45-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Masuala ya Fungu
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب في مسائل من الصوم
45-Mlango Wa Masuala ya Fungu
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا نَسِيَ أَحَدُكُمْ ، فَأكَلَ ، أَوْ شَرِبَ ، فَلْيُتِمَّ صَوْمَهُ ، فَإنَّمَا أطْعَمَهُ اللهُ وَسَقَاهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kama atasahau mmoja wenu akala na akanywa, basi na akamilishe funga yake, kwani Allaah Ndiye Aliyemlisha na ndiye Aliyemnywesha." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن لَقِيط بن صَبِرَةَ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قُلْتُ : يَا رسول الله ، أخْبِرْني عَنِ الوُضُوءِ ؟ قَالَ : (( أسْبغِ الوُضُوءَ ، وَخَلِّلْ بَيْنَ الأَصَابِعِ ، وَبَالِغْ في الاسْتِنْشَاقِ ، إِلاَّ أنْ تَكُونَ صَائِماً )) رواه أَبُو داود والترمذي، وقال : (( حديث حسن صحيح )).
Laqiytw bin Swabirah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Niliuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Nielezee kuhusu wudhuu?" Akasema: "Kamilisha wudhuu na safisha mashina ya vidole vyako na zidisha katika kupandisha maji puani ila utakapokuwa umefunga." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 3
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يُدْرِكُهُ الفَجْرُ وَهُوَ جُنُبٌ مِنْ أهْلِهِ ، ثُمَّ يَغْتَسِلُ وَيَصُومُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anafikiwa na Alfajiri hali ana janaba baada ya kujamiiana na mkewe, kisha anaoga na anaendelea na funga." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na Abu Daawuwd]
Hadiyth – 4
وعن عائشة وأم سلمة رضي الله عنهما ، قالتا : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يُصْبحُ جُنُباً مِنْ غَيْرِ حُلُمٍ ، ثُمَّ يَصُومُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Wamesema 'Aaishah na Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akipambazukiwa katika hali ya janaba bila ya kuwa ameota (kwa kujamiiana na mkewe), kisha anafunga." [Al-Bukhaariy na Muslim].