025-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji:Kulamba Vidole Na Sahani Kabla Ya Kuosha Mkono Au Kuupangusa

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

Adabu Za Kula

 

025-Kulamba Vidole Na Sahani Kabla Ya Kuosha Mkono Au Kuupangusa

 

 

 

 

9- Kulamba Vidole Na Sahani Kabla Ya Kuosha Mkono Au Kuupangusa

 

Toka kwa Jaabir:

 

"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِلَعْقِ الْأَصَابِعِ وَالصَّفْحَةِ ، وَقَالَ : "إِنَّكُمْ لَا تَدْرُونَ: فِي أَيَّهِ الْبَرَكَةُ؟ ".

 

Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kulamba vidole na sahani kwa kusema: “Hakika nyinyi hamjui wapi ilipo baraka yake”. [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2033)].

 

 

Share