01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Dhikri na Kuhimizwa Juu Yake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فَضلِ الذِّكْرِ وَالحَثِّ عليه
01-Mlango Wa Fadhila za Dhikri na Kuhimizwa Juu Yake
قال الله تَعَالَى :
وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۗ ﴿٤٥﴾
Na bila shaka kumdhukuru Allaah ndilo kubwa zaidi. [Al-'Ankabuwt: 45]
فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ ﴿١٥٢﴾
Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni. [Al-Baqarah: 152]
وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ ﴿٢٠٥﴾
Na mdhukuru Rabb wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na kwa ulimi bila sauti kubwa asubuhi na jioni, na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika. [Al-A'raaf: 205]
وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿١٠﴾
Na mdhukuruni Allaah kwa wingi ili mpate kufaulu. [Al-Jumua'ah]
وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾
Na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake, Allaah Amewaandalia Maghfirah na ujira adhimu. [Al-Ahzaab: 35]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿٤١﴾
Enyi walioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru.
وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٤٢﴾
Na Msabbihini asubuhi na jioni. [Al-Ahzaab: 41-42]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلَى اللِّسَانِ ، ثَقِيلَتَانِ فِي المِيزَانِ ، حَبِيبَتَانِ إِلَى الرَّحْمانِ : سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ العظيمِ )) . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Maneno mawili ni mepesi ulimini, mazito katika mizani na yanapendwa na Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma): Subhaana LLaahi wa Bihamdihi Subhaana LLaahil 'Adhiym (Ametakasika Allaah na sifa zote njema anastahiki, Ametakasika Allaah Mtukufu)." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لأَنْ أَقُولَ : سُبْحَانَ اللهِ ؛ وَالحَمْدُ للهِ ؛ وَلاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ ، وَاللهُ أكْبَرُ ، أَحَبُّ إلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kwa mimi kusema: Subhaana Allaah, wal HamduliLLaah, wa Laa Ilaaha Illa Allaah (Ametakasika Allaah, na Sifa zote njema anastahili Allaah na hapana Mola muabudiwa kwa haki ila Allaah na Allaah ni Mkuu) Inanipendeza zaidi kuliko vitu vyote vilivyo chomozewa na jua." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( مَنْ قَالَ لا إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَريكَ لَهُ ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ ؛ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، في يَوْمٍ مِئَةَ مَرَّةٍ كَانَتْ لَهُ عَدْلَ عَشْرِ رِقَابٍ وكُتِبَتْ لَهُ مِئَةُ حَسَنَةٍ ، وَمُحِيَتْ عَنْهُ مِئَةُ سَيِّئَةٍ ، وَكَانَتْ لَهُ حِرْزاً مِنَ الشَّيْطَانِ يَوْمَهُ ذَلِكَ حَتَّى يُمْسِي ، وَلَمْ يَأتِ أَحَدٌ بِأَفْضَلَ مِمَّا جَاءَ بِهِ إِلاَّ رَجُلٌ عَمِلَ أكْثَرَ مِنْهُ )) . وقال : (( مَنْ قَالَ سُبْحَانَ الله وَبِحَمْدِهِ ، في يَوْمٍ مِئَةَ مَرَّةٍ ، حُطَّتْ خَطَايَاهُ ، وَإنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ البَحْرِ )) . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusema Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa Shariyka lahu, lahul Mulku walahul Hamdu wa Huwa ;alaa kulli shay'in Qadiyr (Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, Aliye peke Yake wala hana mshirika, Yeye Ndiye Mwenye Ufalme na sifa zote njema anastahiki Yeye tu Naye ni Muweza wa kufanya kila kitu), kila siku mara mia moja. Zitakuwa kwake sawa na kuacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa mema mia moja, na atafutiwa maovu mia moja. Na itakuwa kinga kwake kumkinga na shetani, siku yake hiyo mpaka jioni. Hakuna yeyote atakayelifanya lililo bora zaidi yake, isipokuwa atakayefanya zaidi ya alivyofanya." Na akasema: "Atakayesema: "Subhaana Allaahi wa Bihamdihi (Ametakasika Allaah na sifa zote njema ni Zake), mara mia moja kwa siku, yatafutwa makosa yake, hata kama yalikuwa kama povu la bahari." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 4
وعن أَبي أيوب الأنصاريِّ رضي اللهُ عنه ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ قَالَ لا إلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ ؛ وَلَهُ الحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، عَشْرَ مَرَّاتٍ . كَانَ كَمَنْ أعْتَقَ أرْبَعَةَ أنْفُسٍ منْ وَلَدِ إسْمَاعِيلَ )) . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Ayyuwb Al-Answaariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakayesema Laa ilaaha illa LLaahu Wahdahu laa Shariyka lahu, lahul Mulku walahul Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay'in Qadiyr (Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, Aliye Peke Yake wala hana mshirika, Yeye Ndiye Mwenye Ufalme na sifa zote njema anastahiki Yeye tu naye ni Muweza wa kufanya kila kitu), mara kumi atakuwa sawa na mwenye kuacha huru nafsi (watumwa) nne katika watoto wa Ismaa'iyl." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ألاَ أُخْبِرُكَ بِأَحَبِّ الكَلاَمِ إِلَى اللهِ ؟ إنَّ أَحَبَّ الكَلاَمِ إِلَى اللهِ : سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ )) . رواه مسلم .
