33-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora wa Kisimamo cha Usiku
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل قيام الليل
33-Mlango Wa Ubora wa Kisimamo cha Usiku
قال الله تَعَالَى :
وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾
Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kwa kuisoma (Qur-aan) ikiwa ni ziada kwako. Asaa Rabb wako Akakuinua cheo cha kuhimidiwa (kusifika). [Al-Israa: 79]
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا ﴿١٦﴾
Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini. [As-Sajdah: 16]
كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾
Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha. [Adh-Dhaariyaat: 17]
Hadiyth – 1
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم يَقومُ مِنَ اللَّيْلِ حَتَّى تَتَفطَّرَ قَدَمَاهُ ، فَقُلْتُ لَهُ : لِمَ تَصْنَعُ هَذَا ، يَا رَسُولَ الله ، وَقَدْ غُفِرَ لَكَ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأخَّرَ ؟ قَالَ : (( أفَلاَ أكُونُ عَبْداً شَكُوراً! )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وَعَن المُغِيرَةِ بن شُعبة نَحْوهُ متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Swalaah ya usiku mpaka miguu yake ikivimba. Nikamwambia: "Kwa nini unafanya hivi ee Rasuli wa Allaah na haliyakuwa Allaah amekusamehe madhambi yako yaliyopita na ya baadaye?" Akasema: "Je, basi nisiwe mja mwenye kushukuru?" [Al-Bukhaariy na Muslim] Na mfano wake katika Swahiyh mbili katika riwaayah ya Mughiyrah bin Shu'bah.
Hadiyth – 2
وعن علي رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم طَرَقَهُ وَفَاطِمَةَ لَيْلاً ، فَقَالَ : (( أَلاَ تُصَلِّيَانِ ؟ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda kwake usiku akiwa na mkewe Faatwimah na akauliza: "Mbona hamuswali (Tahajjud)?" [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai]
Hadiyth – 3
وعن سالم بن عبدِ الله بن عمر بن الخطاب رضي الله عنهما ، عن أبيِهِ : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( نِعْمَ الرَّجُلُ عَبْدُ اللهِ ، لَوْ كَانَ يُصَلِّي مِنَ اللَّيلِ )) قَالَ سالِم : فَكَانَ عَبدُ اللهِ بَعْدَ ذَلِكَ لاَ يَنامُ مِنَ اللَّيلِ إِلاَّ قَلِيلاً . متفقٌ عَلَيْهِ .
Saalim bin 'Abdullaah bin 'Umar bin Al-Khatwaab kutoka kwa babake (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "'Abdullaah ni mtu mzuri na bora sana lau angekua anaswali Swalaah ya usiku." Amesema Saalim: "Baada ya hapo 'Abdullaah hakuwa akilala usiku isipokuwa kidogo." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن عبد الله بن عَمرو بن العاصِ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا عَبدَ اللهِ ، لاَ تَكُنْ مِثْلَ فُلانٍ ؛ كَانَ يَقُومُ اللَّيلَ فَتَرَكَ قِيَامَ اللَّيلِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
'Abdillaah bin 'Amru bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee 'Abdillaah usiwe mfano wa fulani ambaye alikuwa akiswali Swalaah ya usiku kisha akaacha kisimamo hicho cha usiku." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن ابن مسعودٍ رضي الله عنه ، قَالَ : ذُكِرَ عِنْدَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم رَجُلٌ نَامَ لَيْلَةً حَتَّى أصْبَحَ ، قَالَ : (( ذَاكَ رَجُلٌ بَالَ الشَّيطَانُ في أُذُنَيْهِ - أَوْ قَالَ : في أُذُنِهِ - )) متفقٌ عَلَيْهِ
Na Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Kuna mtu mmoja alitajwa mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amelala usiku wote mpaka ikafika asubuhi, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Huyo ni mtu ambaye shetani amemkojolea, masikioni mwake" au alisema: "Katika sikio lake." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai]
Hadiyth – 6
