01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila ya Jihaad
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الجهاد
01-Mlango Wa Fadhila ya Jihaad
قال الله تَعَالَى :
وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿٣٦﴾
Na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita nyote. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa. [At-Tawbah: 36]
كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾
Mmeandikiwa shariy’ah kupigana vita nako kunachukiza mno kwenu. Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni la kheri kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui. [Al-Buqarah: 216]
انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ ﴿٤١﴾
Tokeni mwende (ni sawa) mkiwa na hali ya wepesi na mkiwa na hali ya uzito na fanyeni Jihaad kwa mali zenu na nafsi zenu katika Njia ya Allaah. [At-Tawbah: 41]
إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١١١﴾
Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Jannah. Wanapigana katika Njia ya Allaah, wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi ya haki Aliyojiwekea katika Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Na nani atimizae zaidi ahadi yake kuliko Allaah? Basi furahieni kwa biashara yenu mliyofungamana Naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa. [At-Tawbah: 111]
لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ وَالْمُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ فَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ عَلَى الْقَاعِدِينَ دَرَجَةً ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَفَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ عَلَى الْقَاعِدِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٩٥﴾
Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani), isipokuwa wale wenye udhuru, na kati ya wenye kupigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao. Allaah Amewafadhilisha kwa cheo wenye kupigana Jihaad kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaa nyuma. Na wote Allaah Amewaahidi Al-Husnaa (Jannah). Na Allaah Amewafadhilisha wenye kupigana Jihaad kwa ujira mkubwa mno kuliko wanaokaa (nyuma).
دَرَجَاتٍ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةً وَرَحْمَةً ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٩٦﴾
Ni daraja za vyeo (vya juu) kutoka Kwake na Maghfirah na Rahmah. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [An-Nisaa: 95-96]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿١٠﴾
Enyi walioamini! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo?
تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿١١﴾
Mumuamini Allaah na Rasuli Wake, na mfanye Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zenu, na nafsi zenu. Hivyo ndiyo bora kwenu mkiwa mnajua.
يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٢﴾
(Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito na masikani mazuri katika Jannaat za kudumu milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa mno.
وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٣﴾
Na jengine mlipendalo, (nalo ni) nusura kutoka kwa Allaah na ushindi wa karibu. Na wabashirie Waumini. [Asw-Swaff: 10-13]
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سُئِلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : أيُّ العَمل أفْضَلُ ؟ قَالَ : (( إيمَانٌ بِاللهِ وَرَسُولِهِ )) قيلَ : ثُمَّ مَاذَا ؟ قَالَ : (( الجهادُ في سَبيلِ اللهِ )) قِيلَ : ثُمَّ مَاذَا ؟ قَالَ : (( حَجٌّ مَبْرُورٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Aliulizwa: "Ni amali gani bora zaidi?", Akasema: "Kumuamini Allaah na Rasuli Wake." Pakasemwa: "Kisha ni ipi?" Akasema: "Jihadi katika njia ya Allaah." Akaulizwa tena: "Kisha ni ipi?" Akasema: "Hijjah Mabruwr." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن ابن مسعود رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قُلْتُ : يَا رسولَ الله ، أيُّ العَمَلِ أَحَبُّ إِلَى اللهِ تَعَالَى ؟ قَالَ : (( الصَّلاَةُ عَلَى وَقْتِهَا )) قُلْتُ : ثُمَّ أيُّ ؟ قَالَ : (( بِرُّ الوَالِدَيْنِ )) قلتُ : ثُمَّ أيُّ ؟ قَالَ : (( الجِهَادُ في سَبيلِ اللهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni amali gani inampendeza Allaah Ta'aalaa?.", Akasema: "Ni Swalaah kwa wakati wake." Nikasema: "Kisha ni ipi?" Akasema: "Kuwatendea wema wazazi wawili." Nikasema: "Kisha ipi?" Akasema: "Jihadi katika Njia ya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي ذرّ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قُلْتُ : يَا رسول الله ، أيُّ العَمَلِ أفْضلُ ؟ قَالَ : (( الإيمَانُ بِاللهِ ، وَالجِهَادُ في سَبِيلهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni amali gani iliyo bora?" Akasema: "Ni kumuamini Alaah na kupigana Jihadi katika njia ya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أنس رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَغَدْوَةٌ في سَبيلِ اللهِ ، أَوْ رَوْحَةٌ ، خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kutumia wakati wa mchana kwa kwenda safari katika njia ya Allaah au jioni ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي سعيدٍ الخدريِّ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : أَتَى رَجُلٌ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : أيُّ النَّاسِ أفْضَلُ ؟ قَالَ : (( مُؤْمنٌ يُجَاهِدُ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ في سَبيلِ اللهِ )) قَالَ : ثُمَّ مَنْ ؟ قَالَ : (( مُؤْمِنٌ في شِعبٍ مِنَ الشِّعَابِ يَعْبُدُ اللهَ ، وَيَدَعُ النَّاسَ مِنْ شَرِّهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa alikuja mtu na kumuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni mtu gani aliye bora miongoni mwa watu?" Akasema: "Muumini mpigania Jihadi kwa nafsi yake na mali yake katika njia ya Allaah." Akauliza tena: "Kisha nani?" Akajibu: "Muumini anayeishi mtaani katika mitaa anamuabudu Allaah, na anawaacha watu kutokana na shari yake." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 6
وعن سهل بن سعد رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( رِبَاطُ يَوْمٍ فِي سَبِيلِ اللهِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا ، وَمَوْضِعُ سَوْطِ أَحَدِكُمْ مِنَ الجَنَّةِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا ، وَالرَّوْحَةُ يَرُوحُهَا العَبْدُ في سَبِيلِ اللهِ تَعَالَى ، أَوْ الغَدْوَةُ ، خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kufanya Ribaat (Ni jeshi la Kiislamu linaloweka kambi likiwa na silaha zake na zana za kivita, mpakani mwa adui au mahala popote pa hatari) siku moja katika njia ya Allaah ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake, na sehemu ndogo ya ardhi ya mmoja wenu Peponi iliyo sawa na kiboko ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake. Na kwa mja anaye elekea katika Jihadi katika njia ya Allaah Ta'aalaa jioni au asubuhi ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 7
وعن سَلمَانَ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( رِبَاطُ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ خَيْرٌ مِنْ صِيَامِ شَهْرٍ وَقِيَامِهِ ، وَإنْ مَاتَ جَرَى عَلَيْهِ عَمَلُهُ الَّذِي كَانَ يَعْمَلُ ، وَأُجْرِيَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ ، وَأَمِنَ الفَتَّانَ )) رواه مسلم .
Salmaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: "Ribaat siku moja na usiku wake, ni bora kuliko kufunga mwezi na kusimama kwake, Na akifa ndani yake amali yake aliyokuwa akiifanya itaendelea, na riziki yake itaendelea, na atalindwa na fitna ya kaburi." [Muslim]
Hadiyth – 8
وعن فَضَالَةَ بن عُبَيْد رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( كُلُّ مَيِّتٍ يُخْتَمُ عَلَى عَمَلِهِ إِلاَّ المُرَابِطَ فِي سَبيلِ اللهِ ، فَإنَّهُ يُنْمى لَهُ عَمَلهُ إِلَى يَوْمِ القِيَامَةِ ، وَيُؤَمَّنُ فِتْنَةَ القَبْرِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Kutoka kwa Fadhaalah bin 'Ubayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila maiti anahitimishwa amali zake isipokuwa Muraabit katika njia ya Allaah. Hakika amali zake huendelea kukua mpaka Siku ya Qiyaamah na husalimika na fitna ya kaburi." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 9
وعن عثمان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( رِبَاطُ يَوْمٍ في سَبيلِ اللهِ ، خَيْرٌ مِنْ ألْفِ يَوْمٍ فِيمَا سِوَاهُ مِنَ المَنَازِلِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
'Uthamaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalhi wa sallam) akisema: "Kufanya Ribaat siku moja katika njia ya Allaah ni bora kuliko kufanya amali nyingine kwa siku elfu moja." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 10
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( تَضَمَّنَ الله لِمَنْ خَرَجَ في سَبيلِهِ ، لا يُخْرِجُهُ إِلاَّ جِهَادٌ في سَبيلِي ، وَإيمَانٌ بِي ، وَتَصْدِيقٌ بِرُسُلِي ، فَهُوَ عَلَيَّ ضَامِنٌ أنْ أُدْخِلَهُ الجَنَّةَ ، أَوْ أُرْجِعَهُ إِلَى مَنْزِلهِ الَّذِي خَرَجَ مِنْهُ بِمَا نَالَ مِنْ أجْرٍ ، أَوْ غَنيمَةٍ . وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ ، مَا مِنْ كَلْمٍ يُكْلَمُ في سَبيلِ اللهِ ، إِلاَّ جَاءَ يَوْمَ القِيَامَةِ كَهَيْئَتِهِ يَوْمَ كُلِم ؛ لَوْنُهُ لَوْنُ دَمٍ ، وَرِيحُهُ ريحُ مِسْكٍ . وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ ، لَوْلاَ أنْ يَشُقَّ عَلَى المُسْلِمِينَ مَا قَعَدْتُ خِلاَفَ سَرِيَّةٍ تَغْزُو في سَبيلِ اللهِ أبداً ، وَلكِنْ لاَ أجِدُ سَعَةً فأحْمِلُهُمْ وَلاَ يَجِدُونَ سَعَةً ، وَيَشُقُّ عَلَيْهِمْ أنْ يَتَخَلَّفُوا عَنِّي . وَالَّذِي نَفْس مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ ، لَوَدِدْتُ أنْ أغْزُوَ في سَبيلِ اللهِ ، فَأُقْتَلَ ، ثُمَّ أغْزُوَ فَأُقْتَلَ ، ثُمَّ أغْزُوَ فَأُقْتَلَ )) رواه مسلم ، وروى البخاري بعضه .
Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Amemdhamini mwenye kutoka katika njia Yake, hatoki isipokuwa kupigana Jihadi katika njia yangu na kumuamini Allaah na kwa kusadikisha Rasuli Wake. Yeye (yaani Allaah) amemdhaminia ima kumuingiza Peponi (ikiwa atakuwa shahidi) au kumrudisha katika sehemu ile ile aliyotoka nayo kwa kumpatia thawabu au ngawira. Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi Mwake, mtu huyo hatajeruhiwa na jeraha lolote katika njia ya Allaah isipokuwa atakuja Siku ya Qiyaamah katika hali yake aliyokuwa nayo siku aliyojeruhiwa, rangi yake itakuwa ni rangi ya damu na harufu yake ya manukato. Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi Mwake lau sikuchelea uzoto kwa Waislamu nisinge baki nyuma ya jeshi lolote ambalo linatoka kuelekea katika vita katika njia ya Allaah daima. Lakini sipati wasaa wa vipando vya kuwachukua wala wao wenyewe pia hawana ukunjufu huo na wanakuwa na uzito mkubwa kubakisha nyuma (kwa shughuli kama hiyo). Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi Mwake, ningependa sana kupigana Jihadi katika njia ya Allaah na niwe ni mwenye kuuliwa, kisha nipigane tena, na niuliwe, kisha nipigane tena na niwe ni mwenye kuuliwa." [Muslim, na pia Al-Bukhaariy sehemu ya Hadiyth hiyo]
Hadiyth – 11
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ مَكْلُومٍ يُكْلَم في سَبيِلِ الله إِلاَّ جَاءَ يَومَ القِيَامةِ ، وَكَلْمُهُ يدْمِي : اللَّوْنُ لَوْنُ دَمٍ ، وَالرِّيحُ ريحُ مِسكٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna yeyote anayejeruhiwa katika njia ya Allaah ila mtu huyo atakuja Siku ya Qiyaamah hali ya kuwa rangi yake ni rangi ya damu na harufu yake ni harufu ya manukato (misk)." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 12
وعن معاذٍ رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( مَنْ قَاتَلَ في سَبِيلِ الله من رَجُلٍ مُسْلِمٍ فُوَاقَ نَاقَةٍ ، وَجَبَتْ لَهُ الجَنَّةُ ، وَمَنْ جُرِحَ جُرْحاً في سَبِيلِ اللهِ أَوْ نُكِبَ نَكْبَةً فَإنَّهَا تَجِيءُ يَوْمَ القِيَامَةِ كَأَغزَرِ مَا كَانَتْ : لَونُها الزَّعْفَرَانُ ، وَريحُها كَالمِسْكِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Mu'adh (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kupigana Jihadi katika njia ya Allaah miongoni mwa Waislamu kwa muda mfupi kabisa kama wa kumkama ngamia, imekuwa ni wajibu kwake kuingizwa Peponi. Na yeyote anayejeruhiwa katika njia ya Allaah au kukwaruzwa, hakika atakuja Siku ya Qiyaamah kikiwa kibichi kama kilivyokuwa: rangi yake itakuwa ya zafarani na harufu ni ya misk." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 13
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : مَرَّ رَجُلٌ مِنْ أصْحَابِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم بِشِعبٍ فِيهِ عُيَيْنَةٌ مِنْ مَاءٍ عَذْبَة ، فَأعْجَبَتْهُ ، فَقَالَ : لَو اعْتَزَلْتُ النَّاسَ فَأقَمْتُ في هَذَا الشِّعْبِ ، وَلَنْ أفْعَلَ حَتَّى أسْتَأْذِنَ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فذكَرَ ذَلِكَ لرسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( لاَ تَفعلْ؛ فَإنَّ مُقامَ أَحَدِكُمْ في سَبيلِ اللهِ أفْضَلُ مِنْ صَلاَتِهِ في بَيْتِهِ سَبْعِينَ عَاماً، أَلاَ تُحِبُّونَ أنْ يَغْفِرَ الله لَكُمْ ، وَيُدْخِلَكُمُ الجَنَّةَ ؟ أُغْزُوا في سَبيلِ الله ، من قَاتَلَ في سَبِيلِ اللهِ فُوَاقَ نَاقَةٍ وَجَبَتْ لَهُ الجَنَّةُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alipita mtu miongoni mwa Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika bonde lililokuwa na chemchemu ya maji matamu na akapendezwa sana na hilo. Akasema moyoni mwake: "Lau kama ningejitenga na watu na kuishi sehemu hii lakini nitafanya hivyo tu nikipata idhini ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Alimtajia hilo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ambaye alimwambia: "Usifanye hivyo, kwani yeyote miongoni mwenu ambaye atakuwa tayari kupigana katika njia ya Allaah ni bora kwake kuliko kuswali nyumbani kwake kwa miaka sabiini, je, nyinyi hampendi kusamehewa na Allaah na kuwaingiza nyinyi Peponi? Hivyo, poganeni katika njia ya Allaah kwani mwenye kupigana katika njia ya Allaah kwa muda wa kumkama ngamia mara mbili ni wajibu kwake kuingizwa Peponi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan ]
Hadiyth – 14
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قيل : يَا رسولَ اللهِ ، مَا يَعْدلُ الجهادَ في سَبِيلِ اللهِ ؟ قَالَ : (( لاَ تَسْتَطِيعُونَهُ )) فَأعَادُوا عَلَيْهِ مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلاَثاً كُلُّ ذَلِكَ يَقُولُ : (( لاَ تَسْتَطِيعُونَهُ )) ! ثُمَّ قَالَ : (( مَثَلُ المُجَاهِدِ فِي سَبيلِ اللهِ كَمَثلِ الصَّائِمِ القَائِمِ القَانتِ بآياتِ الله لا يَفْتُرُ مِنْ صِيَامٍ ، وَلاَ صَلاَةٍ ، حَتَّى يَرْجِعَ المُجَاهِدُ في سَبِيلِ اللهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ مسلمٍ .
وفي رواية البخاري : أنَّ رَجُلاً قَالَ : يَا رسول الله ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ يَعْدِلُ الجِهَادَ ؟ قَالَ : (( لاَ أجِدُهُ )) ثُمَّ قَالَ : (( هَلْ تَسْتَطِيعُ إِذَا خَرَجَ المُجَاهِدُ أنْ تَدْخُلَ مَسْجِدَكَ فَتقومَ وَلاَ تَفْتُرَ ، وَتَصُومَ وَلاَ تُفْطِرَ )) ؟ فَقَالَ : وَمَنْ يَسْتَطِيعُ ذَلِكَ ؟! .
Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: "Ni amali gani iliyo sawa na Jihaad katika njia ya Allaah?" Akasema: "Hamuna uwezo wa hilo." Wakarudia hilo swali mara mbili au tatu na kila mara anawajibu: "Hamuna uwezo wa hilo." Kisha akasema: "Mfano wa mwenye kupigana Jihaad (Mujaahid) katika njia ya Allaah ni kama mfano wa mwenye kufunga, kuswali na kusoma ayah za Allaah bila kupumzika anaendelea kuswali na kufunga mpaka anaporudi Mujaahid katika njia ya Allaah." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy, na hii ni lafdhi ya Muslim]
Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy inasema kuwa yupo mtu aliyeuliza: "Ee Rasuli! Nionyeshe amali iliyosawa na Jihaad?" Akasema: "Sioni amali iliyo sawa na Jihaad." Kisha akasema: "Je, unaweza pindi anapotoka Mujaahid kuingia katika Msikiti wako ukawa unaswali bila kuchoka na ufunge bila kufungua?" Akasema: "Na ni nani anayeweza kufanya hivyo?"