Amesema Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu): Aliniambia mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi w sallam): "Je, nikueleze maneno yanayo mpendeza zaidi Allaah? Hakika maneno yanayo mpendeza Allaah ni Subhaana Allaahi wa Bihamdihi." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن أَبي مالك الأشعري رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( الطُّهُورُ شَطْرُ الإيمانِ ، وَالحَمْدُ للهِ تَمْلأُ المِيزَانَ ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالحَمْدُ للهِ تَمْلآنِ – أَوْ تَمْلأُ – مَا بَيْنَ السَّمَاوَاتِ وَالأرْضِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Maalik Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kujitwahirisha ni nusu ya Imaan, na AlhamdulliLLaah (Kila sifa njema anastahiki Allaah) linajaza mizani, na Subhaana Allaah (Allaah ameepukana na kila ya upungufu / Ametakasika Allaah) na AlhamdulliLLaah yanajaza baina ya mbingu na ardhi." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن سعد بن أَبي وقاصٍ رضي اللهُ عنه قَالَ: جَاءَ أعْرَابيٌّ إِلَى رَسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : عَلِّمْنِي كَلاَماً أقُولُهُ . قَالَ : (( قُلْ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَريكَ لَهُ ، اللهُ أكْبَرُ كَبِيراً ، وَالحَمْدُ للهِ كَثيراً ، وَسُبْحَانَ اللهِ رَبِّ العَالِمينَ ، وَلاَ حَولَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللهِ العَزِيزِ الحَكِيمِ )) قَالَ : فهؤُلاءِ لِرَبِّي ، فَمَا لِي ؟ قَالَ : (( قُلْ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ، وَارْحَمْنِي وَاهْدِنِي ، وَارْزُقْنِي )) . رواه مسلم .
Amesema Sa'ad bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuja Bedui kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akaomba: "Nifundishe maneno ambayo nitakuwa nayasema." Akasema: Sema "Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa Sharika lahu, Allaahu Akbar Kabiyra wal Hamdu LiLLaahi Kathiyran wa Subhaana Allaahi Rabbil 'Aalamiyn walaa Hawla walaa Quwwata illa BiLLaahil 'azizil Hakiym" (Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, Peke Yake wala hana mshirika. Allaah ni Mkuu sana na Sifa njema zote na nyingi ni Zake na Ametakasika Allaah Rabb wa walimwengu wote. Na hapana hila wala nguvu isipokuwa kuwezeshwa na Allaah, Mwenye Nguvu na Mwenye Hekima)." Akasema: "Haya ni maneno kwa Rabb wangu. Yangu ni yepi?" Akasema: "Sema: Allaahumma Ghfirliy warhamniy wahdiniy warzuqniy (Ee Mola wangu wa haki! Nighufurie (madhambi yangu), na Unirehemu, na Uniongoze na Uniruzuku)." [Muslim]
Hadiyth – 8
وعن ثَوبانَ رضي اللهُ عنه قَالَ : كَانَ رَسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا انْصَرَفَ مِنْ صَلاَتِهِ اسْتَغْفَرَ ثَلاثَاً ، وَقَالَ : (( اللَّهُمَّ أنْتَ السَّلاَمُ ، وَمِنْكَ السَّلاَمُ ، تَبَارَكْتَ يَاذَا الجَلاَلِ وَالإكْرَامِ )) قِيلَ لِلأوْزَاعِيِّ - وَهُوَ أحَدُ رواة الحديث - : كَيْفَ الاسْتِغْفَارُ ؟ قَالَ : يقول : أسْتَغْفِرُ الله ، أسْتَغْفِرُ الله . رواه مسلم .
Thawbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa anapoandoka toka kwenye Swalaah akileta Istighfar (AstaghfiruLLaah - Nisamehe Ee Allaah) mara tatu na baadae akisema: "Allaahumma Antas Salaam wa Minkas Salaam Tabaarakta Yaa Dhal Jalaal wal Ikraam (Ee Mola wangu wa Haki! Wewe Ndiwe Amani na Kwako kunatoka amani, Umetukuka ee Mwenye Enzi na Mwenye Kustahiki Kuheshimika)." Aliulizwa Al-Awzaa'iy, naye ni mmoja wa wapokezi wa Hadiyth: "Hii Istighfar inaletwa vipi?" Akasema: "Sema: AstaghfiruLLaah, AstaghfiruLLaah." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن المغيرة بن شعبة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا فَرَغَ مِنَ الصَّلاَةِ وَسَلَّمَ ، قَالَ : (( لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، اللَّهُمَّ لاَ مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلاَ يَنْفَعُ ذَا الجَدِّ مِنْكَ الجَدُّ )) . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake Mughiyrah bin Shu'bah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alipomaliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah yake na kutoa salamu akisema: "Laa ilaaha illaAllaah Wahdahu laa shariyka lahu, lahul Mulku walahul Hamdu wa Huwa 'alaa kuli shay'in Qadiyr. Allaahumma Laa Maani'a limaa A'twayta walaa Mu'twiya limaa Mana'ta walaa yanfa'u dhal jaddi Minkal Jadd (Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Yu Peke Yake wala hana mshirika, Yeye Ndiye Mwenye Ufalme na sifa zote njema anastahiki Yeye tu Naye ni Muweza wa kufanya kila kitu. Ee Rabb wangu! Hapana wa kuzuia Ulichotoa wala hapana wa kutoa Ulichozuia, wala tajiri hautamfaa utajiri wake mbele Yako)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 10
وعن عبدِ الله بن الزُّبَيْرِ رضي الله تَعَالَى عنهما أنَّه كَانَ يَقُولُ دُبُرَ كُلِّ صَلاَةٍ ، حِيْنَ يُسَلِّمُ : (( لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَريكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ . لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللهِ ، لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ ، وَلاَ نَعْبُدُ إِلاَّ إيَّاهُ ، لَهُ النِّعْمَةُ وَلَهُ الفَضْلُ وَلَهُ الثَّنَاءُ الحَسَنُ ، لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الكَافِرُونَ )) قَالَ ابْنُ الزُّبَيْرِ : وَكَانَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، يُهَلِّلُ بِهِنَّ دُبُرَ كُلِّ صَلاَةٍ . رواه مسلم .
Alikuwa 'Abdillaah bin Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu 'anhu) akisema baada ya kila Swalaah ya faradhi, pindi anapotoa salamu dua ifuatayo: "Laa ilaaha illaAllaahu Wahdahu laa Shariyka lahu, lahul Mulku walahul Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay'in Qadiyr. Laa hawla wala Quwwata illaa BiLLaah laa ilaaha illaAllaahu, walaa na'budu illaa Iyyaahu lahun Ni'matu, walahul Fadhlu, walahuth Thana'ul hasan. Laa ilaaha illaa Allaahu Mukhliswiyna lahud Diyna walaw karihal Kaafiruwn. (Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Yu Peke Yake wala hana mshirika, Yeye Ndiye Mwenye Ufalme na sifa zote njema anastahiki Yeye tu naye ni Muweza wa kufanya kila kitu. Na hapana hila wala nguvu isipokuwa Allaah wala hatumuabudu ila Yeye. Yeye ndiye Mwenye fadhila na Ndiye Mwenye kusifiwa kwema. Hapana Mola wa kuabudiwa isipokuwa Allaah, tunaitakasa Dini Yake japokuwa watachukia makafiri)." Amesema Ibn Az-Zubayr: "Na alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akimpwekesha Allaah kwa kuleta (dhikri hii) baada ya kila Swalaah ya faradhi." [Muslim]
Hadiyth – 11
