لم ينْزلْ قطّ إلاّ اليومَ فَسَلَّمَ وقال : أبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤتَهُمَا نَبيٌّ قَبْلَكَ : فَاتِحَةُ الكِتَابِ ، وَخَواتِيمُ سُورَةِ البَقَرَةِ ، لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهَا إِلاَّ أُعْطِيتَه . رواه مسلم .

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Jibriyl ('Alayhis Salaam) akiwa amekaa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), alisikia sauti kutoka juu, akainua kichwa chake, akasema: "Huu ni mlango mbinguni umefunguliwa leo haujafunguliwa kabisa ila leo." Humo akateremka Malaaikah, Jibriyl akasema: "Huyu ni Malaaikah ameteremka ardhini, hajateremka kabisa ila leo." Akamsalimia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)na akasema: "Pata bishara ya nuru mbili ulizopewa, hajapewa Nabiy yoyote kabla yako. Ufunguzi wa Kitabu (Suwrah Al-Faatihah), na mwisho wa Suwrah Al-Baqarah. Hatasoma yoyote herufi moja miongoni mwa hizo ila utapewa ujira." [Muslim]

 

 

Share