15-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Safu ya Kwanza na Amri ya Kutimiza Safu ya Kwanza na Kuzinyoosha
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الصف الأول
والأمر بإتمام الصفوف الأُوَل وتسويتها والتراصّ فِيهَا
15-Mlango Wa Fadhila za Safu ya Kwanza na Amri ya Kutimiza Safu ya Kwanza na Kuzinyoosha
Hadiyth – 1
عن جابر بن سَمُرَة رضي الله عنهما ، قَالَ : خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ: (( ألاَ تَصُفُّونَ كَمَا تَصُفُّ المَلائِكَةُ عِندَ رَبِّهَا ؟ )) فَقُلنَا : يَا رَسُول اللهِ ، وَكَيفَ تُصَفُّ المَلائِكَةُ عِندَ رَبِّهَا ؟ قَالَ : (( يُتِمُّونَ الصُّفُوفَ الأُوَلَ ، وَيَتَرَاصُّونَ في الصَّفِّ )) رواه مُسلِم
Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja kutuswalisha naye akauliza: "Kwa nini hamnyooshi safu kama wanyoshavyo Malaaikah mbele ya Rabb wao?" Tukamwuliza: "Malaaikah wananyoshaje safu mbele ya Rabb wao?" Akajibu: "Wanakamilisha safu ya mwanzo, nao hujipanga katika safu zilizonyooka sambamba." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَوْ يَعْلَمُ النَّاسُ مَا فِي النِّدَاءِ وَالصَّفِّ الأَوَّلِ ، ثُمَّ لَمْ يَجِدُوا إلاَّ أنْ يَسْتَهِمُوا عَلَيْهِ لاسْتَهَمُوا )) متفقٌ عَلَيهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau kama watu wangejua fadhila za adhana (kuitikia) na kusimama katika safu ya kwanza, kisha wakawa hawakupata njia ya kudiriki isipokuwa kwa kupiga kura basi wangalipiga kura." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( خيْرُ صُفُوفِ الرِّجَالِ أوَّلُهَا ، وَشَرُّهَا آخِرُهَا ، وَخَيْرُ صُفُوفِ النِّسَاءِ آخِرُهَا ، وَشَرُّهَا أوَّلُهَا )) رواه مُسلِم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Safu bora ya wanaume ni ile ya mbele na safu yenye shari ni ile ya mwisho na bora ya safu kwa wanawake ni ile ya mwisho na safu yenye shari kwao ni ile ya mwanzo." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أبي سعيد الخدرِيِّ رضي الله عنه : أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم رأى في أصْحَابِهِ تَأَخُّراً ، فَقَالَ لَهُمْ : (( تَقَدَّمُوا فَأتَمُّوا بِي ، وَلْيَأتَمَّ بِكُمْ مَنْ بَعْدَكُمْ ، لاَ يَزَالُ قَوْمٌ يَتَأَخَّرُونَ حَتَّى يُؤَخِّرَهُمُ الله )) رواه مُسلِم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaona baadhi ya Swahaaba zake wanachelewa nyuma (wakati wa Swalaah ya jamaa) akawaambia: "Njooni mbele nyuma yangu na wanaofuatia wasimame nyuma yenu. Na hawataacha watu kuendelea kujiweka nyuma mpaka Allaah awaweke nyuma." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أبي مسعود رضي الله عنه ، قال : كَانَ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يَمْسَحُ مَنَاكِبَنَا في الصَّلاَةِ ، وَيَقُولُ : (( اسْتَووا ولاَ تَخْتَلِفُوا فَتَخْتَلِفَ قُلُوبُكُمْ ، لِيَلِيَنِي مِنْكُمْ أُولُو الأحْلاَمِ وَالنُّهَى ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ )) رَوَاهُ مُسلِم .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiyagusa mabega yetu wakati wa Swalaah, na akisema: "Nyookeni na wala msipinde pinde kwani msiponyooka, Allaah Atatia khitilafu nyoyoni mwenu mkhitilafiane. Wasimame nyuma yangu wale waliobaleghe na wenye akili na ilimu, kisha wale wanaowafuata." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قال رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( سَوُّوا صُفُوفَكُمْ ؛ فَإنَّ تَسْوِيَةَ الصَّفِّ مِنْ تَمَامِ الصَّلاَةِ )) متفقٌ عَلَيهِ .
