022-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Asikitie Doa Chakula Au Kukisema Vibaya Kama Hakukipenda
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Adabu Za Kula
022-Asikitie Doa Chakula Au Kukisema Vibaya Kama Hakukipenda
6- Asikitie Doa Chakula Au Kukisema Vibaya Kama Hakukipenda
Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"مَا عَابَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ طَعَامًا قَطُّ ، إِن اشْتَهَاهُ أَكَلَهُ ، وَإِنْ كَرِهَهُ تَرَكَهُ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakukitia doa kamwe chakula. Akikitamani hukila, na kama hakukipenda hukiacha”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5409) na Muslim (2064)].