Hadiyth – 15
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مِنْ خَيْرِ مَعَاشِ النَّاسِ لَهُمْ ، رَجُلٌ مُمْسِكٌ عِنَانَ فَرَسِهِ في سَبِيلِ اللهِ ، يَطِيرُ عَلَى مَتْنِهِ ، كُلَّمَا سَمِعَ هَيْعَةً أَوْ فَزْعَةً طَارَ عَلَيْهِ يَبْتَغِي القَتْلَ وَالمَوْتَ مَظَانَّهُ أَوْ رَجُلٌ في غُنَيْمَةٍ في رَأسِ شَعَفَةٍ مِنْ هَذَا الشَّعَفِ ، أَوْ بَطْنِ وَادٍ مِن الأَوْدِيَةِ ، يُقِيمُ الصَّلاَةَ ، وَيُؤتي الزَّكَاةَ ، وَيَعْبُدُ رَبَّهُ حَتَّى يَأتِيَهُ اليَقِينُ ، لَيْسَ مِنَ النَّاسِ إِلاَّ في خَيْرٍ )) رواه مسلم .
Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Maisha bora kwa watu ni mtu kushika hatamu za farasi wake katika njia ya Allaah anaruka katika matini yake kila anaposikia zogo au fazaiko, anaikimbilia kutaka kumuua adui au kuuliwa yeye, au mtu katka mifugo yake, juu ya mlima au katika jabali ndani ya majabali haya, au ndani ya bonde katika mabonde haya, anasimamisha Swalaah na anatoa Zakaah, anamuabudu Mola wake mpaka yakamfikia mauti hayatangamani na watu ila kwa heri." [Muslim]
Hadiyth – 16
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ في الجنَّةِ مِئَةَ دَرَجَةٍ أعَدَّهَا اللهُ لِلْمُجَاهِدِينَ في سَبِيلِ اللهِ مَا بَيْنَ الدَّرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأرْضِ )) رواه البخاري .
Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika katika Pepo zipo daraja mia moja ambazo Allaah Amewaandalia Mujahidina waliopigana katika njia ya Allaah, baina ya daraja mbili ni kama baina ya mbingu na ardhi." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 17
وعن أَبي سعيد الخدري رضي اللهُ عنه : أنَّ رَسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبّاً ، وَبِالإسْلاَمِ ديناً ، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولاً ، وَجَبَتْ لَهُ الجَنَّةُ )) ، فَعَجِبَ لَهَا أَبُو سَعيدٍ ، فَقَالَ : أَعِدْهَا عَلَيَّ يَا رسولَ اللهِ ، فَأَعَادَهَا عَلَيْهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( وَأُخْرَى يَرْفَعُ اللهُ بِهَا العَبْدَ مِئَةَ دَرَجَةٍ في الجَنَّةِ ، مَا بَيْنَ كُلِّ دَرَجَتَينِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأرْضِ )) قَالَ : وَمَا هيَ يَا رسول الله ؟ قَالَ : (( الجِهَادُ في سَبِيلِ اللهِ ، الجهَادُ في سَبيلِ اللهِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kuridhia kuwa Allaah ni Rabb wake, Uislamu ndiyo Dini yake na Muhammad ni Rasuli basi yeye ni mtu wa Peponi bila shaka yoyote." Abu Sa'iyd aliona ajabu kwa hayo na akamwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) arudie tena hayo. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alirudia tena, kisha akasema: "Na mwingine ni mja ambaye Allaah humnyanyua daraja mia moja Peponi, baina ya kila daraja mbili ni kama baina ya mbingu na ardhi." Akauliza: "Na ni ipi hiyo, ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ni Jihaad katika njia ya Allaah, ni Jihaad katika njia ya Allaah." [Muslim]
Hadiyth – 18
وعن أَبي بكر بن أَبي موسى الأشعريِّ ، قَالَ : سَمِعْتُ أَبي رضي اللهُ عنه ، وَهُوَ بَحَضْرَةِ العَدُوِّ ، يقول : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ أبْوَابَ الجَنَّةِ تَحْتَ ظِلاَلِ السُّيُوفِ )) فَقَامَ رَجُلٌ رَثُّ الهَيْئَةِ ، فَقَالَ : يَا أَبَا مُوسَى أأنْتَ سَمِعْتَ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقول هَذَا ؟ قَالَ : نَعَمْ ، فَرَجَعَ إِلَى أصْحَابِهِ ، فَقَالَ : أقْرَأُ عَلَيْكُم السَّلاَمَ ، ثُمَّ كَسَرَ جَفْنَ سَيْفِهِ فَألْقَاهُ ، ثُمَّ مَشَى بِسَيْفِهِ إِلَى العَدُوِّ فَضَربَ بِهِ حَتَّى قُتِلَ . رواه مسلم .
Abu Bakar bin Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia baba yangu naye akiwa mbele ya adui akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Amesema: "Hakika milango ya Pepo ipo chini ya vivuli vya panga." Hapo alisimama mtu ambaye hakuwa katika hali nzuri na kuuliza: "Ee Abu Muwsaa! Je, wewe ndiyo uliyemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema hayo?" Akasema: "Ndio." Alirudi kwa Swahaaba zake na kuwaambia: "Ninawatoleeni salamu (za mwisho)." Baada ya hapo alivunja ala (uo) ya upanga wake na kuutupa, kisha akatembea na upanga wake kuwaelekea maadui na akapigana nao mpaka akafa shahidi." [Muslim]
Hadiyth – 19
وعن أَبي عبسٍ عبد الرحمان بن جَبْرٍ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ما اغْبَرَّتْ قَدَمَا عَبْدٍ في سَبيلِ اللهِ فَتَمَسَّهُ النَّارُ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abs 'Abdir-Rahmaan bina Jabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna unyayo wa mja uliopata vumbi katika njia ya Allaah kisha ukaingia motoni." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 20
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَلِجُ النَّارَ رَجُلٌ بَكَى مِنْ خَشْيةِ الله حَتَّى يَعُودَ اللَّبَنُ في الضَّرْعِ ، وَلاَ يَجْتَمِعُ عَلَى عَبْدٍ غُبَارٌ في سَبيلِ اللهِ وَدُخَانُ جَهَنَّمَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hataingia Motoni mtu ambaye Amelia kwa kumuogopa Allaah mpaka maziwa yarudi katika matiti yake wala havikusanyiki kwa mja vumbi katika njia ya Allaah na moshi wa jahannam." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 21
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( عَيْنَانِ لاَ تَمسُّهُمَا النَّارُ : عَيْنٌ بَكَتْ مِنْ خَشْيَةِ اللهِ ، وَعَيْنٌ بَاتَتْ تَحْرُسُ في سَبيلِ اللهِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Macho mawili hayatoguswa na moto: Jicho lililolia kwa ajili ya kumuogopa Allaah na jicho lililokesha likilinda katika njia ya Allaah." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 22
وعن زيد بن خالد رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ جَهَّزَ غَازياً في سَبيلِ اللهِ فَقَدْ غَزَا، وَمَنْ خَلَفَ غَازياً في أهْلِهِ بِخَيْرٍ فَقَدْ غَزَا )) متفقٌ عَلَيْهِ.
Zayd bin Khaalid Al-Juhaniy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumtayarisha Mpiganaji katika njia ya Allaah, na yeye amepigana. Na Mwenye kuangalia watu wanaomtegemea mpiganaji na yeye amepigana." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 23
وعن أَبي أُمَامَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أفْضَلُ الصَّدَقَاتِ ظِلُّ فُسْطَاطٍ في سَبِيلِ اللهِ وَمَنيحَةُ خَادِمٍ في سَبِيلِ اللهِ ، أَوْ طَرُوقَةُ فَحلٍ في سَبِيلِ اللهِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swadaqah bora ni kutoa hema kwa ajili ya kuwakinga Mujahidina katika njia ya Allaah na jua na kumpatia mtumishi mtu anayepigana katika njia ya Allaah au kumpa Mujaahid ngamia dume katika njia ya Allaah." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 24
وعن أنس رضي الله عنه : أن فَتَىً مِنْ أسْلَمَ ، قَالَ : يَا رسولَ اللهِ ، إنِّي أُرِيدُ الغَزْوَ وَلَيْسَ مَعِيَ مَا أَتَجهَّزُ بِهِ ، قَالَ : (( ائْتِ فُلاناً فَإنَّهُ قَدْ كَانَ تَجَهَّزَ فَمَرِضَ )) فَأتَاهُ، فَقَالَ : إنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُقْرِئُكَ السَّلاَمَ ، ويقول : أعْطِني الَّذِي تَجَهَّزْتَ بِهِ . قَالَ : يَا فُلاَنَةُ ، أعْطِيهِ الَّذِي كُنْتُ تَجَهَّزْتُ بِهِ ، وَلاَ تَحْبِسِي عَنْهُ شَيْئاً ، فَوَاللهِ لاَ تَحْبِسِي مِنْهُ شَيْئاً فَيُبَارَكَ لَكِ فِيهِ . رواه مسلم .
