023-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Watu Wale Kwa Pamoja Na Mtu Asile Peke Yake
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Adabu Za Kula
023-Watu Wale Kwa Pamoja Na Mtu Asile Peke Yake
7- Watu Wale Kwa Pamoja Na Mtu Asile Peke Yake
Kwa kuwa mikono mingi kwenye chakula hukiongezea baraka kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"طَعَامُ الاِثْنَيْنِ كَافِي الثَّلاَثَةِ وَطَعَامُ الثَّلاَثَةِ كَافِي الأَرْبَعَةِ"
“Chakula cha wawili huwatosha watatu, na chakula cha watatu huwatosha wanne”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5392) na Muslim (2058)].
Imesimuliwa kwamba Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walisema:
"يَا رَسُوْلَ اللهِ ، إِنَّا نَأْكُلُ وَلاَ نَشْبَعُ ، فَقَالَ : فَلَعَلَّكُمْ تَفْتَرِقُوْنَ؟ قَالُوْا نَعَمْ ، قَالَ : فَاحْتَمِعُوْا عَلَى طَعَامِكُمْ ، وَذْكُرُوا اسْمَ الله ، يُبَارِكْ لَكُمْ فِيْهِ"
“Ee Rasuli wa Allaah! Mbona sisi tunakula na wala hatushibi?! Rasuli akawaambia: Huenda nyinyi mnakula kila mmoja kivyake. Wakasema: Ni kweli. Akasema: Basi jumuikeni pamoja katika chakula chenu, na litajeni Jina la Allaah, na Yeye Atawabarikieni ndani yake”. Hadiyth hii ni Dhwa’iyf.