08-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila Za Swalaah
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الصلوات
08-Mlango Wa Fadhila Za Swalaah
قَالَ الله تَعَالَى :
إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ ﴿٤٥﴾
Hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. Na bila shaka kumdhukuru Allaah ni kubwa zaidi. Na Allaah Anajua yale mnayoyatenda. [Al-'Ankabuwt: 45]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول :
(( أرَأيْتُمْ لَوْ أنَّ نَهْرَاً بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ ، هَلْ يَبْقَى مِنْ دَرنهِ شَيْءٌ ؟ )) قالوا : لا يَبْقَى مِنْ دَرنهِ شَيْءٌ ، قَالَ : (( فَذلِكَ مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الخَمْسِ يَمْحُو اللهُ بِهِنَّ الخَطَايَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mnaonaje kama kutakuwa na mto mlangoni kwa mmoja wenu, kila siku anaoga humo mara tano. Je, atabakia na uchafu wowote?" Wakasema: "Hatabakia na uchafu." Akasema: "Basi huo ndio mfano wa Swalaah tano, Allaah anfuta makosa." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hadiyth – 2
وعن جابرٍ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَثَلُ الصَّلَواتِ الخَمْسِ كَمَثَلِ نَهْرٍ جَارٍ غَمْرٍ عَلَى بَابِ أحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَومٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mfano wa Swalaah tano ni kama mfano wa mto ulio jirani wenye maji matamu na mengi ulio katika mlango wa mmoja wenu, anaoga humo kila siku mara tano." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن ابن مسعود رضي اللهُ عنه : أنَّ رَجُلاً أصَابَ مِن امْرَأَةٍ قُبْلَةً ، فَأتَى النبيَّ صلى الله عليه وسلم فَأخْبَرَهُ فَأنْزَلَ اللهُ تَعَالَى : ( أَقِمِ الصَّلاَةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفاً مِنَ اللَّيْلِ ، إنَّ الحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ) [ هود : 114 ] فَقَالَ الرَّجُلُ أَلِيَ هَذَا ؟ قَالَ : (( لِجَمِيعِ أُمَّتِي كُلِّهِمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Mtu mmoja alimbusu mwanamke ajnabi (anayeweza kumuoa), akaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuelezea hilo. Allaah Ta'aalaa Akateremsha: "Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku, hakika mema yanaondosha maovu. Haya ni ukumbusho kwa wanaokumbuka." [Huwd: 114]. Akasema yule mtu: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, hili ni langu tu?" Akasema: "Hili ni kwa Ummah wangu wote." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الصَّلَوَاتُ الخَمْسُ ، وَالجُمُعَةُ إِلَى الجُمُعَةِ ، كَفَّارَةٌ لِمَا بَيْنَهُنَّ ، مَا لَمْ تُغشَ الكَبَائِرُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalaah tano, na Ijumaa hadi Ijumaa na Ramadhwaan hadi Ramadhwaan ni zenye kufuta madhambi yaliyo kati yake kama yakiepukwa madhambi makubwa." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن عثمان بن عفان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مِنْ امْرِئٍ مُسْلِمٍ تَحْضُرُهُ صَلاَةٌ مَكْتُوبَةٌ فَيُحْسِنُ وُضُوءها ؛ وَخُشُوعَهَا، وَرُكُوعَهَا ، إِلاَّ كَانَتْ كَفَّارَةً لِمَا قَبْلَهَا مِنَ الذُّنُوب مَا لَمْ تُؤتَ كَبِيرةٌ ، وَذلِكَ الدَّهْرَ كُلَّهُ )) رواه مسلم .
'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hapana mtu yeyote Muislamu ambaye inamuhudhurikia Swalaah iliyofaradhiwa akautengeneza vizuri wudhuu wake na unyenyekevu wake, na rukuu zake ila itakuwa ni kafara la yaliyo kabla yake miongoni mwa madhambi, muda wa kuwa halijatendwa kosa kubwa na utaratibu huo unaendelea maisha yote." [Muslim[.