02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kubainisha Kikundi cha Mashahidi katika Thawabu za Kesho Akhera, Ambao Wanaoshwa na Kuswaliwa Tofauti na Wale Wanaofariki katika Vita Wakipambana na Makafiri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب بيان جماعة من الشهداء في ثواب الآخرة

يغسلون ويصلى عليهم بخلاف القتيل في حرب الكفار

02-Mlango Wa Kubainisha Kikundi cha Mashahidi katika Thawabu za Kesho Akhera, Ambao Wanaoshwa na Kuswaliwa Tofauti na Wale Wanaofariki katika Vita Wakipambana na Makafiri

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( الشُّهَدَاءُ خَمْسَةٌ : المَطْعُونُ وَالمَبْطُونُ، وَالغَرِيقُ، وَصَاحِبُ الهَدْمِ، وَالشَّهِيدُ في سَبِيلِ اللهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mashahidi ni aina tano: Anayekufa kwa tauni, na anaefariki kwa maradhi ya tumbo, na anayeghariki (kufa maji), na anayeaga dunia kwa kuangukiwa na ukuta na shahidi katika njia ya Allaah (Jihaadi) [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا تَعُدُّونَ الشُّهَدَاءَ فِيكُمْ ؟ )) قالوا : يَا رسولَ اللهِ ، مَنْ قُتِلَ في سَبيلِ اللهِ فَهُوَ شَهِيدٌ . قَالَ : (( إنَّ شهَدَاءَ أُمَّتِي إِذَاً لَقَليلٌ )) ! قالوا: فَمَنْ هُمْ يَا رسول الله ؟ قَالَ : (( مَنْ قُتِلَ في سَبيلِ الله فَهُوَ شَهِيدٌ ، وَمَنْ مَاتَ في سَبيلِ الله فَهُوَ شَهِيدٌ ، وَمَنْ مَاتَ في الطَّاعُونِ فَهُوَ شَهِيدٌ ، وَمَنْ مَاتَ في البَطْنِ فَهُوَ شَهِيدٌ ، وَالغَرِيقُ شَهِيدٌ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliuliza: "Ni nani munamfikiria kuwa ni shahidi miongoni mwenu?" Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Anayeuliwa katika njia ya Allaah ndiye shahidi." Akasema: "Hivyo, hakika mashahidi katika Ummah wangu watakuwa kidogo." Wakasema: "Basi ni kina nani hao, ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Yeyote anayeuliwa katika njia ya Allaah ni shahidi, na anayekufa katika njia ya Allaah pia ni shahidi, na anayekufa kwa sababu ya tauni ni shahidi, na anayekufa kwa sababu ya maradhi ya tumbo pia ni shahidi na anayeghariki ni shahidi." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ قُتِلَ دُونَ مَالِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuuliwa kwa ajili ya kuilinda mali yake ni shahidi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي الأعْوَر سعيد بن زيد بن عَمْرو بن نُفَيْل ، أحَدِ العَشَرَةِ المَشْهُودِ لَهُمْ بِالجَنَّةِ عنهم ، قَالَ: سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: (( مَنْ قُتِلَ دُونَ مَالِهِ فَهُوَ شَهيدٌ ، وَمَنْ قُتِلَ دُونَ دَمِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ ، وَمَنْ قتِلَ دُونَ دِينهِ فَهُوَ شَهِيدٌ ، وَمَنْ قُتِلَ دُونَ أهْلِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema Abil A'war Sa'iyd bin Zayd bin 'Amruw bin Nufayl (Radhwiya Allaah 'anhu) mmoja miongoni wa wale Swahaaba kumi waliobashiriwa Pepo: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kuuliwa kwa sababu ya kuilinda mali yake ni shahidi na mwenye kuuliwa katika kujilinda ni shahidi na mwenye kuuliwa kwa ajili ya Dini yake ni shahidi na mwenye kuuliwa akiilinda familia yake ni shahidi." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : يَا رسولَ اللهِ ، أرَأيتَ إنْ جَاءَ رجلٌ يُرِيدُ أخْذَ مَالِي ؟ قَالَ : (( فَلاَ تُعْطِهِ مَالَكَ )) قَالَ : أَرَأَيْتَ إنْ قَاتَلَنِي ؟ قَالَ : (( قَاتِلْهُ )) قَالَ : أرَأَيْتَ إنْ قَتَلَنِي ؟ قَالَ : (( فَأنْتَ شَهِيدٌ )) قَالَ : أَرَأيْتَ إنْ قَتَلْتُهُ ؟ قَالَ : (( هُوَ فِي النَّارِ )) رواه مسلم .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alikuja mtu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Unaonaje akija mtu kutaka kuchukua mali yangu", Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Usimpe mali yako." Akasema: "Wasemaje akipigana nami?" Akasema: "Pigana naye?" Akasema: "Wasemaje akiniua?" Akasema: "Wewe utakuwa umekufa shahidi." Akauliza tena: "Wasemaje nikimuua?" Akasema: "Yeye atakwenda Motoni." [Muslim]

 

 

Share