07-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora wa Adhaan
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الأذان
07-Mlango Wa Ubora wa Adhaan
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَوْ يَعْلَمُ النَّاسُ مَا في النِّدَاءِ والصَّفِ الأَوَّلِ ، ثُمَّ لَمْ يَجِدُوا إِلاَّ أنْ يَسْتَهِمُوا عَلَيْهِ لاسْتَهَمُوا عَلَيْهِ ، ولو يَعْلَمُونَ مَا فِي التَّهْجِيرِ لاسْتَبَقُوا إِلَيْهِ ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِي العَتَمَةِ وَالصُّبْحِ لأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْواً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau kama watu wangeelewa fadhila za adhana (kuitikia) na kusimama katika safu ya kwanza, kisha wakawa hawakupata njia ya kudiriki isipokuwa kwa kupiga kura basi wangalipiga kura; na kama wangelielewa (fadhila za) kuwahi Swalaah wangalihimiza na kushindana katika kuiendea mapema; na kama wangelielewa (fadhila za) kuswali Swalaah ya Isha na Asubuhi kwa jamaa, wangeziendea Swalaah hizo japokuwa kwa kutambaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن معاوية رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( المُؤَذِّنُونَ أطْوَلُ النَّاسِ أعْناقاً يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwake Mu'awiyah Amesema: 'Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Anasema': "Waadhini watakuwa na shingo ndefu Siku ya Qiyaamah." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن عبدِ الله بن عبدِ الرَّحْمانِ بن أَبي صَعصعة : أنَّ أَبَا سَعيد الخدريَّ رضي اللهُ عنه ، قَالَ لَهُ : (( إنِّي أرَاكَ تُحبُّ الغَنَمَ وَالبَادِيَةَ فَإذَا كُنْتَ في غَنَمِك - أَوْ بَادِيتِكَ - فَأذَّنْتَ للصَّلاَةِ ، فَارْفَعْ صَوْتَكَ بِالنِّدَاءِ ، فَإنَّهُ لا يَسْمَعُ مدى صَوْتِ المُؤذِّنِ جِنٌّ ، وَلاَ إنْسٌ ، وَلاَ شَيْءٌ ، إِلاَّ شَهِدَ لَهُ يَومَ القِيَامَةِ )) قَالَ أَبُو سَعيدٍ : سمعتُهُ مِنْ رَسولِ الله صلى الله عليه وسلم . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Abdir-Rahmaan bin Abu Swa'swa'ah; Abu Sa'iyd alimwambia: "Mimi nakuona wapenda sana kondoo na kuwa katika kijiji, hivyo ukiwa machungioni au katika kijiji chako na ukaadhini kwa ajili ya Swalaah basi nyanyua sauti yako kwa kuita watu katika Swalaah, kwani hatasikia upeo wa sauti ya muadhini huyo jini wala Bin Aadam wala kitu chochote ila atakuwa shahidi yake Siku ya Qiyaamah." Akasema Abu Sa'iyd: "Nimesikia hayo kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا نُودِيَ بالصَّلاَةِ ، أدْبَرَ الشَّيْطَانُ ، وَلَهُ ضُرَاطٌ حَتَّى لاَ يَسْمَعَ التَّأذِينَ ، فَإذَا قُضِيَ النِّدَاءُ أقْبَلَ ، حَتَّى إِذَا ثُوِّبَ للصَّلاةِ أدْبَرَ ، حَتَّى إِذَا قُضِيَ التَّثْوِيبُ أقْبَلَ ، حَتَّى يَخْطِرَ بَيْنَ المَرْءِ وَنَفْسِهِ ، يَقُولُ : اذْكُرْ كَذَا واذكر كَذَا – لِمَا لَمْ يَذْكُر مِنْ قَبْلُ – حَتَّى يَظَلَّ الرَّجُلُ مَا يَدْرِي كَمْ صَلَّى )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Inaponadiwa Swalaah, shetani hukimbia na kutoa mashuzi ili asisikie adhana. Ikisha adhana hurudi; na tena anageuza mgongo na kukimbia pale Swalaah inapokimiwa; ikisha kimiwa hurudi tena, mpaka aingize wasi wasi kati ya mtu na nafsi yake (kwa lengo la kumtoa katika Swalaah), anamwambia: 'Kumbuka kadha, kumbuka kadha kwa yale ambayo kabla alikuwa hakumbuki', mpaka anamfanya hajui ameswali ngapi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن عبدِ الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنّه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول: (( إِذَا سَمِعْتُمُ النداء فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ ؛ فَإنَّه مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْراً ، ثُمَّ سَلُوا اللهَ لِيَ الوَسِيلَةَ ؛ فَإنَّهَا مَنْزِلَةٌ في الجَنَّةِ لاَ تَنْبَغِي إِلاَّ لِعَبْدٍ مِنْ عِبَادِ اللهِ وَأرْجُو أنْ أكونَ أنَا هُوَ ، فَمَنْ سَألَ لِيَ الوَسِيلَةَ حَلَّتْ لَهُ الشَّفَاعَةُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amri bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mtakapomsikia muadhini basi semeni kama anvyosema muadhini kisha nitakieni rehema, kwani anayenitakia rehema mara moja Allaah atamrehemu mara kumi, kisha nitakeni kwa Allaah wasila kwani hiyo ni daraja katika Pepo haipati isipokuwa mja mwema, na ninataraji niwe mimi, yule atakayeniombea wasila atafikiwa na shufaa yangu." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن أَبي سعيد الخدري رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا سَمِعْتُمُ النِّدَاءَ ، فَقُولُوا كَمَا يَقُولُ المُؤذِّنُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mkisikia adhana basi semeni kama anavyosema muadhini." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 7
وعن جابر رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ قَالَ حِيْنَ يَسْمَعُ النِّدَاءَ : اللَّهُمَّ رَبَّ هذِهِ الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ ، وَالصَّلاَةِ القَائِمَةِ ، آتِ مُحَمَّداً الوَسِيلَةَ ، وَالفَضِيلَةَ ، وَابْعَثْهُ مَقَامَاً مَحْمُوداً الَّذِي وَعَدْتَهُ ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتي يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusema pindi anaposikia mwito (adhaan): "Allaahumma Rabba Hadhihid Da'watit Taammati was-Swalaatil Qaa'imati Aaati Muhammadanil Wasiilah wal Fadhiilah wab'athhu maqaaman mahmuudani Ladhii wa'adtah" "Ee Rabb Mola wa ulingano huu mkamilifu. Na Mola wa Swalaah hii yenye kusimama, mpe Muhammad cheo (Wasila) na Fadhila. Na umfufue katika cheo chenye kuhimidiwa" Basi shufaa yangu itakuwa halali kwake Siku ya Qiyaamah." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 8
وعن سعدِ بن أَبي وقَّاصٍ رضي اللهُ عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنَّه قَالَ : (( مَنْ قَالَ حِيْنَ يَسْمَعُ المُؤَذِّنَ : أشْهَدُ أنْ لاَ إلَه إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، وَأنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ ، رَضِيتُ بِاللهِ رَبّاً ، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولاً ، وَبِالإسْلامِ دِيناً ، غُفِرَ لَهُ ذَنْبُهُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwake Sa'd bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusema pindi anapomsikia muadhini: "Nashuhudia kwamba hapana Mola ila Allaah, hana mshirika. Na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja na Rasuli Wake. Nimeridhia Allaah kuwa Rabb wangu, na Muhammad kuwa Rasuli, na Uislamu kuwa Dini", Anasamehemewa dhambi yake." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن أنس رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( الدُّعَاءُ لاَ يُرَدُّ بَيْنَ الأَذَانِ وَالإقَامَةِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Dua baina ya adhana na iqamah hairudishwi (yaani hukubaliwa na Allaah)." [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]