004-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Mnyama Ambaye Hakutajwa Kwenye Qur-aan Au Hadiyth Za Rasuli, Na Waarabu Wakamwona Mbaya Hafai Kuliwa, Je Litazingatiwa Hilo?

 

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

004-Je, Mnyama Ambaye Hakutajwa Kwenye Qur-aan Au Hadiyth Za Rasuli, Na Waarabu Wakamwona Mbaya Hafai Kuliwa, Je Litazingatiwa Hilo?

 

 

 

·        Je, Mnyama Ambaye Hakutajwa Kwenye Qur-aan Au Hadiyth Za Rasuli, Na Waarabu Wakamwona Mbaya Hafai Kuliwa, Je Litazingatiwa Hilo?  [Al-Mughniy (8/585), Ibn ‘Aabidiyna (5/194) na Matwaalibu Ulin Nuhaa (6/311)].

 

 

Ikiwa katika Qur-aan au Sunnah hakuna naswi idulishayo uhalali au uharamu wa mnyama fulani,  baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kwamba itabidi turudi kwa Waarabu.  Kama Waarabu watamwona mnyama huyo ni mzuri analika, basi atakuwa halali, na kama watamwona mbaya hafai kuliwa, basi atakuwa ni haramu.  Na hii ni kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:

 

"وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ"

 

“Na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vilivyo vibaya.  [Al-A’araaf: 157].

 

Ibn Qudaamah (Rahimahul Laah) akiizungumzia maana ya Aayah hii amesema:  

 

“Yaani, mnyama ambaye Waarabu wanamwona kuwa mzuri na anafaa kuliwa, basi huyo ni halali, na yule wanayemwona kuwa mbaya hafai kuliwa, basi huyo ni haramu.  Na Waarabu ambao kipimo chao cha kumwona mnyama huyu anafaa na kuwa mwingine hafai na ambacho kinazingatiwa, ni watu wa Al-Hijaaz, watu waishio kwenye miji.  Kwa kuwa hawa ndio ambao Qur-aan Kariym iliteremka kwao na maneno yake yakaelekezwa kwao pamoja na Sunnah ya Nabiy.  Hivyo matamshi yake mengi yanarejea kwenye ada na desturi zao zaidi kuliko watu wengineo”.

 

 

Share