39-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukarimu na Kutenda Mema na Kuzidisha Mambo ya Kheri katika Mwezi wa Ramadhwaan na Kuongeza Hayo katika Kumi la Mwisho
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الجود وفعل المعروف والإكثار من الخير
في شهر رمضان والزيادة من ذَلِكَ في العشر الأواخر منه
39-Mlango Wa Ukarimu na Kutenda Mema na Kuzidisha Mambo ya Kheri katika Mwezi wa Ramadhwaan na Kuongeza Hayo katika Kumi la Mwisho
Hadiyth – 1
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم أجْوَدَ النَّاسِ ، وَكَانَ أجْوَدَ مَا يَكُونُ في رَمَضَانَ حِيْنَ يَلْقَاهُ جِبْريلُ ، وَكَانَ جِبْريلُ يَلْقَاهُ في كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ فَيُدَارِسُهُ القُرْآنَ ، فَلَرَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، حِيْنَ يَلْقَاهُ جِبرِيلُ أجْوَدُ بالخَيْرِ مِن الرِّيحِ المُرْسَلَةِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa mkarimu zaidi kwa watu katika mambo ya kheri na alikuwa mkarimu zaidi katika mwezi wa Ramadhwaan, wakati anapokutana na Jibriyl, Na Jibriyl alikuwa anakutana naye katika kila usiku wa Ramadhwaan na kumsomesha Qur-aan. Hivyo, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pindi alipokuw anakutana na Jibriyl alikuwa mkarimu zaidi katika mambo ya kheri kuliko upepo uliotumwa (pamoja na mvua) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا دَخَلَ العَشْر أحْيَا اللَّيْلَ ، وَأيْقَظَ أهْلَهُ ، وَشَدَّ المِئْزَرَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Zilipokuwa zinaanza siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhwaan Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali usiku kucha na akiwaamsha familia yake na kukaza mkanda wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]