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ فُقَراءَ المُهَاجِرِينَ أَتَوْا رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فقالوا : ذَهَبَ أهْلُ الدُّثورِ بِالدَّرَجَاتِ العُلَى ، وَالنَّعِيمِ المُقِيمِ ، يُصَلُّونَ كَمَا نُصَلِّي ، وَيَصُومُونَ كَمَا نَصُومُ، وَلَهُمْ فَضْلٌ مِنْ أمْوَالٍ ، يَحُجُّونَ ، وَيَعْتَمِرُونَ ، وَيُجَاهِدُونَ ، وَيَتَصَدَّقُونَ . فَقَالَ : (( ألاَ أُعَلِّمُكُمْ شَيْئاً تُدْرِكُونَ بِهِ مَنْ سَبَقَكُمْ ، وَتَسْبَقُونَ بِهِ مَنْ بَعْدَكُمْ ، وَلاَ يَكُون أَحَدٌ أفْضَل مِنْكُمْ إِلاَّ منْ صَنَعَ مِثْلَ مَا صَنَعْتُمْ ؟ )) قالوا : بَلَى يَا رسول الله ، قَالَ : (( تُسَبِّحُونَ ، وَتَحْمَدُونَ ، وَتُكَبِّرُونَ ، خَلْفَ كُلِّ صَلاَةٍ ثَلاثاً وَثَلاثِينَ )) قَالَ أَبُو صالح الراوي عن أَبي هريرة ، لَمَّا سُئِلَ عَنْ كَيْفِيَّةِ ذِكْرِهِنَّ قَالَ : يقول : سُبْحَان اللهِ ، وَالحَمْدُ للهِ واللهُ أكْبَرُ ، حَتَّى يَكُونَ مِنهُنَّ كُلُّهُنَّ ثَلاثاً وَثَلاثِينَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
وزاد مسلمٌ في روايته : فَرَجَعَ فُقَراءُ المُهَاجِرينَ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فقالوا : سَمِعَ إخْوَانُنَا أهْلُ الأمْوَالِ بِمَا فَعَلْنَا فَفَعَلُوا مِثْلَهُ ؟ فَقَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ذَلِكَ فَضْلُ الله يُؤتِيهِ مَنْ يَشَاءُ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mafukara wa Muhaajiriyn walikuwa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Wenye mali wameondoka na daraja za juu na neema za daima: Wao wanaswali kama tunavyoswali na wafunga kama tunavyofunga. Na wana fadhila ya mali: Wanakwenda Hijjah, na kutekeleza Umrah, na wanapigana Jihaad na wantoa Swadaqah." Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je, si wafundishi nyinyi kitu ambacho kwayo mutawafikia waliowapiteni na mutashindana na wale watakaokuja baada yenu na hakuna atakaye kuwa bora kuliko nyinyi isipokuwa yule atakayefanya kama munavyofanya?" Wakasema: "Ndio (tuambie) ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Msabihini Allaah(kwa kusema Subhaana Allaah), muhimidini (kwa kusema AlhamduliLLaah) na leteni takbiri baada ya kila Swalaah (ya Faradhi) mara thelethini na tatu (33)." Akasema Abu Swalih mpokezi kutoka kwa Abu Huraiyrah: "Aliulizwa jinsi ya kutekeleza dhikri hii." Akasema: "Wanasema: Subhaana Allaah wal HamduliLLaah wa Allaahu Akbar, mpaka zifike zote hizo mara thelathini na tatu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na Abu Daawuwd]
Na ameongeza Muslim katika riwaayah yake: "Baada ya muda walirudi tena mafakiri wa Muhaajiriyn kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: Ndugu zetu wenye mali wamesikia kwa yale tunayofanya na wakawa wanafanya mfano wetu?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hiyo ni fadhila kutoka kwa Allaah naye anampatia amtakaye."
Hadiyth – 12
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ سَبَّحَ الله في دُبُرِ كُلِّ صَلاَةٍ ثَلاثاً وَثَلاثِينَ ، وحَمِدَ اللهَ ثَلاثاً وَثَلاَثِينَ ، وَكَبَّرَ الله ثَلاثاً وَثَلاَثِينَ ، وقال تَمَامَ المِئَةِ : لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لَهُ ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، غُفِرَتْ خَطَايَاهُ وَإنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ البَحْرِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kumsabih Allaah baada ya kila Swalaah ya faradhi mara thelathini na tatu na akamuhimidi Allaah mara thelathini na tatu na akaleta takbira mara thelathini na tatu na akasema kukamilisha mara mia: Laa ilaaha illaAllaahu Wahdahu laa Shariyka Lahu, Lahul Mulku walahul Hamdu wa Huwa 'alaa kuli shay'in Qadiyr, atasamehewa makosa yake japokuwa yatakuwa kama povu la bahari." [Muslim]
Hadiyth – 13
وعن كعب بن عُجْرَةَ رضي اللهُ عنه ، عن رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مُعَقِّباتٌ لاَ يَخِيبُ قَائِلُهُنَّ – أَوْ فَاعِلُهُنَّ – دُبُرَ كُلِّ صَلاَةٍ مَكْتُوبَةٍ: ثَلاثٌ وَثَلاثونَ تَسْبِيحَةً. وَثَلاثٌ وثَلاَثونَ تَحْمِيدَةً ، وَأرْبَعٌ وَثَلاَثونَ تَكْبِيرَةً )) . رواه مسلم.
