020-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kula Toka Pembezoni Mwa Chakula Na Si Kutoka Katikati Yake
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Adabu Za Kula
020-Kula Toka Pembezoni Mwa Chakula Na Si Kutoka Katikati Yake
4- Kula Toka Pembezoni Mwa Chakula Na Si Kutoka Katikati Yake
Toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الْبَرَكَة تَنْزِلُ فِيْ وَسَطِ الطَّعَامِ ، فَكُلُوا مِنْ حَافَتَيْهِ ، وَلاَ تَأْكُلُوا مِنْ وَسَطِهِ"
“Baraka inateremka katikati ya chakula, basi kuleni toka pambizo zake, na msile toka katikati yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3772), Ibn Maajah (3277) na Ahmad (1/343-345)].