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Kijana katika kabila la Aslam alikuja na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! Mimi ninataka kushiriki katika vita, lakini sina chochote cha kujitayarisha nacho?" Akasema: 'Nenda kwa fulani kwani yeye alikuwa amejitayarisha lakini akashikwa na maradhi.' Huyu kijana akaenda kwa huyo mtu na kumwambia: 'Kwa hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anakutolea salamu na anakwambia: Nipatie mimi vifaa ulivyovitayarisha ili kuvitumia katika vita.' Akasema (yule mtu): 'Ee mke wangu mpatie nilichojitayarisha nacho usibakishe chochote. Naapa kwa Allaah, ikiwa hutamnyima chochote katika vifaa nilivyotayarisha, Allaah atakubariki katika hivyo." [Muslim]
Hadiyth – 25
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم بَعَثَ إِلَى بَنِي لَحْيَانَ، فَقَالَ : (( لِيَنْبَعِثْ مِنْ كُلِّ رَجُلَيْنِ أحَدُهُمَا ، وَالأجْرُ بَيْنَهُمَا )) رواه مسلم .
وفي روايةٍ لَهُ : (( لِيَخْرُجَ مِنْ كُلِّ رَجُلَيْنِ رَجُلٌ )) ثُمَّ قَالَ للقاعد : (( أيُّكُمْ خَلَفَ الخَارِجَ في أهْلِهِ وَمَالِهِ بِخيْرٍ كَانَ لَهُ مِثْلُ نِصْفِ أجْرِ الخَارِجِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma jeshi kwa Bani Lahyaan, akasema: "Katika kila watu wawili atoke mmoja (Kwenda katika Jihaad) na ujira (thawabu) ni baina yao." [Muslim]
Na katika riwaayah yake nyingine: "Atoke mtu mmoja katika kila watu wawili." Kisha akawaambia waliobaki nyuma: "Yeyote miongoni mwenu atakaye iangalia familia ya aliyetoka (kwenda katika Jihaad) na kumtizamia mali yake vyema zaidi atakuwa na nusu ya thawabu mfano wa yule aliyetoka."
Hadiyth – 26
وعن البَراءِ رضي الله عنه ، قَالَ : أتَى النبيَّ صلى الله عليه وسلم رَجُلٌ مُقَنَّعٌ بالحَدِيدِ ، فَقَالَ : يَا رسولَ اللهِ ، أُقَاتِلُ أَوْ أُسْلِمُ ؟ قَالَ : (( أسْلِمْ ، ثُمَّ قَاتِلْ )) . فَأسْلَمَ ، ثُمَّ قَاتَلَ فَقُتِلَ . فَقَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( عَمِلَ قَلِيلاً وَأُجِرَ كَثِيراً )) متفقٌ عَلَيْهِ. وهذا لفظ البخاري .
Al-Baraa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mtu aliyekuwa na silaha kamili na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! Nipigane kwanza au nisilimu?" Akamjibu: "Silimu kwanza, kisha pigana." Akasilimu, kisha akapigana na kuuliwa. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Amefanya amali kidogo na akapata ujira mwingi." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 27
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَا أَحَدٌ يَدْخُلُ الجَنَّةَ يُحِبُّ أنْ يَرْجِعَ إِلَى الدُّنْيَا وَلَهُ مَا عَلَى الأرْضِ مِنْ شَيْءٍ إِلاَّ الشَّهِيدُ ، يَتَمَنَّى أنْ يَرْجِعَ إِلَى الدُّنْيَا ، فَيُقْتَلَ عَشْرَ مَرَّاتٍ ؛ لِمَا يَرَى مِنَ الكَرَامَةِ )) .
وفي رواية : (( لِمَا يَرَى مِنْ فَضْلِ الشَّهَادَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna yeyote atakaeingia Peponi akatamani kurudi duniani hata kama atapatiwa vyote vilivyomo ndani yake isipokuwa shahidi, yeye hutamani sana arudi ulimwenguni ili auliwe mara kumi (kwa ajili ya Allaah) kwa anavyoona katika karama (na fadhila za kufa shahidi)."
Na katika riwaayah nyingine: "Kwa yale anayoona katika ile fadhila ya kutunukiwa shahada." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 28
وعن عبدِ الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يَغْفِرُ اللهُ لِلْشَّهِيدِ كُلَّ شَيْءٍ إِلاَّ الدَّيْنَ )) . رواه مسلم .
وفي روايةٍ له : (( القَتْلُ في سبيلِ اللهِ يُكَفِّرُ كُلَّ شيءٍ إلاَّ الدَّيْن )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Allaah humsamehe shahidi madhambi yote isipokuwa deni." [Muslim]
Na katika riwaayah yake nyingine: "Anayeuliwa katika njia ya Allaah anafutiwa madhambi yake yote ila deni."
Hadiyth – 29
وعن أَبي قتادة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَامَ فِيهِم فَذَكَرَ أنَّ الجِهَادَ في سَبيلِ اللهِ ، وَالإيمَانَ بِاللهِ ، أفْضَلُ الأعْمَالِ ، فَقَامَ رَجُلٌ ، فَقَالَ : يَا رسولَ اللهِ ، أرأيْتَ إنْ قُتِلْتُ في سَبيلِ اللهِ ، أتُكَفَّرُ عَنِّي خَطَايَايَ ؟ فَقَالَ لهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( نَعَمْ ، إنْ قُتِلْتَ في سَبيلِ الله وَأنْتَ صَابِرٌ مُحْتَسِبٌ ، مُقْبِلٌ غَيْرُ مُدْبِرٍ )) ، ثُمَّ قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( كيْفَ قُلْتَ ؟ )) قَالَ : أرَأيْتَ إنْ قُتِلْتُ في سَبيلِ اللهِ ، أتُكَفَّرُ عَنِّي خَطَايَايَ ؟ فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( نَعَمْ ، وَأنْتَ صَابرٌ مُحْتَسِبٌ ، مُقْبِلٌ غَيرُ مُدْبِرٍ ، إِلاَّ الدَّيْنَ فَإنَّ جِبْريلَ u قَالَ لِي ذَلِكَ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama kuwahutubia watu na akawaeleza wao kwamba Jihaad katika njia ya Allaah na Imaani kwa Allaah ni amali zilizo bora kabisa. Hapo akasimama mtu mmoja na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje nikiuliwa katika njia ya Allaah nitafutiwa madhambi yangu?" Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Ndio, ukiuliwa katika njia ya Allaah huku ukisubiri na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah, ukisonga mbele katika vita bila kukimbia." Kisha akauliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Umesema nini?" Akasema: "Waonaje nilikuwa katika njia ya Allaah nitafutiwa madhambi yangu?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ndio, nawe umesubiri na kutarajia malipo, ukiwa unasonga mbele katika vita bila kukimbia isipokuwa deni kwani Jibriyl ameniambia hilo sasa hivi." [Muslim]
Hadiyth – 30
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَجُلٌ : أيْنَ أنَا يَا رسول الله إنْ قُتِلْتُ ؟ قَالَ : (( في الجَنَّةِ )) فَألْقَى تَمَرَاتٍ كُنَّ فِي يَدِهِ ، ثُمَّ قَاتَلَ حَتَّى قُتِلَ . رواه مسلم .
Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Alisema mtu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya Uhud: 'Unaonaje mimi nikiuliwa nitakuwa wapi?' Akasema: 'Peponi." Yule mtu alitupa tende zilizokuwa mkononi mwake. Baada ya hapo alipigana mpaka akauliwa." [Muslim]
Hadiyth – 31
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : انْطَلَقَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَأصْحَابُهُ حَتَّى سَبَقُوا المُشْرِكِينَ إِلَى بَدْرٍ ، وَجَاءَ المُشْرِكُونَ ، فَقَالَ رَسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَقْدمَنَّ أَحَدٌ مِنْكُمْ إِلَى شَيْءٍ حَتَّى أكُونَ أنَا دُونَهُ )) . فَدَنَا المُشْرِكُونَ ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قُومُوا إِلَى جَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّماوَاتُ وَالأرْضُ )) قَالَ : يَقُولُ عُمَيْرُ بن الحُمَامِ الأنْصَارِيُّ رضي الله عنه : يَا رسولَ اللهِ ، جَنَّةٌ عَرْضُهَا السَّماوَاتُ وَالأرْضُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) قَالَ : بَخٍ بَخٍ ؟ فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا يَحْمِلُكَ عَلَى قَولِكَ بَخٍ بَخٍ ؟ )) قَالَ : لاَ وَاللهِ يَا رَسُولَ اللهِ إِلاَّ رَجَاءَ أَنْ أَكُونَ مِنْ أهْلِهَا ، قَالَ : (( فَإنَّكَ مِنْ أهْلِهَا )) فَأخْرَجَ تَمَرَاتٍ مِنْ قَرَنِهِ ، فَجَعَلَ يَأكُلُ مِنْهُنَّ ، ثُمَّ قَالَ : لَئِنْ أَنَا حَييتُ حَتَّى آكُلَ تَمَرَاتِي هذِهِ إنّهَا لَحَياةٌ طَوِيلَةٌ ، فَرَمَى بِمَا كَانَ مَعَهُ مِنَ التَّمْرِ ، ثُمَّ قَاتَلَهُمْ حَتَّى قُتِلَ . رواه مسلم .