Imepokewa kutoka kwake Ka'b bin 'Ujrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Zipo Dhikri baada ya kila Swalaah ya faradhi, mwenye kuzisoma hatavunjika moyo - au mwenye kuzifanya. Hiyo ni kuleta tasbihi mara thelathini na tatu, tahmidi mara thelathini na tatu na takbira mara thelathini na nne." [Muslim]
Hadiyth – 14
وعن سعد بن أَبي وقاص رضي اللهُ عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يَتَعَوَّذُ دُبُرَ الصَّلَواتِ بِهؤُلاءِ الكَلِمَاتِ : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعوذُ بِكَ مِنَ الجُبْنِ وَالبُخْلِ ، وَأعُوذُ بِكَ مِنْ أنْ أُرَدَّ إِلَى أَرْذَلِ العُمُرِ ، وَأعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الدُّنْيَا ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ القَبْرِ )) . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwake Sa'd bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akijikinga baada ya kila Swalaah ya faradhi kwa maneno haya: "Allaahumma inni a'uwdhu bika minal jubni wal bukhli wa a'iuwdhu bika min an uradda ila ardhalil 'umri wa a'uwdhu bika min fitnatid dunyaa wa a'uwdhu bika min fitnatil qabri (Ee Rabb wangu! Hakika mimi najilinda Kwako na uzembe na ubakhili, na najilinda Kwako na kurudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, na najilinda Kwako na fitna ya dunia na najilinda Kwako na fitna ya kaburini)." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 15
وعن معاذ رضي اللهُ عنه : أن رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، أخذ بيده ، وقال : (( يَا مُعَاذُ ، وَاللهِ إنِّي لأُحِبُّكَ )) فَقَالَ : (( أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ لاَ تَدَعَنَّ في دُبُرِ كُلِّ صَلاَة تَقُولُ : اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ ، وَشُكْرِكَ، وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ )) . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimshika mkono wake na kumwambia: "Ee Mu'aadh! Naapa kwa Allaah kuwa nakupenda." Na akasema: "Nakuusia ee Mu'aadh usiache kusema baada ya kila Swalaah ya faradhi (maneno yafuatayo): "Allaahumma a'iinniy 'alaa Dhikrika wa Shukrika wa Husni 'Ibaadatika (Ee Rabb wangu! Nisaidie juu ya utajo wako na Kushukuriwa Kwako na uzuri wa ibada Yako)." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]
Hadiyth – 16
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا تَشَهَّدَ أَحَدُكُمْ فَلْيَسْتَعِذْ بِاللهِ مِنْ أرْبَعٍ ، يقول : اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ ، وَمِنْ عَذَابِ القَبْرِ ، وَمِنْ فِتْنَةِ المَحْيَا وَالْمَمَاتِ ، وَمِنْ شَرِّ فِتْنَةِ المَسِيحِ الدَّجَّالِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapopiga shahada (katika Tahiyyatu) mmoja wenu basi atake ulinzi wa Allaah kwa mambo manne kwa kusema: "Allaahumma Inni A'uwdhu Bika min 'adhaabil qabri wa min fitnatil mahyaa wal mamaat wa min sharri fitnatil Masiyhid Dajjaal (Ee Rabb wangu! Hakika mimi najilinda Kwako na adhabu ya ahanam, na adhabu ya kaburini, na fitna ya uhai na mauti na shari ya fitna ya Masiyhi Dajjaal)." [Muslim]
Hadiyth – 17
وعن عليٍّ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ يَكُونُ مِنْ آخِرِ مَا يَقُولُ بَيْنَ التَّشَهُّدِ وَالتَّسْلِيمِ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أخَّرْتُ ، وَمَا أسْرَرْتُ وَمَا أعْلَنْتُ ، وَمَا أسْرَفْتُ ، وَمَا أنْتَ أعْلَمُ بِهِ مِنِّي ، أنْتَ الْمُقَدِّمُ ، وَأنْتَ المُؤَخِّرُ ، لا إلهَ إِلاَّ أنْتَ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa anaposimama kwa ajili ya Swalaah maneno ya mwisho anayo yasema baina ya Tashahhud na kutoa salamu ni: "Allaahumma Ghfirli maa qaddamtu wa maa Akhkhartu wa maa asrartu wa maa a'lantu wa maa asraftu wa maa anta a'lamu bihi minniy antal muqaddimu wa antal mu'akhkhiru laa ilaaha illa Anta (Ee Rabb wangu! Nisamehe mimi madhambi niliyotanguliza na yanayokuja, na niliyofanya kwa siri na niliyodhihirisha, niliyoyafanyia isirafu, na yale madhambi, Unayoyajua zaidi kuliko mimi mwenyewe. Wewe Mwenye kutanguliza na Wewe Ndiye Mwenye kuchelewesha. Hapana Mola wa kuabudiwa ila Wewe)." [Muslim]
Hadiyth – 18
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم يُكْثِرُ أنْ يَقُولَ في رُكُوعِهِ وَسُجُودِهِ : (( سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وبِحَمْدِكَ ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي )) متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akikithirisha kusema katika kurukuu na kusujudu: "Subhaanakal Lahumma Rabbaana wa Bihamdika Allahumma Ghfirli (Utakaso ni Wako ee Allaah na sifa zote njema Unastahiki Wewe, ee Rabb Wangu nisamehe)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nisaaiy]
Hadiyth – 19
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يقولُ في رُكُوعِهِ وَسُجُودِهِ : (( سبُّوحٌ قُدُّوسٌ رَبُّ المَلاَئِكَةِ وَالرُّوحِ )) . رواه مسلم .
Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa katika Rukuu' na sijdah yake akisema: "Subbuwhun Qudduws Rabbul Malaaikati war Ruuh (Ametakasifu mno Mtukufu mno Rabb wa Malaaikah na roho)." [Muslim]
Hadiyth – 20
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( فَأمَّا الرُّكُوعُ فَعَظِّمُوا فِيهِ الرَّبَّ عزوجل ، وَأمَّا السُّجُودُ فَاجْتَهِدُوا في الدُّعَاءِ ، فَقَمِنٌ أنْ يُسْتَجَابَ لَكُمْ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ama katika rukuu Mtukuzeni Rabb ndani yake na katika kusujudu fanyeni juhudi katika kuomba duaa. Kwani ni hakika kujibiwa duaa zenu." [Muslim]
Hadiyth – 21
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أقْرَبُ مَا يَكُونُ العَبْدُ مِنْ رَبِّهِ وَهُوَ سَاجِدٌ ، فَأَكْثِرُوا الدُّعَاءَ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mja anakuwa karibu na Rabb wake akiwa katika sijdah, hivyo jitahidini na ongezeni duaa (katika hali hiyo ya sijdah)." [Muslim]
Hadiyth – 22
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقُولُ في سجودِهِ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لي ذَنْبِي كُلَّهُ : دِقَّهُ وَجِلَّهُ ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ ، وَعَلاَنِيَتَهُ وَسِرَّهُ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema yafuatayo anaposujudu: "Allaahummaghfirli dhambi kullahu diqqahu wa jillahu, wa awwalahu wa aakhirahu, wa 'alaaniyatahu wa sirrahu (Ee Rabb wangu! Nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, na za dhahiri na za siri)." [Muslim]
Hadiyth – 23
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها، قالت : افْتَقَدْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، ذَاتَ لَيْلَةٍ ، فَتَحَسَّسْتُ ، فإذا هُوَ راكِعٌ – أَوْ سَاجِدٌ – يقولُ : (( سُبْحَانَكَ وَبِحَمْدِكَ ، لاَ إلهَ إِلاَّ أنت )) وفي روايةٍ : فَوَقَعَتْ يَدِي عَلَى بَطْنِ قَدَمَيْهِ ، وَهُوَ في المَسْجِدِ وَهُمَا مَنْصُوبَتَانِ ، وَهُوَ يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ ، وَبِمعَافَاتِكَ مِنْ عُقُوبَتِكَ، وأعُوذُ بِكَ مِنْكَ، لاَ أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ أنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ )). رواه مسلم .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nilimkosa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) usiku mmoja, nami nikaanza kumtafuta, nikampata akiwa katika rukuu au sijdah akiomba kwa kusema: "Subhaanaka wa Bihamdika Laa ilaaha illa Anta (Utakaso ni wako na sifa zote njema unastahiki Wewe. Hapana Mola wa kuabudiwa isipokuwa Wewe)."
Na katika riwaayah nyingine: "Mkono wangu ukashika matumbo ya mguu wake yakiwa yamesimamishwa wima akiwa ndani ya Msikiti, naye anasema: "Allaahumma inni a'uwdhu Biridhwaaka min Sakhatwika wa Bimu'aafatika min 'Uquwbatika wa a'uwdhu Bika Minka Laa uhswaa Thanaa'an 'Alayka Anta kamaa Athnayta 'alaa Nafsika (Ee Mola wangu! Mimi ninajilinda kwa radhi Zako dhidi ya ghadhabu Zako, na msamaha Wako dhidi ya adhabu Yako, na ninaomba ulinzi Wako. Mimi sidhibiti kutaja (au kuhesabu) sifa Zako wewe ni kama Ulivyo jisifu Mwenyewe)." [Muslim]
Hadiyth – 24
وعن سعد بن أَبي وقاصٍ رضي الله عنه قَالَ : كنا عِنْدَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( أيعجزُ أحَدُكُمْ أنْ يَكْسِبَ في كلِّ يومٍ ألْفَ حَسَنَةٍ ! )) فَسَأَلَهُ سَائِلٌ مِنْ جُلَسائِهِ : كَيْفَ يَكْسِبُ ألفَ حَسَنَةٍ ؟ قَالَ : (( يُسَبِّحُ مِئَةَ تَسْبِيحَةٍ فَيُكْتَبُ لَهُ ألْفُ حَسَنَةٍ ، أَوْ يُحَطُّ عَنْهُ ألفُ خَطِيئَةٍ )) . رواه مسلم .
