06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora wa Wudhuu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل الوضوء

06-Mlango Wa Ubora wa Wudhuu

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى :

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٦﴾

Enyi walioamini!  Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah; osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi, na panguseni (kwa kupaka maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu hadi vifundoni. Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni. Na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akitoka msalani, au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji; basi tayammamuni (ikusudieni) ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. Allaah Hataki kukufanyieni magumu, lakini Anataka kukutwaharisheni na Akutimizieni neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru. [Al-Maaidah: 6]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  إنَّ أُمَّتِي يُدْعَوْنَ يَوْمَ القِيَامَةِ غُرَّاً مُحَجَّلينَ مِنْ آثَارِ الوُضُوءِ ، فَمَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمْ أنْ يُطِيلَ غُرَّتَهُ فَلْيَفْعَلْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika Ummah wangu utaitwa Siku ya Qiyaamah Ghurran Muhajjaliyn (Ghurrah ni kuosha kwa kuzidisha ile sehemu ya faradhi katika pambizoni mwa paji la uso, masikio na baadhi ya shingo na hivyo kulifanya paji la uso na sehemu hizo kuwa na weupe Siku ya Qiyaamah. Muhajjaliyn ni kurefusha kuosha miguu na mikono katika zile sehemu za faradhi, hivyo kuzifanya ziwe nyeupe Siku ya Qiyaamah). Kutokana na athari ya wudhuu; kwa atakayeweza miongoni mwenu kurefusha Ghurra yake na afanye." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ خليلي صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  تَبْلُغُ الحِلْيَةُ مِنَ المُؤمِنِ حَيْثُ يَبْلُغُ الوُضُوءُ )) رواه مسلم .

Na Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimsikia kipenzi changu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Uzuri wa Muumini Peponi utafika umbali wa maji aliyotumia kuchukua nayo wudhuu. [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن عثمان بن عفان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  من تَوَضَّأ فَأَحْسَنَ الوُضُوءَ ، خَرَجَتْ خَطَايَاهُ مِنْ جَسَدِهِ حَتَّى تَخْرُج مِنْ تَحْتِ  أَظْفَارِهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutawadha vizuri, madhambi yake hutoka katika mwili wake mpaka yatatoka kutoka chini ya kucha zake." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن عثمان بن عفان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : رَأيتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم تَوَضَّأَ مِثْلَ وُضُوئِي هَذَا ، ثُمَّ قَالَ : ((  مَنْ تَوَضَّأ هكَذَا ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ ، وَكَانَتْ صَلاَتُهُ وَمَشْيُهُ إِلَى المَسْجدِ نَافِلَةً )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitawadha mfano wa Wudhuu wangu huu, kisha akasema: "Yeyote atakaye tawadha hivi, anasamehewa madhambi yake yaliyotangulia na Swalaah yake inakuwa na kutembea kwake Msikitini ni nyongeza (ya mizani yake ya mambo mema). [Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  إِذَا تَوَضَّأ العَبْدُ المُسْلِمُ - أَو المُؤْمِنُ - فَغَسَلَ وَجْهَهُ ، خَرَجَ مِنْ وَجْهِهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ نَظَرَ إِلَيْهَا بِعَيْنَيْهِ مَعَ المَاءِ ، أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ ، فَإذَا غَسَلَ يَدَيْهِ ، خَرَجَ مِنْ يَدَيْهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ كَانَ بَطَشَتْهَا يَدَاهُ مَعَ المَاءِ ، أَو مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ ، فَإذَا غَسَلَ رِجْلَيْهِ ، خَرَجَتْ كُلُّ خَطِيئَةٍ مَشَتْهَا رِجْلاَهُ مَعَ المَاءِ ، أَو مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ ، حَتَّى يَخْرُجَ نَقِيَّاً مِنَ الذُّنُوبِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mja , Muumini au Muislamu atakapotawadha kila kosa ambalo ameangalia kwa macho yako pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji, na akikosha mikono yake huondoka kila dhambi ambayo ameifanya kwa mikono yake pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji. Anapokosha miguu yake, huondoka kila dhambi ambayo ameifanya kwa miguu yake pamoja na maji au pamoja na tone la mwisho la maji, mpaka anatoka akiwa amesafika na dhambi." [Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أتى المقبرة ، فَقَالَ : ((  السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ دَارَ قَومٍ مُؤْمِنِينَ ، وَإنَّا إنْ شَاءَ اللهُ بِكُمْ لاَحِقُونَ ، وَدِدْتُ أنَّا قَدْ رَأَيْنَا إخْوانَنَا )) قالوا : أوَلَسْنَا إخْوَانَكَ يَا رسول الله ؟ قَالَ : ((  أنْتُمْ أصْحَابِي ، وَإخْوَانُنَا الَّذِينَ لَمْ يَأتُوا بَعْدُ )) قالوا : كَيْفَ تَعْرِفُ مَنْ لَمْ يَأتِ بَعْدُ مِنْ أُمَّتِكَ يَا رَسولَ الله ؟ فَقَالَ : ((  أرَأيْتَ لَوْ أنَّ رَجُلاً لَهُ خَيلٌ غُرٌّ مُحَجَّلَةٌ بَيْنَ ظَهْرَيْ خَيْلٍ دُهْمٍ  بُهْمٍ ، ألا يَعْرِفُ خَيْلَهُ ؟ )) قالوا : بَلَى يَا رسول الله ، قَالَ : ((  فإنَّهُمْ يَأتُونَ غُرّاً مُحَجَّلينَ مِنَ الوُضُوءِ ، وأنَا فَرَطُهُمْ عَلَى الحَوْضِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitembelea makaburi ya Baqii' akasema: As-Salaamu 'alaykum daara Qawmi Mu'miniyna wa Innaa In shaa Allaah bikum laahiquwn (Amani iwashukiewatu wa nyumba ya Waumini, na sisi akitaka Allaah tutakutana nanyi). Ilikuwa ni hamu yangu kubwa kukutana na ndugu zangu." Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Sisi si ndugu zako?" Akasema: "Nyinyi ni Swahaaba zangu, na ndugu zetu ni ambao hawajaja bado (Duniani)." Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Umejua vipi ambao hawajaja bado katika uma wako?" Akasema: "Mnaonaje lau mtu ana farasi weupe kwenye nyuso zao na weupe katika kwato zao na wakachanganyika na farasi weusi hatawatambua farasi wake?" Wakasema: "Atawatambua ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Hakika wao watakuja Ghurran Muhajjaaliin kwa sababu ya wudhuu, nami nitawatangulia kwenye Hawdh (birika)." [Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  ألاَ أَدُّلُكُمْ عَلَى مَا يَمْحُو اللهُ بِهِ الخَطَايَا ، وَيَرْفَعُ بِهِ الدَّرَجَاتِ ؟ )) قالوا : بَلَى يَا رسول الله ، قَالَ : ((  إسْبَاغُ الوُضُوءِ عَلَى المَكَارِهِ ، وَكَثْرَةُ الخُطَا إِلَى المَسَاجِدِ ، وَانْتِظَارُ الصَّلاَةِ بَعْدَ الصَّلاَةِ ؛ فَذلِكُمُ الرِّبَاطُ ؛ فَذَلِكُمُ الرِّبَاطُ )) رواه مسلم .

Kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Huvi niwafahamishe juu ya kile ambacho anafuta nacho Allaah makosa na ananyanyua nacho daraja?" Wakasema: "Kwa nini ee Rasuli wa Allaah, tufahamishe." Akasema: "Ni kujieneza wudhuu pamoja na machukivu (mfano baridi, hali ya hewa nzito, kuumwa) na uwingi wa nyayo kwenda Msikitini na kungojea Swalaah baada ya Swalaah, huo ndio ulingaji, huo ndio ulindaji." [Muslim]

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي مالك الأشعري رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  الطُّهُورُ شَطْرُ الإيمَانِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Maalik Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kujitwahirisha ni nusu ya Imani." [Muslim]

 

Hadiyth – 9

وعن عمر بن الخطاب رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَا مِنْكُمْ مِنْ أحَدٍ يَتَوَضَّأُ فَيُبْلغُ – أَوْ فَيُسْبِغُ – الوُضُوءَ ، ثُمَّ يقول : أشهَدُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، وَأشْهَدُ أنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ ؛ إِلاَّ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ )) رواه مسلم .

وزاد الترمذي : ((  اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنَ التَّوَّابِينَ ، وَاجْعَلْنِي مِنَ المُتَطَهِّرِينَ )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna yeyote mingoni mwenu anatawadha vizuri au akaeneza wudhuu, kisha akasema: "Nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Allaah, Peke Yake hana mshirika. Na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja na Rasuli Wake." Isipokuwa itafunguliwa milango minane ya Pepo ataingia katika mlango wowote autakao." [Muslim]

Akaongeza At-Tirmidhiy: "Ee Mola wa haki nifanye mimi ni katika miongoni mwa wenye kutubia na nifanye mimi ni katika wenye kujitakasa." 

 

 

Share