Na amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alitoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Swahaaba zake hadi wakawatangulia washirikina Badr. Washirikina wakaja, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Asitangulie mmoja wenu kwa chochote mpaka mimi niwe wa mwanzo wenu." Washirikina wakakaribia, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Simameni kwenye pepo upana wake ni mbingu na ardhi." 'Umayr bin Al-Humaam Al-Answaariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Pepo upana wake ni mbingu na ardhi?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Bakhin bakhin! (ni neno linalotumika kukuza jambo na kutukuza katika kheri)." Akauliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni kitu gani kimekufanya utamke Bakhin bakhin?", Akasema: "Naapa kwa Allaah, ee Rasuli wa Allaah! ni matarajio niwe katika watu wake." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika wewe ni miongoni mwa watu wake." 'Umayr (Radhwiya Allaahu 'anhu) alitoa tende akawa anazila. Kisha akasema: "Lau mimi nitaishi hadi nimalize kula hizi tende, hayo yatakuwa ni maisha marefu." Akatupa tende alizokuwa nazo, kisha akapigana mpaka akauwawa." [Muslim]
Hadiyth – 31
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ نَاسٌ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم أن ابْعَثْ مَعَنَا رِجَالاً يُعَلِّمُونَا القُرْآنَ وَالسُّنَّةَ ، فَبَعَثَ إلَيْهِمْ سَبْعِينَ رَجُلاً مِنَ الأنْصَارِ يُقَالُ لَهُمْ : القُرّاءُ ، فِيهِم خَالِي حَرَامٌ ، يَقْرَؤُونَ القُرْآنَ ، وَيَتَدَارَسُونَ بِاللَّيْلِ يَتَعَلَّمُونَ ، وَكَانُوا بِالنَّهَارِ يَجِيئُونَ بِالمَاءِ، فَيَضَعُونَهُ في المَسْجِدِ ، وَيَحْتَطِبُونَ فَيَبِيعُونَهُ ، وَيَشْتَرُونَ بِهِ الطَّعَامَ لأَهْلِ الصُّفَّةِ ، وَلِلفُقَرَاءِ ، فَبَعَثَهُمُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، فَعَرَضُوا لَهُمْ فَقَتَلُوهُمْ قَبْلَ أنْ يَبْلغُوا المَكَانَ ، فَقَالُوا : اللَّهُمَّ بَلِّغْ عَنَّا نَبِيَّنَا أنَّا قَدْ لَقِينَاكَ فَرضِينَا عَنْكَ وَرَضِيتَ عَنَّا ، وَأتَى رَجُلٌ حَراماً خَالَ أنَسٍ مِنْ خَلْفِهِ ، فَطَعَنَهُ بِرُمْحٍ حَتَّى أنْفَذَه ، فَقَالَ حَرَامٌ : فُزْتُ وَرَبِّ الكَعْبَةِ ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ إخْوَانَكُمْ قَدْ قُتِلُوا وَإنَّهُمْ قَالُوا : اللَّهُمَّ بَلِّغْ عَنَّا نَبِيَّنَا أنَّا قَدْ لَقِينَاكَ فَرَضِينَا عَنْكَ وَرَضِيتَ عَنَّا )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ مسلم .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Walikuja watu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wakaomba; 'Tuma watu pamoja nasi watusomeshe Qur-aan na Sunnah. Akawatumia watu sabiini, katika Answaar wanaitwa Qurraa' (wasomi) katika wao yumo mjombangu, Haraam. Wanasoma Qur-aan, wanasomesha usiku na kujifunza, Asubuhi walikuwa wanabeba maji wanayaweka Msikitini, na wakitaka kuni na kuziuza. Na wananunulia nazo chakula cha watu wa Suffah na mafukara. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawatuma wakawavamia wakawauwa kabla hawajafika mahali, wakasema: "Ee Mola wetu! Mfikishie Nabiy wetu, kwani sisi tumefika Kwako tumekuridhia Nawe Umeturidhia. Alikuja mtu nyuma ya Haraam, mjombake Anas akamdunga mkuki hadi ukaingia. Akasema: "Nimefuzu, naapa kwa Mola wa Ka'abah." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika ndugu zenu wameuwawa, nao wamesema: 'Ee Mola wetu! Mfikishie Nabiy wetu, kuwa sisi tumekutana nawe tumekuridhia Nawe Umeturidhia." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Muslim]
Hadiyth – 32
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : غَابَ عَمِّي أنسُ بنُ النَّضْرِ رضي الله عنه عن قِتَالِ بَدْرٍ ، فَقَالَ : يَا رسولَ اللهِ ، غِبْتُ عَنْ أوَّلِ قِتَالٍ قَاتَلْتَ المُشْرِكِينَ ، لَئِنِ اللهُ أشْهَدَنِي قِتَالَ المُشْرِكِينَ لَيَرَيَنَّ اللهُ مَا أصْنَعُ . فَلَمَّا كَانَ يَومُ أُحُدٍ انْكَشَفَ المُسْلِمُونَ فَقَالَ : اللَّهُمَّ إنِّي اعْتَذِرُ إلَيْكَ مِمَّا صَنَعَ هؤُلاءُ - يعني : أصْحَابَهُ - وَأبْرَأُ إلَيْكَ مِمَّا صَنَعَ هؤُلاءِ - يَعنِي : المُشْرِكِينَ - ثُمَّ تَقَدَّمَ فَاسْتَقْبَلَهُ سَعْدُ بنُ مُعَاذٍ فَقَالَ : يَا سَعَدَ بنَ مُعَاذٍ ، الجَنَّةَ وَرَبِّ النَّضْرِ ، إنِّي أجِدُ ريحَهَا مِنْ دُونِ أُحُدٍ ! فَقَالَ سَعْدٌ : فَمَا اسْتَطَعْتُ يَا رسولَ اللهِ مَا صَنَعَ ! قَالَ أنسٌ : فَوَجدْنَا بِهِ بِضعاً وَثَمَانِينَ ضَربَةً بِالسَّيْفِ ، أَوْ طَعْنَةً برُمح أَوْ رَمْيةً بِسَهْمٍ ، وَوَجَدْنَاهُ قَدْ قُتِلَ وَمَثَّلَ بِهِ المُشْرِكُونَ ، فَمَا عَرَفَهُ أحَدٌ إِلاَّ أُخْتُهُ بِبَنَانِهِ . قَالَ أنسٌ : كُنَّا نَرَى - أَوْ نَظُنُّ - أنَّ هذِهِ الآية نَزَلتْ فِيهِ وَفي أشْبَاهِهِ : [ مِنَ المُؤمِنينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ ] [ الأحزاب : 23 ] إِلَى آخرها . متفقٌ عَلَيْهِ
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Ami yangu, Anas bin An-Nadhr (Radhwiya Allaahu 'anhu) hakuwepo Vita vya Badr. Akasema: 'Ee Rasuli wa Allaah! Sikuwepo vita vya kwanza vya washirikina. Ila Allaah akinipa fursa ya kupigana na washirikina Nitamuonyesha nitakayofanya.' Ilipofika Siku ya Uhud, Waislamu walielemewa. Anas Akasema: 'Ee Mola wangu! Ninakuomba udhuru kwa waliyoyafanya hawa - Yaani masahibu zake - na ninajitenga Kwako kwa waliyoyafanya hawa - Yaani washirikina.' Kisha akasogea mbele akakutana na Sa'ad bin Mu'aadh (Radhwiya Allaahu 'anhu) akamwambia: 'Ee Sa'ad bin Mu'aadh! Naapa kwa Mola wa an-Nadhr nasikia harufu ya Pepo kutoka Uhud.' Sa'ad akasema: 'Ee Rasuli wa Allaah! Sikuweza (Ushujaa) aliofanya.' Akasema Anas: 'Tukampata yeye akiwa na majeraha zaidi ya themanini yaliyosababishwa na pigo la panga, mikuki na mishale. Tukampata ameuwawa, na washirikina wamemkatakata, hakuweza kutambuliwa na yeyote isipokuwa dadake kwa ncha za vidole vyake.' Akasema Anas: 'Tulikuwa tukiona au tukidhani kwamba ayah hii iliteremka kwa ajili yake na watu mfano wake.' Allaah Anasema: 'Miongoni mwa Waumini, wapo wanaume waliotimiza kikweli waliyoahidiana na Allaah. Basi miongoni mwao wako waliotimiza nadhiri yao (wamekufa Shuhadaa), na miongoni mwao wako wanaongojea na hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo." [Al-Ahzaab: 23] [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 33
وعن سَمُرَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( رَأيْتُ اللَّيْلَةَ رَجُلَيْنِ أتيَانِي ، فَصَعِدَا بِي الشَّجرةَ فَأدْخَلاَنِي دَاراً هِيَ أحْسَنُ وَأَفضَلُ ، لَمْ أَرَ قَطُّ أحْسَنَ مِنْهَا ، قالا : أمَّا هذِهِ الدَّارُ فَدَارُ الشُّهَدَاءِ )) . رواه البخاري ، وَهُوَ بعض من حديث طويل فِيهِ أنواع من العلم سيأتي في باب تحريم الكذب إنْ شاء الله تَعَالَى .