وفي رواية للبخاري : (( فَإنَّ تَسْوِيَةَ الصُّفُوفِ مِنْ إقَامَةِ الصَّلاَةِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nyoosheni safu zenu kwani kunyoosha safu ni katika kukamilisha safu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: "Hakika kunyoosha safu ni katika kusimamisha Swalaah."
Hadiyth – 7
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : أُقِيمَتِ الصَّلاَةُ فَأقْبَلَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم بِوَجْهِهِ ، فَقَالَ : (( أقِيمُوا صُفُوفَكُمْ وَتَرَاصُّوا ؛ فَإنِّي أرَاكُمْ مِنْ وَرَاءِ ظَهْرِي )) رواه البُخَارِيُّ بلفظه ، ومسلم بمعناه .
وفي رواية للبخاري: وَكَانَ أَحَدُنَا يُلْزِقُ مَنْكِبَهُ بِمَنْكِبِ صَاحِبِهِ وَقَدَمَهُ بِقَدَمِهِ.
Na kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Siku moja palikuwa pamekimiwa, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akageuka akatukabili, akasema: "Nyoosheni safu zenu, najipangeni kwani ninawaona nyuma ya mgongo wangu." [Al-Bukhaariy kwa lafdhi hiyo na Muslim kwa maana yake.
Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: "Kila moja wetu alikuwa akiambatanisha bega la mwenziwe aliye karibu naye, na hivyo hivyo mguu wake na wa mwenziwe katika safu."
Hadiyth – 8
وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : سمعت رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ ، أوْ لَيُخَالِفَنَّ اللَّهُ بَيْنَ وُجُوهِكُمْ )) متفقٌ عَلَيهِ .
وفي رواية لمسلم : أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يُسَوِّي صُفُوفَنَا ، حَتَّى كَأنَّمَا يُسَوِّي بِهَا القِدَاحَ حَتَّى رَأى أنَّا قَدْ عَقَلْنَا عَنْهُ ، ثُمَّ خَرَجَ يَوماً فَقَامَ حَتَّى كَادَ يُكَبِّرُ ، فَرَأى رَجُلاً بَادِياً صَدْرُهُ مِنَ الصَّفِّ ، فَقَالَ : (( عِبَادَ اللهِ ، لتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ ، أو لَيُخَالِفَنَّ اللهُ بَيْنَ وُجُوهِكُمْ )) .
An-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Pangeni safu zenu, au sivyo Allaah Atabadilisha nyuso zenu (yaani kuwaingisha baina yenu uadui, bughudha na khitilafu ya mioyo yenu) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Muslim: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipanga safu zetu kama kwamba anapanga mishale katika ala, mpaka akatuona tumemfahamu. Akatoka siku moja na kusimama mpaka akakaribia kupiga takbira ya kwanza ya Swalaah, hapo akamuona mtu ametoa kifua chake nje ya safu, akasema: 'Enyi waja wa Allaah! WaLlaahi zipangeni safu zenu sawa, au kama sivyo Allaah Atazibadilisha nyuso zenu (kuwa za wanyama)."
Hadiyth – 9
وعن البراءِ بن عازِبٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم يَتَخَلَّلُ الصَّفَّ مِنْ نَاحِيَةٍ إلى نَاحِيَةٍ ، يَمْسَحُ صُدُورَنَا وَمَنَاكِبَنَا ، وَيَقُولُ : (( لا تَخْتَلِفُوا فَتَخْتَلِفَ قُلُوبُكُمْ )) وكانَ يَقُولُ : (( إنَّ اللهَ وَمَلائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى الصُّفُوفِ الأُوَلِ )) رواه أبُو دَاوُدَ بإسناد حسن .
