024-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kulila Tonge Likianguka Baada Ya Kulipangusa Uchafu
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Adabu Za Kula
024-Kulila Tonge –Likianguka- Baada Ya Kulipangusa Uchafu
8- Kulila Tonge –Likianguka- Baada Ya Kulipangusa Uchafu
Toka kwa Jaabir amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أَحَدِكُمْ فَلْيَأْخُذْهَا ، فَلْيُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنَ الأَذَى وَلْيَأْكُلْهَا ، وَلاَ يَدَعْهَا لِلشَّيْطَانِ"
“Likianguka tonge la mmoja wenu basi aliokote, kisha alipanguse uchafu uliolipata na alile, na wala asiliache kwa shaytwaan.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2033)].