Amesema Sa'd bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akasema: "Je, anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku hasanah (thawabu) elfu moja?" Akamuuliza muulizaji miongoni mwa waliokuwa katika kikao hicho: "Vipi atachuma mema elfu moja?" Akasema: "Amtakase (Allaah) kwa kuleta Tasbihi mia moja (kwa kusema Subhaana Allaah), hivyo kuandikiwa mema elfu moja au afutiwe madhambi elfu moja." [Muslim]
Hadiyth – 25
وعن أَبي ذر رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يُصْبحُ عَلَى كُلِّ سُلاَمَى مِنْ أَحَدِكُمْ صَدَقةٌ : فَكُلُّ تَسْبيحَةٍ صَدَقةٌ ، وَكُلُّ تَحْميدَةٍ صَدَقَةٌ ، وَكُلُّ تَهْلِيلةٍ صَدَقَةٌ ، وَكُلُّ تَكْبيرَةٍ صَدَقَةٌ ، وأمْرٌ بالمَعْرُوفِ صَدَقَةٌ ، وَنَهْيٌ عَنِ المُنْكَرِ صَدَقَةٌ ، وَيجْزئُ مِنْ ذَلِكَ رَكْعَتَانِ يَرْكَعُهُمَا مِنَ الضُّحَى )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Kila kiungo cha mmoja wenu kinapambazukiwa kwa kufanya Swadaqah (jambo jema). Hivyo kila tasbiyh ni swadaqah, na kila tahmiyd ni swadaqah, na kila takbiyra ni swadaqah na kuamrisha mema ni swadaqah na kukataza mabaya ni swadaqah. Na rakaa mbili za Swalaah ya Dhuwhaa unazoswali zatosheleza (kama swadaqah ya yote haya)." [Muslim]
Hadiyth – 26
وعن أم المؤمنين جُويْريَةَ بنت الحارِث رَضِيَ اللهُ عنها: أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم خرجَ مِنْ عِنْدِهَا بُكْرَةً حِيْنَ صَلَّى الصُّبْحَ وَهِيَ في مَسْجِدِها ، ثُمَّ رَجَعَ بَعدَ أنْ أضْحَى وَهِيَ جَالِسَةٌ ، فقالَ : (( مَا زِلْتِ عَلَى الحالِ الَّتي فَارقَتُكِ عَلَيْهَا ؟ )) قالت : نَعَمْ ، فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( لَقَدْ قُلْتُ بَعْدَكِ أرْبَعَ كَلِمَاتٍ ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، لَوْ وُزِنَتْ بِمَا قُلْتِ مُنْذُ اليَوْمِ لَوَزَنَتْهُنَّ : سُبْحَانَ الله وَبِحَمْدِهِ عَدَدَ خَلْقِهِ ، وَرِضَا نَفْسِهِ ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ ، وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ )) . رواه مسلم .
وفي روايةٍ لَهُ : (( سُبْحانَ الله عَدَدَ خَلْقِهِ ، سُبْحَانَ الله رِضَا نَفْسِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ زِنَةَ عَرْشِهِ ، سُبْحَانَ الله مِدَادَ كَلِمَاتِهِ )) .
