34-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kuswali Swalaah ya Ramadhwaan Nayo ni Tarawehe
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب قيام رمضان وَهُوَ التراويح
34-Mlango Wa Kupendeza Kuswali Swalaah ya Ramadhwaan Nayo ni Tarawehe
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إيماناً وَاحْتِسَاباً غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusimama usiku katika mwezi wa Ramadhwaan kwa 'Ibadah hali ya kuwa na Imaani, na hali ya kutarajia kupata thawabu mtu huyo husamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُرَغِّبُ في قِيَامِ رَمَضَانَ مِنْ غَيْرِ أنْ يَأمُرَهُمْ فِيهِ بِعَزِيمَةٍ ، فيقولُ : (( مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إيمَاناً وَاحْتِسَاباً غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ )) رواه مسلم .
Na amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) : Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akihimiza kusimamisha usiku wa Ramadhwaan bila kuwaamuru wao kuwa ni lazima akisema: "Mwenye kusimama usiku Ramadhwaan kwa Imaani, na kutarajia thawabu huyo husamehewa madhambi yake yaliyotangulia." [Muslim]