Imepokewa kutoka kwake Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jana usiku niliwaona watu wawili waliokuja kwangu (katika ndoto). Walinichukua na wakaanza kupanda nami kwenye mti na wakaniingiza katika nyumba ambayo ni nzuri na bora sana, sijaona kabisa mfano wake kwa uzuri." Wale watu wawili waliniambia: "Ama nyumba hii ni ya mashahidi." [Al-Bukhaariy]. Hii ni sehemu ya Hadiyth ndefu inayoelezea aina za elimu ambayo itakuja katika mlango wa kuharamisha uongo, In shaa Allaah.
Hadiyth – 34
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ أمَّ الرُّبيعِ بنتَ البَرَاءِ وهي أُمُّ حَارِثة بن سُرَاقَةَ ، أتَتِ النبي صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَتْ : يَا رسولَ اللهِ ، ألاَ تُحَدِّثُنِي عَنْ حَارِثَةَ - وَكَانَ قُتِلَ يَوْمَ بَدْرٍ - فَإنْ كَانَ في الجَنَّةِ صَبَرْتُ ، وَإنْ كَانَ غَيْرَ ذَلِكَ اجْتَهَدْتُ عَلَيْهِ في البُكَاءِ ، فَقَالَ : (( يَا أُمَّ حَارِثَةَ إنَّهَا جِنَانٌ في الجَنَّةِ ، وَإنَّ ابْنَكِ أصابَ الفِرْدَوْسَ الأَعْلَى )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) anahadithia ya kuwa Ummur Rubayyi' bintil Baraa', naye alikuwa ni mama wa Haarithah bin Suraaqah alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, hunielezi mimi kuhusu Haarithah, ambaye aliuliwa katika Vita vya Badr?, Ikiwa atakuwa yupo Peponi basi nitasubiri na ikiwa ni kinyume cha hivyo basi nitalia sana." Akasema: "Ee Umm Haarithah! Hakika zipo Pepo nyingi huko Peponi, na hakika mtoto wako amepita Firdaws ya juu kabisa." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 35
وعن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما ، قَالَ : جِيءَ بِأَبِي إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَدْ مُثِّلَ بِهِ ، فَوُضِعَ بَيْنَ يَدَيْهِ ؛ فَذَهَبْتُ أكْشِفُ عَنْ وَجْهِهِ فَنَهَانِي قَوْمِي ، فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَا زَالتِ المَلائِكَةُ تُظِلُّهُ بِأَجْنِحَتِهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema Jaabir bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Mwili wa babangu ulio katwa katwa uliletwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Nilikuwa naenda kuufunua uso wake lakini baadhi ya watu walinikataza. Hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Malaaikah bado wanaendelea kumfunika na mbawa zao." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 36
وعن سهل بن حنيف رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( مَنْ سَألَ اللهَ تَعَالَى الشَّهَادَةَ بِصِدْقٍ بَلَّغَهُ اللهُ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ ، وَإنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Hunayf (Radhwiya Allaahu 'anhu), (naye alishuhudia Badr) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Yeyote atakayemuomba Allaah Ta'aalaa kufa shahidi kwa ukweli (na ikhlasi), Allaah humuekea cheo cha mashahidi hata akifa kitandani mwake." [Muslim]
Hadiyth – 37
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ طَلَبَ الشَّهَادَةَ صَادِقاً أُعْطِيَهَا ولو لَمْ تُصِبْهُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuomba kufa shahidi kwa kweli atapatiwa thawabu zake japokuwa hatopatikana (kwa kuumizwa na kufa katika vita)." [Muslim]
Hadiyth – 38
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا يَجِدُ الشَّهِيدُ مِنْ مَسِّ القَتْلِ إِلاَّ كَمَا يَجِدُ أَحَدُكُمْ مِنْ مَسِّ القَرْصَةِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Shahidi huwa hahisi chochote katika uchungu anapouliwa isipokuwa kama anavyohisi mmoja wenu pindi anapoumwa." [At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 39
وعن عبد الله بن أَبي أوْفَى رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم في بَعْضِ أيَّامِهِ الَّتي لَقِيَ فِيهَا العَدُوَّ انْتَظَرَ حَتَّى مَالَتِ الشَّمْسُ ، ثُمَّ قَامَ في النَّاسِ فَقَالَ : (( أَيُّهَا النَّاسُ ، لا تَتَمَنَّوا لِقَاءَ العَدُوِّ، وَاسْأَلُوا اللهَ العَافِيَةَ، فَإذَا لَقِيتُموهُمْ فَاصْبِروا ؛ وَاعْلَمُوا أنَّ الجَنَّةَ تَحْتَ ظِلاَلِ السُّيُوفِ )) ثُمَّ قَالَ : (( اللَّهُمَّ مُنْزِلَ الكِتَابِ ، وَمُجْرِيَ السَّحَابِ ، وَهَازِمَ الأحْزَابِ ، أهْزِمْهُمْ وَانْصُرْنَا عَلَيْهِمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Abu Awfaa (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika baadhi ya masiku yake aliyokutana na adui alisubiri mpaka jua likashuka, kisha alisimama kati ya watu na kuwaambia: "Enyi watu! Musitamani kukutana na adui, na muombeni Allaah 'aafiyah, na kama mtakutana naye vumilieni, na eleweni kuwa Pepo iko chini ya vivuli vya panga." Kisha akasema: "Ee Mola Wangu! Mteremsha Kitabu na Mpeleka mawingu, na Mshinda makundi, Washinde na utunusuru juu yao." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 40
وعن سهل بن سعد رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ثِنْتَانِ لاَ تُرَدَّانِ، أَوْ قَلَّمَا تُرَدَّانِ: الدُّعَاءُ عِنْدَ النِّدَاءِ وَعِنْدَ البَأسِ حِيْنَ يُلْحِمُ بَعْضُهُم بَعضَاً )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Sahl bin Sa'ad (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mbili hazirudishwi au nadra kurudishwa: Duaa wakati wa adhaan na wakati wa vita pindi vinapokuwa vikali sana." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 41
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا غَزَا ، قَالَ : (( اللَّهُمَّ أنْتَ عَضْديِ وَنَصِيرِي ، بِكَ أَحُولُ ، وَبِكَ أَصُولُ ، وَبِكَ أُقَاتِلُ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa anapokwenda katika vita akomba: "Allaahumma Anta 'adhuddiy wa naswiyriy Bika ahuulu wa Bika Aswuulu wa Bika Uqaatil - Ee Mola Wangu! Wewe ndiye mwenye kunisaidia na kuninusuru. Kwako tu ndiyo narejea, na kutoka Kwako ndiyo napata nguvu na kwa usaidizi Wako ndiyo napigana." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 42
وعن أَبي موسى رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا خَافَ قَوماً ، قَالَ : (( اللَّهُمَّ إنَّا نَجْعَلُكَ في نُحُورِهِمْ ، وَنَعُوذُ بِكَ مِنْ شُرُورِهمْ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiogopa watu alikuwa anasema: "Allaahumma Innaa Naj'aluka Fiy Nuhuurihim wa Na'uwdhu Bika min Shururihim - Ee Mola Wangu wa haki hakika sisi tunakuweka shingoni mwao na tunataka hifadhi Kwako na hsari zao." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]
Hadiyth – 43
وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( الخَيْلُ مَعقُودٌ في نَوَاصِيهَا الخَيْرُ إِلَى يَومِ القِيَامَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Farasi waliofungwa kwenye tosi zao ni kheri mpaka Siku ya Qiyaamah." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 44
وعن عروة البارِقِيِّ رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : ((الخَيْلُ مَعقُودٌ في نَوَاصِيهَا الخَيْرُ إِلَى يَومِ القِيَامَةِ : الأجْرُ ، وَالمَغْنَمُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
'Urwah Al-Baariqiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Farasi waliofungwa kwenye tosi zao ni kheri mpaka Siku ya Qiyaamah, ni thawabu na ngawira." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 45
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ احْتَبَسَ فَرَساً فِي سَبِيلِ اللهِ ، إيمَانَاً بِاللهِ ، وَتَصْدِيقَاً بِوَعْدِهِ ، فَإنَّ شِبَعَهُ ، وَرَيَّهُ ورَوْثَهُ ، وَبَوْلَهُ في مِيزَانِهِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه البخاري .
Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufunga farasi katika njia ya Allaah kwa kumuamini Allaah na kusadikisha ahadi yake, Hakika shibe yake, kukata kwake kiu yake, kinyesi chake, mkojo wake, ni katika mizani yake Siku ya Qiyaamah." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 46
وعن أَبي مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبيِّ صلى الله عليه وسلم بِنَاقةٍ مَخْطُومَةٍ فَقَالَ : هذِهِ في سَبيلِ اللهِ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لَكَ بِهَا يَوْمَ القِيَامَةِ سَبْعُمئَةِ نَاقَةٍ كُلُّهَا مَخْطُومَةٌ )) رواه مسلم .
Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na ngamia jike aliyefungwa hatamu, akasema: "Huyu namtoa kwa ajili ya Allaah katika njia Yake." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Utapata kwa ajili yake ngamia wa kike mia saba wote wamefungwa Siku ya Qiyaamah." [Muslim]
Hadiyth – 47
وعن أَبي حمادٍ - ويقال : أَبُو سعاد ، ويقال : أَبُو أسدٍ ، ويقال : أَبُو عامِر ، ويقال : أَبُو عمرو ، ويقال : أَبُو الأسود ، ويقال : أَبُو عبسٍ - عُقبة بن عامِر الجُهَنيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ ، يقول : (( [ وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ ] ، أَلاَ إنَّ القُوَّةَ الرَّميُ ، ألاَ إنَّ القُوَّةَ الرَّمْيُ ، ألاَ إنَّ القُوَّةَ الرَّمْيُ )) رواه مسلم .
Amesema Abu Hamaad - na panasemwa Abu Su'aad, panasemwa Abu Asad, panasemwa Abu 'Aamir, panasemwa Abu 'Amruw, panasemwa Abul Aswad, na panasemwa Abu 'Abs - 'Uqbah bin 'Aamir Al-Juhaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa juu ya minbar akisema: "Na waandalieni nguvu zozote mziwezazo " [Al-Anfaal: 60] Fahamu hakika maana ya nguvu ni kurusha mishale, fahamu hakika ni kuwa nguvu ni kurusha mishale, fahamu hakika kuwa nguvu ni kurusha mishale." [Muslim]
Hadiyth – 48
وعن أَبي حمادٍ - ويقال : أَبُو سعاد ، ويقال : أَبُو أسدٍ ، ويقال : أَبُو عامِر ، ويقال : أَبُو عمرو ، ويقال : أَبُو الأسود ، ويقال : أَبُو عبسٍ - عُقبة بن عامِر الجُهَنيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( سَتُفْتَحُ عَلَيْكُمْ أَرْضُونَ ، وَيَكْفِيكُمُ اللهُ ، فَلاَ يَعْجِز أَحَدُكُمْ أنْ يَلْهُوَ بِأَسْهُمِهِ )) رواه مسلم .
Amesema Abu Hamaad - na panasemwa Abu Su'aad, panasemwa Abu Asad, panasemwa Abu 'Aamir, panasemwa Abu 'Amruw, panasemwa Abul Aswad, na panasemwa Abu 'Abs - 'Uqbah bin 'Aamir Al-Juhaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Itafunguliwa juu yenu ardhi, na Allaah atakusaidieni, basi mmoja wenu asifanye ajizi kucheza na mishale yake." [Muslim]
Hadiyth – 49
وعن أَبي حمادٍ - ويقال : أَبُو سعاد ، ويقال : أَبُو أسدٍ ، ويقال : أَبُو عامِر ، ويقال : أَبُو عمرو ، ويقال : أَبُو الأسود ، ويقال : أَبُو عبسٍ - عُقبة بن عامِر الجُهَنيِّ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ عُلِّمَ الرَّمْيَ ، ثُمَّ تَرَكَهُ ، فَلَيْسَ مِنَّا ، أَوْ فَقَدْ عَصَى )) رواه مسلم .
Amesema Abu Hamaad - na panasemwa Abu Su'aad, panasemwa Abu Asad, panasemwa Abu 'Aamir, panasemwa Abu 'Amruw, panasemwa Abul Aswad, na panasemwa Abu 'Abs - 'Uqbah bin 'Aamir Al-Juhaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu): kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayefunzwa kulenga shabaha (kwa kutumia mshale), kisha akaacha, si katika sisi au tayari ameasi." [Muslim]
Hadiyth – 50
ووعن أَبي حمادٍ - ويقال : أَبُو سعاد ، ويقال : أَبُو أسدٍ ، ويقال : أَبُو عامِر ، ويقال : أَبُو عمرو ، ويقال : أَبُو الأسود ، ويقال : أَبُو عبسٍ - عُقبة بن عامِر الجُهَنيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ اللهَ يُدْخِلُ بِالسَّهْمِ الوَاحِدِ ثَلاَثَةَ نَفَرٍ الجَنَّةَ : صَانِعَهُ يَحْتَسِبُ في صَنْعَتِهِ الخَيْرَ ، وَالرَّامِي بِهِ ، ومُنْبِلَهُ .وَارْمُوا وَارْكَبُوا ، وَأنْ تَرْمُوا أحَبُّ إليَّ مِنْ أنْ تَرْكَبُوا . وَمَنْ تَرَكَ الرَّمْيَ بَعْدَ مَا عُلِّمَهُ رَغْبَةً عَنْهُ فَإنَّهَا نِعْمَةٌ تَرَكَهَا )) أَوْ قَالَ : (( كَفَرَهَا )) رواه أَبُو داود .
Amesema Abu Hamaad - na panasemwa Abu Su'aad, panasemwa Abu Asad, panasemwa Abu 'Aamir, panasemwa Abu 'Amruw, panasemwa Abul Aswad, na panasemwa Abu 'Abs - 'Uqbah bin 'Aamir Al-Juhaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika Allaah atawaingiza Peponi watu watatu kwa mshale mmoja: mwenye kuutengeneza anatarajia kheri katika utengenezaji wake, na mwenye kuurusha, na mwenye kupigania Jihaad. Na rusheni - mishale - na pandeni, (farasi, n.k). Kurusha kunapendeza zaidi kwangu kuliko kupanda. Na mwenye kurusha baada ya kufundishwa kwa kuichukia, Hakika hiyo ni neema ameiacha, au alisema: "ameikataa". [Abu Daawuwd]
Hadiyth – 51
وعن سَلَمة بن الأكَوعِ رضي الله عنه ، قَالَ : مَرَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَى نَفَرٍ يَنْتَضِلُونَ ، فَقَالَ : (( ارْمُوا بَنِي إسمعِيلَ فَإنَّ أَبَاكُمْ كَانَ رَامِياً )) رواه البخاري .
Amesema Salamah bin Akwa' : Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alipita kwenye kikundi cha watu wanashindana kurusha mishale, Akawaambia: "Enyi watoto wa Isma'iyl! Rusheni mishale kwani baba yenu alikuwa mrushaji." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 52
وعن عمرو بن عبسة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ رَمَى بِسَهمٍ في سَبيلِ الله فَهُوَ لَهُ عِدْلُ مُحَرَّرَةٍ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Amesema 'Amruw bin 'Abasah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kurusha mshale katika njia ya Allaah (Jihaad), hilo kwake litakuwa sawa na kuacha mtumwa huru." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 53
وعن أَبي يحيى خُرَيْم بن فاتِكٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أنْفَقَ نَفَقَةً في سَبيلِ اللهِ كُتِبَ لَهُ سَبْعُمِئَةِ ضِعْفٍ )) رواه الترمذي ، وقال :
(( حديث حسن )) .
