027-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kumwombea Du’aa Aliyeandaa Au Kualika Chakula
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Adabu Za Kula
027-Kumwombea Du’aa Aliyeandaa Au Kualika Chakula
12- Kumwombea Du’aa Aliyeandaa Au Kualika Chakula. Kati ya du’aa zilizothibiti kwa hilo ni:
"أَفْطَـرَ عِنْدَكُمُ الصَّـائِمُوْنَ ، وَأَكَلَ طَعَامَـكُمُ الأبْـرَارُ ، وَصَلَّـتْ عَلَـيْكُمُ الملائِكَـةُ"
“Wamefungua kwenu waliofunga, na wamekula chakula chenu watu wema, na Malaika wamewaombeeni rahmah”. [Hadiyth Swahiyh kwa wenza wake. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3854), Ibn Maajah (1747) na wengineo].
"اللّهُـمَّ بارِكْ لَهُمْ فيما رَزَقْـتَهُم، وَاغْفِـرْ لَهُـمْ وَارْحَمْهُمْ"
“Ee Allaah! Wabarikie katika Ulivyowaruzuku, Waghufirie na Warehemu”.
[Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (3805), At-Tirmidhiy (3500) na Abu Daawuwd (3241)].