44-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Amri kwa Mfungaji Kuhifadhi Ulimi Wake na Viungo Vyake kwa Kwenda Kinyume na Matusi na Mfano Wake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب أمر الصائم بحفظ لسانه وجوارحه
عن المخالفات والمشاتمة ونحوها
44-Mlango Wa Amri kwa Mfungaji Kuhifadhi Ulimi Wake na Viungo Vyake kwa Kwenda Kinyume na Matusi na Mfano Wake
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا كَانَ يَوْمُ صَوْمِ أَحَدِكُمْ ، فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَصْخَبْ ، فَإنْ سَابَّهُ أحَدٌ أَوْ قَاتَلَهُ ، فَلْيَقُلْ : إنِّي صَائِمٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ikiwa mmoja wenu amefunga basi asiseme maneno machafu na wala asifanye zogo, kama yeyote (katika watu) ikatokea kumtukana au kupigana naye na aseme, 'Mimi nimefunga'." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ لَمْ يَدَعْ قَوْلَ الزُّورِ وَالعَمَلَ بِهِ فَلَيْسَ للهِ حَاجَةٌ في أنْ يَدَعَ طَعَامَهُ وَشَرَابَهُ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote ambaye hataacha maneno ya uwongo na matendo machafu, Allaah hana haja kuacha kwake chakula na kinywaji." [Al-Bukhaariy].