Abu Yahya Khuraym bin Faatik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutoa katika njia ya Allaah ataandikiwa thawabu mara mia saba." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 54
وعن أَبي سعيد رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ عَبْدٍ يَصُومُ يَوْماً فِي سَبيلِ اللهِ إِلاَّ بَاعَدَ اللهُ بِذلِكَ اليَوْمِ وَجهَهُ عَنِ النَّارِ سَبْعِينَ خَرْيفاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna mja yeyote anafunga siku moja katika njia ya Allaah isipokuwa Allaah atauweka mbali uso wake na moto kwa hiyo siku aliyofunga, umbali wa safari ya miaka sabini." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 55
وعن أَبي أُمَامَة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ صَامَ يَوْماً في سَبيلِ اللهِ جَعَلَ اللهُ بَيْنَهُ وَبَيْنَ النَّارِ خَنْدَقاً كما بَيْنَ السَّمَاءِ والأَرْضِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Abu Umaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufunga siku moja katika njia ya Allaah, Allaah ataweka handaki baina yake na moto kama baina ya mbingu na ardhi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 56
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ مَاتَ وَلَمْ يَغْزُ ، وَلَمْ يُحَدِّثْ نَفْسَهُ بالغَزْوِ ، مَاتَ عَلَى شُعْبَةٍ مِنَ النِّفَاقِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufa bila ya kupigana vita na bila kuiambia nafsi yake kuhusu vita basi mtu huyo amekufa juu ya fungu la unafiki." [Muslim]
Hadiyth – 57
وعن جابر رضي الله عنه، قَالَ: كنا مَعَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم، في غَزاةٍ فقالَ: (( إنَّ بِالمَدِينَةِ لَرِجَالاً مَا سِرْتُمْ مَسِيراً ، وَلاَ قَطَعْتُمْ وَادِياً إِلاَّ كَانُوا مَعَكُمْ، حَبَسَهُمُ المَرَضُ )) .
وفي رواية : (( حَبَسَهُمُ العُذْرُ )) .
وفي رواية : (( إِلاَّ شَرَكُوكُمْ في الأجْرِ )) رواه البخاري من رواية أنس ، ورواه مسلم من رواية جابر واللفظ لَهُ .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Tulikuwa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita, naye akasema: 'Hakika Madiynah kuna watu ambao wapo na nyinyi japokuwa hawakufunga safari wala hawakuvuka mabonde, lakini ni maradhi tu ndio yamewazuia."
Na katika riwaayah nyingine: "Wamezuiliwa na udhuru (wa kisheria, hivyo hawakuweza kushiriki)."
Na katika riwaayah nyingine: "Isipokuwa wanashirikiana nanyi katika thawabu." [Al-Bukhaariy amenukuu kutoka kwa Anas, na Muslim kutoka kwa Jaabir na tamshi ni la kwake].
Hadiyth – 58
وعن أَبي موسى رضي الله عنه: أنَّ أعرابياً أتى النبيَّ صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: يَا رسولَ اللهِ، الرَّجُلُ يُقَاتِلُ لِلْمَغْنَمِ ، وَالرَّجُلُ يُقَاتِلُ لِيُذْكَرَ ، وَالرَّجُلُ يُقَاتِلُ ليُرَى مَكَانُهُ ؟
وفي رواية : يُقَاتِلُ شَجَاعَةً ، وَيُقَاتِلُ حَمِيَّةً .
وفي رواية : يُقَاتِلُ غَضَباً ، فَمَنْ في سبيل الله ؟ فقالَ رسولُ اللهِ : (( مَنْ قَاتَلَ لِتَكُونَ كَلِمَةُ اللهِ هِيَ العُلْيَا ، فَهُوَ في سَبيلِ اللهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Aliulizwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Bedui: "Ee Rasuli wa Allaah! Mtu anapigana kwa ajili ya ngawira, na mtu anapigana ili atajwe na mtu anayepigana kwa ajili ya sehemu yake."
Na katika riwaayah nyingine: "Anapigana ili aonekane kuwa yeye ni shujaa na anapigana kwa ghera."
Na katika riwaayah nyingine: "Na anapigana kwa ghadhabu, ni yupi katika hawa yupo katika njia ya Allaah?" Akasema Rasuli wa Allaah: "Yule anayepigana ili neno la Allaah Liwe la juu basi huyo yuko katika njia ya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 59
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ غَازِيَةٍ ، أَوْ سَرِيّةٍ تَغْزُو ، فَتَغْنَمُ وَتَسْلَمُ ، إِلاَّ كَانُوا قَدْ تَعَجَّلُوا ثُلُثَيْ أُجُورهُمْ ، وَمَا مِنْ غَازِيَةٍ أَوْ سَرِيّةٍ تُخْفِقُ وَتُصَابُ إِلاَّ تَمَّ لَهُمْ أجُورهُمْ )) رواه مسلم .
'Abdillaah bin 'Amru bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Hakuna jeshi au kikosi kinachopigana (kwa ajili ya Allaah) ambacho kitakusanya ngawira na kuisalimisha kama ilivyo na katika hali nzuri isipokuwa wanapewa thuluthi mbili ya ujira wao, hapo hapo. Hivyo hivyo, hakuna jeshi au kikosi ambacho hakitapata ngawira na kushindwa isipokuwa ujira wao umekamilika (na watawekewa mpaka Siku ya Qiyaamah)." [Muslim]
Hadiyth – 60
وعن أَبي أُمَامَة رضي الله عنه : أنَّ رجلاً ، قَالَ : يَا رسولَ اللهِ ، ائْذَنْ لي في السِّيَاحَةِ فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ سِيَاحَةَ أُمَّتِي الجِهَادُ في سَبيلِ اللهِ عزوجل )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيدٍ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mtu mmoja alitaka ruhusa kwa kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! Nipatie idhini kutembea katika ardhi (yaani kuacha nchi yake na kwenda katika sehemu nyengine za ardhi hii)." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Hakika matembezi ya Ummah wangu ni Jihaad katika njia ya Allaah." [Abu Daawuwd kwa Isnaad nzuri]
Hadiyth – 61
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( قَفْلَةٌ كَغَزْوَةٍ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيدٍ .
Imepokewa kutoka kwa Abdillaah bin Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika matembezi ya Ummah wangu ni Jihaad katika njia ya Allaah." [Abu Daawuwd kwa Isnaad nzuri]
Hadiyth – 62
وعن السائب بن يزيد رضي الله عنه ، قَالَ : لَمَّا قَدِمَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم مِنْ غَزْوَةِ تَبُوك تَلَقَّاهُ النَّاسُ ، فَتَلَقّيتُهُ مَعَ الصِّبْيَانِ عَلَى ثَنيَّةِ الوَدَاعِ . رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيح بهذا اللفظ .
ورواه البخاري قَالَ: ذَهَبنا نَتَلَقَّى رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم، مَعَ الصِّبْيَانِ إِلَى ثَنِيَّةِ الوَدَاعِ.
As-Sai'ib bin Yaziyd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Aliporudi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka katika Vita vya Taabuk, watu walitoka Madiynah kuja kukutana naye. Hivyo, nami nilikwenda pamoja na watoto na kukutana naye katika Thaniyyatil Wadaa' (sehemu iliyo karibu na Madiynah ambako anapokewa msafiri na kuagwa hapo) . [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh kwa lafdhi hii]
Na imepokewa na Al-Bukhaariy ambaye amesema: "Tulikuwa pamoja na watoto wengine kumpokea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Thaniyyatil Wadaa'.
Hadiyth – 63
وعن أَبي أُمَامَة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ لَمْ يَغْزُ ، أَوْ يُجَهِّزْ غَازِياً ، أَوْ يَخْلُفْ غَازياً في أهْلِهِ بِخَيرٍ ، أصَابَهُ اللهُ بِقَارعَةٍ قَبْلَ يَوْمِ القِيَامَةِ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote asiyepigana au akamtayarishia mwenye kupigana au akawatazama vyema familia ya mpiganaji basi Allaah atamuadhibu vikali kabla ya Siku ya Qiyaamah." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]
Hadiyth – 64
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( جَاهِدُوا المُشْرِكِينَ بِأَمْوَالِكُمْ وَأنْفُسِكُمْ وَألْسِنَتِكُمْ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Piganeni Jihaad na washirikina kwa kutumia mali yenu na nafsi zenu na ndimi zenu." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 65
وعن أَبي عمرو - ويقالُ : أَبُو حكيمٍ - النُّعْمَانِ بن مُقَرِّن رضي الله عنه قَالَ : شَهِدْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، إِذَا لَمْ يُقَاتِلْ من أوَّلِ النَّهَارِ أخَّرَ القِتَالَ حَتَّى تَزُولَ الشَّمْسُ، وَتَهُبَّ الرِّيَاحُ، وَيَنْزِلَ النَّصْرُ . رواه أَبُو داود والترمذي، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Amesema Abu 'Amruw, na inasemekana ni Abu Hakiym An-Nu'maan bin Muqarrin (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemshuhudia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alikuwa asipopigana mwanzo wa mchana basi huchelewesha mapambano mpaka linapozama jua na upepo kuanza na huvyo nusura kuteremka." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 66
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَتَمَنَّوْا لِقَاءَ العَدُوِّ ، وَاسْأَلُوا اللهَ العَافِيَةَ ، فَإذَا لَقِيتُمُوهُمْ فَاصْبِرُوا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musitamani kukutana na adui, na kama mtakutana naye vumilieni." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 67
وعن أَبي هريرة وعن جابرٍ رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الحَرْبُ خَدْعَةٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah na Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhumaa] kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Vita ni hadaa." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]