026-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kumhimidi Allaah Na Kuomba Du’aa Baada Ya Kumaliza Kula

 

 

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

 

Adabu Za Kula

 

026- Kumhimidi Allaah Na Kuomba Du’aa Baada Ya Kumaliza Kula

 

 

 

 

10 -11 –  Kumhimidi Allaah Na Kuomba Du’aa Baada Ya Kumaliza Kula

 

Toka kwa Anas, amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى لَيَرْضَى عَنِ العَبْدِ أَنْ يَأْكُلَ الأكْلَةَ فَيَحْمَدُهُ عَلَيْهِ أَوْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا"

 

“Hakika Allaah Humridhia kwa yakini mja anayekula mlo mmoja tu (au tonge moja tu) akamshukuru Allaah kwa mlo huo, au anayekunywa mara moja tu (au funda moja tu) akamshukuru Allaah kwa unywaji huo”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2724) na At-Tirmidhiy (1816)].

 

Matamshi mengi ya himdi na du’aa yamethibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumaliza kula.  Kati yake ni:

 

1-  "الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي كَفَانَا وَأَرْوَانَا، غَيْرَ مَكْفِيٍّ، وَلاَ مَكْفُورٍ" 

 

Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Ametutosheleza mahitajio yetu na Akatuondoshea kiu, hazilipiki (Fadhila Zake) wala hazikanushiki.  [Hadiyth  Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5459)].

 

 

2- "الْحَمْـدُ للهِ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُبـارَكاً فِيْهِ، غَيْرَ مَكْفِيٍّ وَلا مُوَدَّعٍ وَلا مُسْتَغْـنىً عَنْـهُ رَبَّـنا"

 

Himdi Anastahiki Allaah, himdi zilizo nyingi, zilizo njema na zilizojaa baraka tele ndani yake, haziwezi kulipika, wala kuachwa, wala kutohitajiwa tena, ee Rabbi wetu”.  [Hadiyth  Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5458), Abu Daawuwd (3849), Ibn Maajah (3284 na Ahmad (5/256)].

 

3- "الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِيْ أَطْعَمَ وَسَقَى وَسَوَّغَهُ وَجَعَلَ لَهُ مَخْرَجًا"

 

“Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Amelisha, Amenywesha, Akakifanya (chakula) kuwa chepesi kuingia mwilini, na Akakiwekea njia ya kutoka mwilini.”  [Hadiyth  Swahiyh.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3851) na Ibn As-Sunniy].

 

4- "اللّهُمَّ أَطْعَمْتَ وَسَقَيْتَ وَأَغْنَيْتَ وَأَقْنَيْتَ وَهَدَيْتَ وَأَحْيَيْتَ ، فَلَكَ الحَمْدُ عَلَى مَا أَعْطَيْتَ"

 

“Ee Allaah! Umelisha, Umenywesha, Umetosheleza, Umekinaisha, Umeongoa, na Umehuisha.  Basi ni Yako Himdi kwa yote Uliyotoa”.  [Hadiyth  Hasan.  Imekharijiwa na Ahmad katika “Al-Musnad” nambari 1600].

 

 

Share