13-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhimiza Kuhudhuria Jamaa Katika Swalah ya Asubuhi na Ishaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الحث عَلَى حضور الجماعة في الصبح والعشاء

13-Mlango Wa Kuhimiza Kuhudhuria Jamaa Katika Swalah ya Asubuhi na Ishaa

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن عثمان بن عفان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ صَلَّى العِشَاءَ فِي جَمَاعَةٍ ، فَكَأنَّمَا قَامَ نِصْفَ اللَّيْلِ ، وَمَنْ صَلَّى الصُّبْحَ في جَمَاعَةٍ ، فَكَأنَّمَا صَلَّى اللَّيْلَ كُلَّهُ )) رواه مُسلِم .

وفي رواية الترمذي عن عثمان بن عفان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ شَهِدَ العِشَاءَ فِي جَمَاعَةٍ كَانَ لَهُ قِيَامُ نِصْفَ لَيلَةٍ ، وَمَنْ صَلَّى العِشَاءَ وَالفَجْرَ فِي جَمَاعَةٍ ، كَانَ لَهُ كَقِيَامِ لَيْلَةٍ )) قَالَ الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .

'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) Amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kuswali Swalaah ya Ishaa kwa jamaa ni kama ameswali nusu ya usiku na mwenye kuswali Asubuhi kwa jamaa ni kama kwamba ameswali usiku kucha (usiku wote)." [Muslim]

Na katika riwaayah ya At-Tirmidhiy kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kushuhudia Swalaah ya Ishaa kwa jamaa ni kama aliyesimama kuswali nusu ya usiku. Na mwenye kuswali Ishaa na Alfajiri kwa jamaa ni kama kwamba ameswali usiku mzima." [Amesema At-Tirmidhiy kuwa hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 2

وعن أبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا في العَتَمَةِ وَالصُّبْحِ لأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوَاً )) متفقٌ عَلَيهِ . وقد سبق بِطولِهِ .

Imepokewa kutoka kwaAbuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Na lau kama wanafiki wangejua fadhila za Swalaah ya Ishaa na Asubuhi basi wangekuja hata kwa kutambaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لَيْسَ صَلاَةٌ أثْقَلَ عَلَى المُنَافِقِينَ مِنْ صَلاَةِ الفَجْرِ وَالعِشَاءِ ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِيهِمَا لأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْواً )) متفقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna Swalaah nzito kwa wanafiki kuliko Swalaah ya Alfajiri na Ishaa, na lau wangejua ubora wa Swalaah hizi mbili wangezijia hata kwa kutambaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share