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يَعْقِدُ الشَّيطَانُ عَلَى قَافِيَةِ رَأسِ أحَدِكُمْ ، إِذَا هُوَ نَامَ ، ثَلاَثَ عُقَدٍ ، يَضْرِبُ عَلَى كُلِّ عُقْدَةٍ : عَلَيْكَ لَيْلٌ طَويلٌ فَارْقُدْ، فَإن اسْتَيقَظَ ، فَذَكَرَ اللهَ تَعَالَى انحَلَّتْ عُقْدَةٌ ، فَإنْ تَوَضّأ ، انْحَلّتْ عُقدَةٌ ، فَإنْ صَلَّى ، انْحَلَّتْ عُقَدُهُ كُلُّهَا ، فَأصْبَحَ نَشِيطاً طَيِّبَ النَّفْسِ ، وَإلاَّ أصْبحَ خَبيثَ النَّفْسِ كَسْلاَنَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Shetani anafunga kwenye kichogo cha mmoja wenu anapolala fundo tatu anapiga juu ya kila fundo 'lala usiku mrefu' na anapoamka mja na akamtaja Allaah linafunguka fundo na akitawadha linafunguka fundo la pili na akiswali linafunguka fundo la mwisho na atafika asubuhi akiwa mwenye nguvu mchangamfu mwenye nafsi nzuri na kama si hivyo atafika asubuhi akiwa na nafsi mbaya mvivu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd na An-Nasaai]
Hadiyth – 7
وعن عبد الله بن سلام رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أيُّهَا النَّاسُ : أفْشُوا السَّلامَ ، وَأطْعِمُوا الطَّعَامَ ، وَصَلُّوا بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ ، تَدْخُلُوا الجَنَّةَ بِسَلاَمٍ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Salaam (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Enyi watu! Enezeni ujumbe (salamu) wa Kiislamu, na walisheni masikini na Swalini Swalaah ya usiku wakati watu wengine wamelala, mtaingia Peponi kwa amani." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 8
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( أفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ : شَهْرُ اللهِ المُحَرَّمُ ، وَأفْضَلُ الصَّلاَةِ بَعْدَ الفَرِيضَةِ : صَلاَةُ اللَّيْلِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Funga bora baada ya Ramadhwaan ni mwezi wa Allaah Muharram. Na Swalaah bora baada ya faradhi ni Swalaah ya usiku." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( صَلاةُ اللَّيْلِ مَثْنَى مَثْنَى ، فَإذَا خِفْتَ الصُّبْحَ فَأوْتِرْ بِوَاحِدَةٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalaah ya usiku ni rakaa mbili mbili na unapoogopea kuingia kwa asubuhi swali witri rak'ah moja." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na Abu Daawuwd]
Hadiyth – 10
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي مِنَ اللَّيْلِ مَثْنَى مَثْنَى ، وَيُوتِرُ بِرَكْعَةٍ .متفقٌ عَلَيْهِ .
Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akiswali Swalaah ya usiku rak'ah mbili mbili na akimalizia na rak'ah moja ya witri." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 11
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُفْطِرُ مِنَ الشَّهْرِ حَتَّى نَظُنَّ أنْ لاَ يَصُومَ مِنْهُ ، وَيَصُومُ حَتَّى نَظُنَّ أنْ لاَ يُفْطِرَ مِنْهُ شَيْئاً ، وَكَانَ لاَ تَشَاءُ أنْ تَرَاهُ مِنَ اللَّيلِ مُصَلِّياً إِلاَّ رَأيْتَهُ ، وَلاَ نَائِماً إِلاَّ رَأيْتَهُ . رواه البخاري .
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akila katika mwezi mpaka tukidhani hatafunga katika mwezi huo, na akifunga mpaka tukidhani hatofungua katika mwezi huo. Na ukitaka kumuona akiswali usiku utaona hilo na ukitaka kumuona akiwa amelala usiku utamuona pia." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 12
وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يُصَلِّي إحْدَى عَشْرَةَ رَكْعَةً – تَعْنِي في اللَّيلِ – يَسْجُدُ السَّجْدَةَ مِنْ ذَلِكَ قَدْرَ مَا يَقْرَأُ أحَدُكُمْ خَمْسِينَ آيَةً قَبْلَ أنْ يَرْفَعَ رَأسَهُ ، وَيَرْكَعُ رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلاَةِ الفَجْرِ ، ثُمَّ يَضْطَجِعُ عَلَى شِقِّهِ الأيْمَنِ حَتَّى يَأتِيَهُ المُنَادِي للصَلاَةِ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali rak'ah kumi na moja yaani usiku, anasujudu katika hizo rak'ah sawa na kisomo cha ayah hamsini kabla ya kunyanyua kichwa chake. Na alikuwa akiswali rak'ah mbili kabla ya Swalaah ya Alfajiri, kisha alikuwa akijilaza kwa ubavu wake wa kulia mpaka anapokuja muadhini kumuita kwa ajili ya Swalaah." [Al-Bukhaariy].
