46-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kubainisha Fadhila ya Kufunga ya Mwezi wa Muharram na Sha'baan na Miezi Mitukufu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل صوم المحرم وشعبان والأشهر الحرم

46-Mlango Wa Kubainisha Fadhila ya Kufunga ya Mwezi wa Muharram na Sha'baan na Miezi Mitukufu

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ : شَهْرُ الله المُحَرَّمُ ، وَأفْضَلُ الصَّلاَةِ بَعدَ الفَرِيضَةِ : صَلاَةُ اللَّيْلِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Funga bora baada ya Ramadhwaan ni mwezi wa Allaah Muharram. Na Swalaah bora baada ya faradhi ni Swalaah ya usiku." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

عن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : لَمْ يكن النبي صلى الله عليه وسلم يَصُومُ مِنْ شَهْرٍ أكْثَرَ مِنْ شَعْبَانَ ، فَإنَّهُ كَانَ يَصُومُ شَعْبَانَ كُلَّهُ .

وفي رواية : كَانَ يَصُومُ شَعْبَانَ إِلاَّ قَلِيلاً . متفقٌ عَلَيْهِ .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hakuwa anafunga mwezi zaidi kuliko Sha'baan kwani alikuwa anafunga Sha'baan yote.

Na katika riwaayah nyingine: Alikuwa akifunga Sha'baan isipokuwa kwa siku chache. [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 3

وعن مُجِيبَةَ البَاهِليَّةِ ، عن أبيها أَوْ عمها : أنه أتى رسولَ اللهِ رضي اللهُ عنه ، ثُمَّ انطَلَقَ فَأَتَاهُ بَعْدَ سَنَةٍ – وَقَدْ تَغَيَّرَتْ حَالُهُ وَهيئَتُهُ – فَقَالَ : يَا رسولَ الله ، أمَا تَعْرِفُنِي ؟ قَالَ : (( وَمَنْ أنْتَ )) ؟ قَالَ : أَنَا الباهِليُّ الَّذِي جِئْتُك عام الأَوَّلِ . قَالَ : (( فَمَا غَيَّرَكَ ، وَقَدْ كُنْتَ حَسَنَ الهَيْئَةِ ! )) قَالَ : مَا أكَلْتُ طَعَاماً مُنْذُ فَارقتُكَ إِلاَّ بِلَيْلٍ . فَقَالَ رسولُ اللهِ رضي اللهُ عنه : (( عَذَّبْتَ نَفْسَكَ ! )) ثُمَّ قَالَ : (( صُمْ شَهْرَ الصَّبْرِ ، وَيَوماً مِنْ كُلِّ شَهْرٍ )) قَالَ : زِدْنِي ، فَإنَّ بِي قُوَّةً ، قَالَ : (( صُمْ يَوْمَيْن )) قَالَ : زِدْنِي ، قَالَ : (( صُمْ ثَلاثَةَ أيَّامٍ )) قَالَ : زِدْنِي ، قَالَ : (( صُمْ مِنَ الحُرُم وَاتركْ ، صُمْ مِنَ الحُرُمِ وَاتركْ ، صُمْ مِنَ الحُرُمِ وَاتركْ )) وقال بأصابِعه الثَّلاثِ فَضَمَّها ، ثُمَّ أرْسَلَهَا . رواه أَبُو داود .

Kutoka kwa Mujiyban Al-Baahiliyyah na kutoka kwa Babake au ami yake amesema: Alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kisha akaondoka, akamjia baada ya mwaka - hali na umbo lake limebadilika. Akasaema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hujanitambua?" Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Na wewe ni nani?" Akasema: "Mimi ni Al-Bukhaariy nilikuja mwaka uliopita." Akasema: "Na ni kitu gani kimekubadilisha na ulikuwa mzuri wa umbo?", Akajibu: "Sijala chakula tangu nilipoachana nawe, isipokuwa usiku tu." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akamwambia: "Umeiadhibu nafsi yako!" Kisha akamwambia: "Funga mwezi wa subira, na siku moja kila mwezi." Akasema: "Niongezee" akasema: "Funga siku tatu." Akasema: "Nizidihsie." Akamwambia: "Funga miezi mitukufu na uchache, funga, funga miezi mitukufu na uchache kufunga." Alisema kwa vidole vyake mara tatu, akavikunja, kisha akaviacha." [Abu Daawuwd]

 

 

 

 

Share