38-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Wajibu wa Fungu na Kubainisha Fadhila za Fungu na Mambo Yanayohusiana Nayo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب وجوب صوم رمضان

وبيان فضل الصيام وَمَا يتعلق بِهِ

38-Mlango Wa Wajibu wa Fungu na Kubainisha Fadhila za Fungu na Mambo Yanayohusiana Nayo

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾

Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

 

أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ ۚ وَأَن تَصُومُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٤﴾

(Swiyaam ni) Siku za kuhesabika. Lakini atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa mashaka na kutaabika watoe fidia kulisha masikini. Na atakayefanya kwa khiari yake jema lolote, basi hilo ni bora kwake. Na mkifunga Swiyaam ni bora kwenu mkiwa mnajua.

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ  ﴿١٨٥﴾

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. [Al-Baqarah: 183-185]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( قَالَ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ : كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ لَهُ إِلاَّ الصِّيَام ، فَإنَّهُ لِي وَأنَا أجْزِي بِهِ ، وَالصِّيَامُ جُنَّةٌ ، فَإذَا كَانَ يَومُ صَوْمِ أحَدِكُمْ فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَصْخَبْ فإنْ سَابَّهُ أحَدٌ أَوْ قَاتَلَهُ فَلْيَقُلْ: إنِّي صَائِمٌ . وَالذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَخُلُوفُ فَمِ الصَّائِمِ أطْيَبُ عِنْدَ اللهِ مِنْ رِيحِ المِسْكِ . لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ يَفْرَحُهُمَا : إِذَا أفْطَرَ فَرِحَ بفطره ، وَإذَا لَقِيَ رَبَّهُ فَرِحَ بِصَوْمِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ روايةِ البُخَارِي .

وفي روايةٍ لَهُ : (( يَتْرُكُ طَعَامَهُ ، وَشَرَابَهُ ، وَشَهْوَتَهُ مِنْ أجْلِي ، الصِّيَامُ لي وَأنَا أجْزِي بِهِ ، وَالحَسَنَةُ بِعَشْرِ أمْثَالِهَا )) .

وفي رواية لمسلم : (( كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يضاعَفُ ، الحسنةُ بِعَشْرِ أمْثَالِهَا إِلَى سَبْعِمِئَةِ ضِعْفٍ . قَالَ الله تَعَالَى : إِلاَّ الصَّوْمَ فَإنَّهُ لِي وَأنَا أجْزِي بِهِ ؛ يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أجْلِي . للصَّائِمِ فَرْحَتَانِ : فَرْحَةٌ عِنْدَ فِطْرِهِ ، وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ . وَلَخُلُوفُ فِيهِ أطْيَبُ عِنْدَ اللهِ مِنْ رِيحِ المِسْكِ )) .

Abu Huraiyrah amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Allaah Ta'aalaa amesema: Kila 'Ibadah ya mwanadamu ni yake isipokuwa funga, hiyo ni Yangu na Mimi Nitailipa. Funga ni kinga, na ikiwa mmoja wenu amefunga asiropoke, wala asifanye zogo, yeyote akimtukana au akimpiga, na aseme, 'Mimi nimefunga." Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad iko Mikononi Mwake, harufu ya kinywa cha mfungaji ni nzuri zaidi kwa Allaah kuliko harufu ya miski. Mfungaji ana furaha mbili anazofurahia; Anapofuturu anafurahi futari yake, na atakapo kutana na Rabb wake atafurahia funga yake." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy] Na hii ni lafdhi ya riwaayah ya Al-Bukhaariy. 

Na katika riwaayah yake: "Anaacha chakula chake, kinywaji chake, na matamanio yake kwa ajili Yangu. Funga ni Yangu na Mimi Nitailipa na jema ni mara kumi mfano wake."

Na katika riwaayah ya Muslim: "Kila amali ya mwanadamu huzidishwa: Jema ni mara kumi hadi nyongeza mia saba. Amesema Allaah Ta'aalaa: 'Isipokuwa funga hiyo ni Yangu Nami nitailipa. Anaacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu.' Mfungaji ana furaha mbili: Furaha anapofuturu na atakapo kutana na Rabb wake. Na harufu ya kinywa cha mfungaji ni nzuri zaidi mbele ya Allaah kuliko harufu ya miski." 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ أنْفَقَ زَوْجَيْنِ في سَبِيلِ اللهِ نُودِيَ مِنْ أبْوَابِ الجَنَّةِ ، يَا عَبْدَ اللهِ هَذَا خَيرٌ ، فَمَنْ كَانَ مِنْ أهْلِ الصَّلاَةِ دُعِيَ مِنْ بَابِ الصَّلاَةِ ، وَمَنْ كَانَ مِنْ أهْلِ الجِهَادِ دُعِيَ مِنْ بَابِ الجِهَادِ ، وَمَنْ كَانَ مِنْ أهْلِ الصِّيَامِ دُعِيَ مِنْ بَابِ الرَّيَّانِ ، وَمَنْ كَانَ مِنْ أهْلِ الصَّدَقَةِ دُعِيَ مِنْ بَابِ الصَّدَقَةِ )) قَالَ أَبُو بَكْرٍ رضي اللهُ عنه : بِأبي أنْتَ وَأُمِّي يَا رسولَ اللهِ ! مَا عَلَى مَنْ دُعِيَ مِنْ تِلْكَ الأَبْوَابِ مِنْ ضَرورةٍ ، فهل يُدْعى أحَدٌ مِنْ تِلْكَ الأبوَابِ كُلِّهَا ؟ فَقَالَ : (( نَعَمْ ، وَأرْجُو أنْ تَكُونَ مِنْهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakaye toa vitu viwili katika njia ya Allaah, ataitwa kwenye milango ya Pepo, ee mtumwa wa Allaah, hii ni kheri. Atakayekuwa katika watu wa Swalaah, ataitwa katika mlango wa Swalaah, atakayekuwa katika watu wa Jihadi ataitwa katika mlango wa Jihaad na atakayekuwa katika watu wa funga ataitwa katika mlango wa Rayyan. Na atakayekuwa katika watu wa Swadaqah ataitwa katika mlango wa Swadaqah." Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) Akasema: "Fidia yako ni baba yangu na mam yangu, ee Rasuli wa Allaah hakuna dhara kwa atakayeitwa kwa milango yote. Je, kuna yeyote atakayeitwa milango hiyo yote?" Akasema: "Ndiyo na nataraji utakuwa miongoni mwa hao." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 3

وعن سهل بن سعد رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ في الجَنَّةِ بَاباً يُقَالُ لَهُ : الرَّيَّانُ ، يَدْخُلُ مِنْهُ الصَّائِمُونَ يَومَ القِيَامَةِ ، لاَ يَدْخُلُ مِنْهُ أحدٌ غَيْرُهُمْ ، يقال : أيْنَ الصَّائِمُونَ ؟ فَيَقُومُونَ لاَ يَدخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ ، فَإذَا دَخَلُوا أُغْلِقَ فَلَمْ يَدْخُلْ مِنْهُ أَحَدٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Peponi kuna mlango unaitwa Rayyan, wataingia katika mlango huo Siku ya Qiyaamah wafungaji na hataingia yeyote katika mlango huo asiyekuwa katika wao. Patasemwa, 'Wako wapi wafungaji?' Watasimama, na hatoingia katika mlango huo isipokuwa wao tu. Wakisha ingia utafungwa na haingii hapo yeyeote zaidi yao." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي سعيد الخدري رضي اللهُ عنه، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ عَبْدٍ يَصُومُ يَوْماً في سَبِيلِ اللهِ إِلاَّ بَاعَدَ اللهُ بِذَلِكَ اليَوْمِ وَجْهَهُ عَنِ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفَاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu Sa'iyd Al-Khudry (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna mja yeyote anafunga siku moja katika njia ya Allaah isipokuwa Allaah atauweka mbali uso wake na moto kwa hiyo siku aliyefunga, umbali wa safari ya miaka sabini." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إيمَاناً وَاحْتِسَاباً ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ 

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufunga Ramadhwaan hali ya kuwa na Imaani na kutarajia kupata thawabu husamehewa mtu huyo madhambi yaliyotangulia." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا جَاءَ رَمَضَانُ ، فُتِحَتْ أبْوَاب الجَنَّةِ ، وَغُلِّقَتْ أبْوَابُ النَّارِ ، وَصفِّدَتِ الشَّيَاطِينُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Inapoingia Ramadhwaan, inafunguliwa milango ya Pepo na ianfungwa milango ya moto na wanafungwa mashetani minyororo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ، وَأفْطِرُوا لِرُؤيَتِهِ، فَإنْ غَبِيَ عَلَيْكُمْ ، فَأكمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلاَثِينَ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ البخاري .

وفي رواية لمسلم : (( فَإنْ غُمَّ عَلَيْكُمْ فَصُومُوا ثَلاَثِينَ يَوْماً )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu HUraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Fungeni kwa kuonekana kwake na kuleni kwa kuonekana kwake, na ukizibwa juu yenu na mawingu basi kamilisheni Sha'baan siku thalathini." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Muslim: "Ikiwa haukuonekana kwenu basi fungeni siku thelathini."

 

 

 

 

Share