028-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kuosha Mkono Ili Kuondosha Harufu Ya Chakula
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Adabu Za Kula
028-Kuosha Mkono Ili Kuondosha Harufu Ya Chakula
13- Kuosha Mkono Ili Kuondosha Harufu Ya Chakula
Toka kwa Abu Hurayrah, amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا بَاتَ أَحَدُكُمْ وَفِيْ يَدِهِ غَمَرٌ فَأَصَابَهُ شَيْءٌ ، فَلَا يَلُومَنَّ إِلَّا نَفْسَهُ"
“Ikiwa mmoja wenu atalala na hali ana uchafu mkononi mwake, halafu akapatwa na lolote, basi asilaumu chochote ila ajilaumu yeye mwenyewe.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1860), Abu Daawuwd (3852), Ibn Maajah (3297) na Ahmad (8175)].
…………………