14-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Amri ya Kuhifadhi Swalah za Faradhi na Onyo Kali kwa Kuziacha

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الأمر بالمحافظة عَلَى الصلوات المكتوبات

والنهي الأكيد والوعيد الشديد في تركهنّ

14-Mlango Wa Amri ya Kuhifadhi Swalah za Faradhi na Onyo Kali kwa Kuziacha

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾

Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu. [Al-Baqarah: 238]

 

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ ﴿٥﴾

Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi iacheni njia yao (huru). [At-Tawbah: 5]

 

Hadiyth – 1

وعن ابن مسعود رضي اللهُ عنه ، قال : سألت رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم أيُّ الأعْمَالِ أفْضَلُ ؟ قَالَ : (( الصَّلاَةُ عَلَى وَقْتِهَا )) قلتُ : ثُمَّ أيٌّ ؟ قَالَ : (( بِرُّ الوَالِدَيْنِ )) قلتُ : ثُمَّ أيٌّ ؟ قَالَ : (( الجِهَادُ في سَبِيلِ اللهِ )) متفقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni amali gani inampendeza Allaah zaidi ?" Akasema: "Ni Swalaah kwa wakati wake." Nikasema: "Kisha ni ipi?" Akasema: "Kuwatendea wema wazazi wawili." Nikasema: "Kisha ipi?" Akasema: "Jihadi katika Njia ya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( بُنِيَ الإسْلامُ عَلَى خَمْسٍ : شَهَادَةِ أنْ لاَ إلهَ إلاَّ اللهُ ، وَأنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللهِ ، وَإِقَامِ الصَّلاَةِ ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ ، وَحَجِّ البَيْتِ ، وَصَوْمِ رَمَضَانَ )) متفقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Uislamu Umejengwa juu ya nguzo tano: Kukiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kuhiji na kufunga mwezi wa Ramadhwaan." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai].

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( أُمِرْتُ أنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يَشْهَدُوا أنْ لاَ إلهَ إلاَّ اللهُ ، وأنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللهِ ، وَيُقِيمُوا الصَّلاَةَ ، وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ، فَإذَا فَعَلُوا ذَلِكَ ، عَصَمُوا مِنِّي دِمَاءهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ ، إلاَّ بِحَقِّ الإسْلاَمِ ، وَحِسَابُهُمْ عَلَى اللهِ )) متفقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka wakubali kuwa hakuna Mola wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah. Wakifanya hivyo zitahifadhika kwangu damu zao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislaamu, na hesabu yao iko kwa Allaah Ta'aalaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن معاذٍ رضي الله عنه ، قَالَ : بَعثنِي رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم إلى اليَمَنِ ، فَقَالَ : (( إنَّكَ تَأْتِي قَوْماً مِنْ أَهْل الكِتَابِ ، فَادْعُهُمْ إلى شَهَادَةِ أنْ لاَ إلهَ إلاَّ اللهُ ، وأنِّي رَسُولُ اللهِ ، فَإنْ هُمْ أطاعُوا لِذلِكَ ، فَأعْلِمْهُمْ أنَّ اللهَ تَعَالَى افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَومٍ وَلَيلَةٍ ، فَإنْ هُمْ أطَاعُوا لِذَلِكَ ، فَأعْلِمْهُمْ أنَّ اللهَ تَعَالَى افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤخَذُ مِنْ أغْنِيَائِهِمْ فَتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ ، فَإنْ هُمْ أطَاعُوا لِذلِكَ ، فَإيَّاكَ وَكَرَائِمَ أمْوَالهِمْ ، واتَّقِ دَعْوَةَ المَظْلُومِ ، فَإنَّهُ لَيْسَ بَينَهَا وبَيْنَ اللهِ حِجَابٌ )) متفقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinituma: "Hakika wewe unaenda kwa watu waliopewa Kitabu, hivyo waite katika Uislaamu na washuhudie ya kwamba hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba mimi ni Rasuli Wake. Wakikutii katika hilo, wafahamishe kuwa Allaah amewafaradhishia juu yao Swalaah tano kwa kila mchana na usiku. Wakikutii katika hilo, wafahamishe kuwa Allaah amewafaradhishia juu yao kutoa Swadaqah, inayochukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupatiwa mafakiri miongoni mwao. Ikiwa wao watakutii katika hilo, tahadhari sana na vilivyo bora ya mali zao. Naogopa sana dua ya mwenye kudhulumiwa kwa sababu hakuna kizuizi baina yake na Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن جابرٍ رضي الله عنه ، قال : سمعت رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ بَيْنَ الرَّجُلِ وَبَيْنَ الشِّرْكِ والكفر ، تَرْكَ الصَّلاَةِ )) رواه مُسلِم .

Na Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Kizuizi kilichoko baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha Swalaah." [Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن بُرَيْدَة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( العَهْدُ الَّذِي بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ الصَّلاَةُ ، فَمَنْ تَرَكَهَا فَقَدْ كَفَرَ )) رواه التِّرمِذِيُّ ، وَقَالَ : (( حَدِيثٌ حَسَنٌ صحيح )) 

Imepokewa kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Tofauti iliyopo baina yetu na wao (yaani wanafiki) ni Swalaah, mwenye kuiacha hakika amekufuru." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 7

وعن شقِيق بن عبدِ الله التَّابِعيِّ المتفق عَلَى جَلاَلَتِهِ رَحِمهُ اللهُ ، قَالَ : كَانَ أصْحَابُ محَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم لا يَرَوْنَ شَيْئاً مِنَ الأعْمَالِ تَرْكُهُ كُفْرٌ غَيْرَ الصَّلاَةِ . رَوَاهُ التِّرمِذِيُّ في كِتابِ الإيمان بإسنادٍ صحيحٍ .

Na kutoka kwa Shaqiyq bin 'Abdillaah, Tabi'iy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye utukufu kumeafikiwa na ubora wake amesema kwamba: Swahaaba wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Walikuwa hawaoni ni chochote katika amali ambazo kuziacha ni ukafiri isipokuwa Swalaah." [At-Tirmidhiy katika Kitabu cha Iymaan kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

Hadiyth – 8

وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ أوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ العَبْدُ يَوْمَ القِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلاَتُهُ ، فَإنْ صَلَحَتْ ، فَقَدْ أفْلَحَ وأَنْجَحَ ، وَإنْ فَسَدَتْ ، فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ ، فَإنْ انْتَقَصَ مِنْ فَرِيضَتِهِ شَيْءٌ ، قَالَ الرَّبُ عزوجل : انْظُرُوا هَلْ لِعَبدي من تطوّعٍ ، فَيُكَمَّلُ مِنْهَا مَا انْتَقَصَ مِنَ الفَرِيضَةِ ؟ ثُمَّ تَكُونُ سَائِرُ أعْمَالِهِ عَلَى هَذَا )) رواه التِّرمِذِيُّ ، وَقَالَ : (( حَدِيثٌ حَسَنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Faradhi ya kwanza atakayoulizwa Muislamu Siku ya Qiyaamah kuwa kaitekeleza - na kaitekeleza vilivyo ni Swalaah. Ikiwa aliitekeleza vilivyo basi amefaulu na kuokoka. Na kama faradhi yake imepungua chochote Rabb atasema angalieni Swalaah za Sunnah, na alizileta vilivyo? Ikiwa alifanya hivyo ataungiwaungiwa katika hizo faradhi alizoziharibu kidogo. Kisha amali nyengine zitahesabiwa hivyo hivyo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Share