48-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Funga ya Arafah na 'Aashuuraa' na Ta'suu'aa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل صوم يوم عرفة وعاشوراء وتاسوعاء

48-Mlango Wa Fadhila za Funga ya Arafah na 'Aashuuraa' na Ta'suu'aa

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي قتادة رضي اللهُ عنه، قَالَ : سُئِلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم عن صَومِ يَوْمِ عَرَفَةَ ، قَالَ : (( يُكَفِّرُ السَّنَةَ المَاضِيَةَ وَالبَاقِيَةَ )) رواه مسلم .

Amesema Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Aliulizwa kuhusu funga ya siku ya Arafah. Akasema: "Hufuta madhambi ya mwaka uliopita na ujao." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم صَامَ يَومَ عاشوراءَ وَأمَرَ بِصِيامِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifunga siku ya 'Aashuwraa' na akawaamuru watu wafunge (siku hiyo)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي قتادة رضي اللهُ عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم سُئِلَ عَنْ صِيامِ يَوْمِ عَاشُوراءَ، فَقَالَ : (( يُكَفِّرُ السَّنَةَ المَاضِيَةَ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu funga ya 'Aashuwraa', akasema: "Inafuta madhambi ya mwaka uliopita." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لَئِنْ بَقِيتُ إِلَى قَابلٍ لأَصُومَنَّ التَّاسِعَ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nikibakia mpaka mwaka ujao nitafunga tarehe tisa (yaani katika mwezi wa Muharram, nayo inaitwa Ta'suw'aa)." [Muslim]

 

 

 

Share