40-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kutanguliza Ramadhwaan kwa Kufunga Siku Moja Baada ya Nusu ya Sha'baan Isipokuwa kwa Yule Aliyekuwa na Ada ya Kufunga Jumatatu na Alkhamis

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن تقدم رمضان بصوم بعد نصف

شعبان إِلاَّ لمن وصله بما قبله أَوْ وافق عادة لَهُ بأن كَانَ

عادته صوم الإثنين والخميس فوافقه

40-Mlango Wa Kukatazwa Kutanguliza Ramadhwaan kwa Kufunga Siku Moja Baada ya Nusu ya Sha'baan Isipokuwa kwa Yule Aliyekuwa na Ada ya Kufunga Jumatatu na Alkhamis

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ يَتَقَدَّمَنَّ أَحَدُكُم رَمَضَانَ بِصَوْمِ يَوْمٍ أَوْ يَوْمَيْنِ ، إِلاَّ أنْ يَكُونَ رَجُلٌ كَانَ يَصُومُ صَومَهُ ، فَليَصُمْ ذَلِكَ اليَوْمَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asitangulize mmoja wenu Ramadhwaan kwa funga ya siku moja au siku mbili isipokuwa kama mtu anayo funga yake anayofunga na aifunge siku hiyo." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَصُومُوا قَبْلَ رَمضَانَ ، صُومُوا لِرُؤيَتِهِ ، وَأفْطِرُوا لِرُؤيَتِهِ ، فَإنْ حَالَتْ دُونَهُ غَيَايَةٌ فَأكْمِلُوا ثَلاثِينَ يَوْماً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسنٌ صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msifunge kabla ya Ramadhwaan, fungeni kwa kuonekena kwake (mwezi) na kuleni kwa kuonekana kwake. Ikiwa kuna mawingu (hivyo kutoonekana mwezi) basi kamilisheni siku thalathini." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا بَقِيَ نِصْفٌ مِنْ شَعْبَانَ فَلاَ تَصُومُوا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Inapobakia nusu ya Sha'baan basi musifunge." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي اليقظان عمارِ بن يَاسِرٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : مَنْ صَامَ اليَوْمَ الَّذِي يُشَكُّ فِيهِ ، فَقَدْ عَصَى أَبَا القَاسِمِ صلى الله عليه وسلم . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema Abu Al-Yaqdhaan 'Ammaar bin Yaasir (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Mwenye kufunga siku yenye shaka amemuasi Abal Qaasim (yaani Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Share