Na kutoka kwa Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akipita kati ya safu toka mwanzo mpaka mwisho kuzinyoosha huku akisema: "Msizipindishe safu zenu ili Allaah Asizipindishe nyoyo zenu mkawa mmoja dhidi ya mwengine." Na alikuwa akisema: "Hakika Allaah na Malaaika Wake wanamimina baraka Zao juu ya safu ya mwanzo." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]
Hadiyth – 10
وعن ابن عمر رَضِيَ اللهُ عَنهُما : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أقيمُوا الصُّفُوفَ ، وَحَاذُوا بَيْنَ المَنَاكِبِ ، وَسُدُّوا الخَلَلَ ، وَلِينوا بِأيْدِي إخْوانِكُمْ ، ولاَ تَذَرُوا فُرُجَاتٍ للشَّيْطَانِ ، وَمَنْ وَصَلَ صَفّاً وَصَلَهُ اللهُ ، وَمَنْ قَطَعَ صَفّاً قَطَعَهُ اللهُ )) رواه أبُو دَاوُدَ بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nyoosheni safu zenu na mlinganishe mabega yenu na jazeni mapengo (nafasi) katika safu zenu na kuweni wapole na wema kwa ndugu zenu na wala msiache mapengo kwa shetani. Na Allaah humkamilishia yake anayekamilisha safu na asiyekamilisha safu Allaah Hamkamilishii yake." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 11
وعن أنس رَضِيَ اللهُ عَنهُ : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( رُصُّوا صُفُوفَكُمْ ، وَقَارِبُوا بَيْنَهَا ، وَحَاذُوا بِالأعْنَاقِ ؛ فَوَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إنِّي لأَرَى الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ مِنْ خَلَلِ الصَّفِّ ، كَأَنَّهَا الحَذَفُ )) حديث صحيح رَوَاهُ أبُو دَاوُدَ بإسنادٍ عَلَى شرط مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nyoosheni safu zenu, na karibianeni baina yake, na linganisheni shingo zenu. Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake kwani mimi namuona shetani anajipenyeza penyeza kwenye safu kama kwamba ni vitoto vya kondoo." [Hadiyth Swahiyh iliyopokewa na Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyoafikiana na sharti zilizowekwa na Muslim]
Hadiyth – 12
وعن أنس رَضِيَ اللهُ عَنهُ : أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أتِمُّوا الصَّفَّ المُقَدَّمَ ، ثُمَّ الَّذِي يَلِيهِ ، فَمَا كَانَ مِنْ نَقْصٍ فَلْيَكُنْ في الصَّفِّ المُؤَخَّرِ )) رواه أبُو دَاوُدَ بإسناد حسن .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kamilisheni safu ya mwanzo kisha inayofuata na kama kuna upungufu basi uwe tu katika safu ya mwisho." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Hasan]
Hadiyth – 13
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عَنها ، قالت : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ وَمَلاَئِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى مَيَامِنِ الصُّفُوفِ )) رواه أبُو دَاوُدَ بإسنادٍ عَلَى شرط مسلم ، وفيه رجل مُخْتَلَفٌ في تَوثِيقِهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah na Malaaika Zake wanawarehemu watu wanaoswali kuliani mwa safu." [Abu Daawuwd kwa Isnaad na sharti ya Muslim, na katika wapokezi yupo mtu ambaye wametafautiana wanazuoni juu ya uaminifu wake].
Hadiyth – 14
وعن البراء رَضِيَ اللهُ عَنهُ ، قَالَ : كُنَّا إذَا صَلَّيْنَا خَلْفَ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم أحْبَبْنَا أنْ نَكُونَ عَنْ يَمِينهِ ، يُقْبِلُ عَلَيْنَا بِوَجْهِهِ ، فَسَمِعْتُهُ يَقُولُ : (( رَبِّ قِني عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ - أو تَجْمَعُ - عِبَادَكَ )) رواه مُسلِمٌ .
Na Al-Baraa (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Tulikuwa tunaswali nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tunapenda kuwa upande wake wa kulia, anatuelekea kwa uso wake, anasema: "Rabb wangu niepushe adhabu Yako siku utakayofufua au Utakayokusanya waja Wako." [Muslim]
Hadiyth – 15
وعن أبي هريرة رَضِيَ اللهُ عَنهُ ، قَالَ: قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( وَسِّطُوا الإمَامَ ، وَسُدُّوا الخَلَلَ )) رواه أبُو دَاوُد .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mfanyeni Imamu awe katikati na jazeni mapengo." [Abuu Daawuwd]