Hadiyth – 13
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : مَا كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَزيدُ - في رَمَضَانَ وَلاَ في غَيْرِهِ - عَلَى إحْدَى عَشْرَةَ رَكْعَةً : يُصَلِّي أرْبَعاً فَلاَ تَسْألْ عَنْ حُسْنِهِنَّ وَطُولِهِنَّ ، ثُمَّ يُصَلِّي أرْبَعاً فَلاَ تَسْألْ عَنْ حُسْنِهِنَّ وطُولِهِنَّ، ثُمَّ يُصَلِّي ثَلاثاً. فَقُلتُ: يَا رسولَ اللهِ ، أتَنَامُ قَبْلَ أنْ تُوتِرَ؟ فَقَالَ: (( يَا عَائِشَة، إنَّ عَيْنَيَّ تَنَامَانِ وَلاَ يَنَامُ قَلْبِي)) متفقٌ عَلَيْهِ.
Na amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) : Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa haswali zaidi ya rak'ah kumi na moja katika Ramadhwaan wala katika miezi mingine. Alikuwa akiswali rak'ah nne, wala usiulize kuhusu urefu wake! Kisha alikuwa akiswali rak'ah nne wala usiulize uzuri, ukamilifu na urefu wake! Kisha alikuwa anaswali rak'ah tatu. Nikamuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! je, unalala kabla ya kuswali witri?" Akasema: "Ee 'Aaishah! Hakika macho yangu yanalala lakini moyo wangu haulali." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 14
وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَنَامُ أوّلَ اللَّيلِ ، وَيَقُومُ آخِرَهُ فَيُصَلِّي . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa analala mwanzo wa usiku na baadae akiamka mwisho wake (wa usiku) kwa ajili ya kuswali (Swalaah ya usiku)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 15
وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : صَلَّيْتُ مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم لَيْلَةً ، فَلَمْ يَزَلْ قائِماً حَتَّى هَمَمْتُ بِأَمْر سوءٍ ! قيلَ : مَا هَمَمْتَ ؟ قَالَ : هَمَمْتُ أنْ أجِلْسَ وَأدَعَهُ . متفقٌ عَلَيْهِ
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Niliswali pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) usiku naye akarefusha kisimamo mpaka nikaanza kufikiria jambo baya." Akaulizwa: "Hilo jambo baya ni lipi?" Alisema: "Nilifikiria kukaa na kuacha kumfuata (katika Swalaah)." [Ahmad, Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 16
وعن حذيفة رضي الله عنه ، قَالَ: صَلَّيْتُ مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ لَيْلَةٍ فَافْتَتَحَ البَقرَةَ ، فَقُلْتُ : يَرْكَعُ عِنْدَ المئَةِ ، ثُمَّ مَضَى ، فقلتُ : يُصَلِّي بِهَا في رَكْعَةٍ فَمَضَى ، فقلتُ : يَرْكَعُ بِهَا ، ثُمَّ افْتَتَحَ النِّسَاءَ فَقَرَأَهَا ، ثُمَّ افْتَتَحَ آلَ عِمْرَانَ فَقَرَأَهَا ، يَقرَأُ مُتَرَسِّلاً : إِذَا مَرَّ بآيةٍ فِيهَا تَسبيحٌ سَبَّحَ ، وَإذَا مَرَّ بسُؤَالٍ سَأَلَ ، وَإذَا مَرَّ بتَعَوُّذٍ تَعَوَّذَ ، ثُمَّ رَكَعَ ، فَجَعَلَ يَقُولُ : (( سُبْحَانَ رَبِّيَ العَظِيمِ )) فَكَانَ رُكُوعُهُ نَحواً مِنْ قِيَامِهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ ، رَبَّنَا لَكَ الحَمْدُ )) ثُمَّ قَامَ طَويلاً قَريباً مِمَّا رَكَعَ ، ثُمَّ سَجَدَ ، فَقَالَ : (( سُبْحَانَ رَبِّيَ الأَعْلَى )) فَكَانَ سجُودُهُ قَريباً مِنْ قِيَامِهِ. رواه مسلم.
Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Niliswali nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) usiku, Akaanza Suwrah Al-Baqarah. Nikasema atarukuu ayah ya mia, Akapita, Nikasema huenda akamaliza katika rakaa, lakini aliendelea. Nikasema ataiswalia rakaa moja, akapita, Alianza Suwrah An-Nisaa akaisoma, kisha akaanza Aal-'Imraan akaisoma, Akawa anasoma mutarassila (kisomo ambacho alikuwa akibainisha vilivyo kila herufi na kuzipatia haki zake) na anapofika katika ayah ya tasbihi, analeta tasbihi, na anapofika katika maombo huomba, na akifika ayah ya kujilinda anajilinda, Kisha akarukuu akawa anasema: 'Subhaana Rabbiyal 'Adhiym - Ametakasika Mola wangu Mtukufu'. Rukuu yake ilikuwa kama kisimamo chake, kisha akasema: 'Sami'a LLaahu liman hamidahu, Rabbanaa Lwalakal hamdu' - Allaah anamsikia anayemhimidi, Ee Rabb wetu kuhimidiwa ni Kwako'. Kisha akasimama kisimamo kirefu karibu ya alichorukuu. Kisha akasujudu akasema: 'Subhaana Rabbiyal a'alaa' - Ametakasika Rabb wangu Aliye juu.' Sijda yake ikakaribia kisimamo chake." [Muslim]
Hadiyth – 17
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : سُئِلَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أيُّ الصَّلاَةِ أفْضَلُ ؟ قَالَ : (( طُولُ القُنُوتِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: "Ni Swalaah gani iliyo bora?" Akasema: "Yenye kisimamo kirefu." [Muslim]
Hadiyth – 18
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أحَبُّ الصَّلاةِ إِلَى اللهِ صَلاةُ دَاوُدَ ، وَأحَبُّ الصِّيَامِ إِلَى اللهِ صِيَامُ دَاوُدَ ، كَانَ يَنَامُ نِصْفَ اللَّيلِ وَيَقُومُ ثُلُثَهُ وَيَنَامُ سُدُسَهُ وَيَصُومُ يَوماً وَيُفْطِرُ يَوْماً )) متفقٌ عَلَيْهِ
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amri bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalaah inayopendwa sana na Allaah Ta'aalaa ni Swalaah ya Daawuwd na funga inayopendeza sana mbele ya Allaah Ta'aalaa ni funga ya Daawuwd. Alikuwa akilala nusu ya usiku na kusimama kuswali thuluthi (1/3) yake na akilala sudusi (nusu ya thuluthi - 1/6) na alikuwa akifunga siku moja na akila siku ya pili." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 19
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ في اللَّيْلِ لَسَاعَةً، لاَ يُوَافِقُهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ يَسْألُ الله تَعَالَى خَيْراً مِنْ أمْرِ الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، إِلاَّ أعْطَاهُ إيَّاهُ ، وَذَلِكَ كُلَّ لَيْلَةٍ )) رواه مسلم .
Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika upo wakati usiku hatauwahi mtu yeyote Muislamu anayemuomba Allaah Ta'aalaa jambo lolote la kheri la unia na Aakhera ila Atampatia. Na hilo linakuwa kwa kila usiku." [Muslim]
Hadiyth – 20
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا قَامَ أحَدُكُمْ مِنَ اللَّيْلِ فَلْيَفْتَتِحِ الصَّلاَةَ بركْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu ;anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapoamka mmoja wenu kwa ajili ya kuswali Swalaah ya usiku aanze kwa rak'ah mbili nyepesi." [Muslim]
Hadiyth – 21
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ افْتَتَحَ صَلاَتَهُ بِرَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ . رواه مسلم .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa anapoamka kwa Swalaah ya usiku akianza kwa rakaa mbili nyepesi." [Muslim]
Hadiyth – 22
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا فَاتَتْهُ الصَّلاةُ مِن اللَّيْلِ مِنْ وَجَعٍ أَوْ غَيْرِهِ ، صَلَّى مِنَ النَّهَارِ ثِنْتَيْ عَشرَةَ ركْعَةً . رواه مسلم .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa inapompita Swalaah ya usiku kwa sababu ya maumivu au sababu nyengine yoyote, anaswali mchana rakaa kumi na mbili (za Sunnah)." [Muslim]
Hadiyth – 23
وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ نَامَ عَنْ حِزْبِهِ ، أَوْ عَنْ شَيْءٍ مِنْهُ ، فَقَرَأَهُ فيما بَيْنَ صَلاَةِ الفَجْرِ وصلاة الظُّهْرِ ، كُتِبَ لَهُ كَأنَّمَا قَرَأهُ مِنَ اللَّيْلِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote anayelala bila kutekeleza Hizb (ni anachojaalia mtu kufanya kwa nafasi yake kwa mfano kusoma Qur-aan au kuswali au kufanya amali nyengine yoyote) yake au sehemu ya hiyo, akawa ni mwenye kusoma baina ya Swalaah ya Alfajiri na Adhuhuri anaandikiwa ni kama amesoma usiku." [Muslim]
Hadiyth – 24
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( رَحِمَ اللهُ رَجُلاً قَامَ مِنَ اللَّيْلِ ، فَصَلَّى وَأيْقَظَ امْرَأَتَهُ ، فَإنْ أبَتْ نَضَحَ في وَجْهِهَا المَاءَ ، رَحِمَ اللهُ امْرَأَةً قَامَتْ مِنَ اللَّيْلِ ، فَصَلَّتْ وَأيْقَظَتْ زَوْجَهَا ، فَإن أبَى نَضَحَتْ فِي وَجْهِهِ المَاءَ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah amrehemu mtu anaamka usiku, akaswali, na akamuamsha mkewe. Akikataa anamnyunyizia maji usoni mwake. Allaah amrehemu mwanamke ambaye ameamka usiku ili kuswali (Swalaah ya usiku) na akamuamsha mumewe akikataa akamnyunyizia maji usoni mwake." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]
Hadiyth – 25
وعن أَبي هريرة وعن أَبي سعيدٍ رضي الله عنهما ، قالا : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أَيْقَظَ الرَّجُلُ أهْلَهُ مِنَ اللَّيْلِ فَصَلَّيَا - أَوْ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ جَمِيعاً ، كُتِبَا في الذَّاكِرِينَ وَالذَّاكِرَاتِ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Kutoka kwa Abu Huraiyrah na kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) wamesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mume anapomuamsha Mkewe wakati wa usiku na wakaswali pamoja - au wakaswali rak'ah mbili wote (kwa jamaa), wanaandikiwa kuwa ni miongoni mwa wenye kumdhukuru Allaah, katika wanaume na wanawake." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]
Hadiyth – 26
وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا نَعَسَ أحَدُكُمْ في الصَّلاَةِ ، فَلْيَرْقُدْ حَتَّى يَذْهَبَ عَنْهُ النَّوْمُ ، فَإنَّ أحَدَكُمْ إِذَا صَلَّى وَهُوَ نَاعِسٌ ، لَعَلَّهُ يَذْهَبُ يَسْتَغْفِرُ فَيَسُبَّ نَفْسَهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aaishah amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Akisinzia mmoja wenu naye anaswali basi alale mpaka usingizi unapomalizika. Hakika mmoja wenu anaposwali naye anasinzia hatafahamu maneno anayosema, hivyo huenda akawa anaitukana (anajilaani) nafsi yake badala ya kuomba msamaha." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
Hadiyth – 27
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا قَامَ أحَدُكُمْ مِنَ اللَّيْلِ ، فَاسْتَعْجَمَ القُرْآنَ عَلَى لِسَانِهِ ، فَلَمْ يَدْرِ مَا يَقُولُ ، فَلْيَضْطَجِع )) رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapoamka mmoja wenu usiku (Tahajjud) na akaona vigumu kutamka ayah za Qur-aan (inavyotakiwa) kwa ulimi wake, na akawa hajui anayosema basi alale." [Muslim]