وفي رواية الترمذي: (( ألا أُعَلِّمُكِ كَلِمَاتٍ تَقُولِينَهَا؟ سُبحَانَ الله عَدَدَ خَلْقِهِ؛ سُبحَانَ الله عَدَدَ خَلْقِهِ ، سُبحَانَ الله عَدَدَ خَلْقِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ رِضَا نَفْسِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ رِضَا نَفْسِهِ ، سُبْحَانَ الله رِضَا نَفْسِهِ ، سُبْحَانَ الله زِنَةَ عَرْشِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ زِنَةَ عَرشِهِ ، سُبْحَانَ الله زِنَةَ عَرشِهِ ، سُبْحَانَ الله مِدَادَ كَلِمَاتِهِ ، سُبْحَانَ الله مِدَادَ كَلِمَاتِهِ ، سُبْحَانَ الله مِدَادَ كَلِمَاتِهِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini, Juwayriyah bin Al-Haarith (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka chumbani kwake mapema pindi aliposwali Swalaah ya Asubuhi, naye (Juwayriyah) alikuwa akiswali. Baadae alirudi (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kuswali Swalaah ya Dhuwhaa, naye (Juwayriyah) alikuwa bado ameketi (katika mswala wake). Akasema: "Bado upo katika hali ile ile niliyokuacha nayo?" Nikasema: "Ndiyo." Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika baada ya kuondoka nimesema maneno manne mara tatu, lau zitapimwa na kufananishwa na yale uliyosema asubuhi ya leo basi zitakuwa ni nzito zaidi: Subhaana Allaahi Wa Bihamdihi 'adada Khalqihi wa Ridhwaa' Nafsihi wa zinata 'Arshihi wa midaada Kalimaatih
Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) na namhimidi kwa idadi ya Viumbe Vyake, na kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake, na kwa uzito wa ‘Arshi Yake, na kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake. [Muslim]
Na katika riwaayah yake nyengine:
سُبْحانَ الله عَدَدَ خَلْقِهِ ، سُبْحَانَ الله رِضَا نَفْسِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ زِنَةَ عَرْشِهِ ، سُبْحَانَ الله مِدَادَ كَلِمَاتِهِ
"Subhaana Allaahi 'adada Khalqihi, Subhaana Allaahi Ridhwaa' Nafsihi, Subhaana Allaahi zinata 'Arshihi, Subhaana Allaahi midaada Kalimatih
Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) kwa idadi ya Viumbe Vyake, Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake, Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) kwa uzito wa ‘Arshi Yake, Namtakasa Allaah kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake.
Na katika riwaayah ya At-Tirmidhiy: "Sikufundishi maneno ambayo utayasema?
سُبحَانَ الله عَدَدَ خَلْقِهِ؛ سُبحَانَ الله عَدَدَ خَلْقِهِ ، سُبحَانَ الله عَدَدَ خَلْقِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ رِضَا نَفْسِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ رِضَا نَفْسِهِ ، سُبْحَانَ الله رِضَا نَفْسِهِ ، سُبْحَانَ الله زِنَةَ عَرْشِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ زِنَةَ عَرشِهِ ، سُبْحَانَ الله زِنَةَ عَرشِهِ ، سُبْحَانَ الله مِدَادَ كَلِمَاتِهِ ، سُبْحَانَ الله مِدَادَ كَلِمَاتِهِ ، سُبْحَانَ الله مِدَادَ كَلِمَاتِهِ
"Subhaana Allaahi 'adada Khalqihi, Subhaana Allaahi 'adada Khalqihi, Subhaana Allaahi 'adada Khalqihi, Subhaana Allaahi Ridhwaa' Nafsihi, Subhaana Allaahi Ridhwaa' Nafsihi, Subhaana Allaahi Ridhwaa' Nafsihi, Subhaana Allaahi zinata 'Arshihi, Subhaana Allaahi zinata 'Arshihi, Subhaana Allaahi zinata 'Arshihi, Subhaana Allaahi midaada Kalimatih, Subhaana Allaahi midaada Kalimatih, Subhaana Allaahi midaada Kalimatih.
Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) kwa idadi ya Viumbe Vyake (mara tatu), Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake (mara tatu), Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) kwa uzito wa ‘Arshi Yake (mara tatu), Namtakasa Allaah kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake (mara tatu).
Hadiyth – 27
وعن أَبي موسى الأشعري رَضِيَ اللهُ عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَثَلُ الَّذِي يَذْكُرُ رَبَّهُ وَالَّذِي لا يَذْكُرُهُ مَثَلُ الحَيِّ وَالمَيِّتِ )) . رواه البخاري .
ورواه مسلم فَقَالَ : (( مَثَلُ البَيْتِ الَّذِي يُذْكَرُ اللهُ فِيهِ ، وَالبَيْتِ الَّذِي لا يُذْكَرُ اللهُ فِيهِ ، مَثَلُ الحَيِّ والمَيِّتِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mfano wa yule mwenye kumdhukuru Rabb wake na yule asiye mdhukuru, ni mfano wa aliye hai na maiti." [Al-Bukhaariy]
Na amepokea Muslim kwa kusema: "Mfano wa nyumba ambayo Allaah hutajwa ndani yake na nyumba asiyotajwa Allaah ndani yake, ni mfano wa kilicho hai na maiti."
Hadiyth – 28
وعن أَبي هريرة رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يقول الله تَعَالَى : أنا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي ، وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي ، فإنْ ذَكَرَنِي في نَفْسِهِ ، ذَكَرْتُهُ في نَفْسِي ، وإنْ ذَكَرنِي في ملأٍ ذَكرتُهُ في مَلأٍ خَيْرٍ مِنْهُمْ )) متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Amesema Allaah Ta'aalaa: "Mimi niko katika dhana ya mja Wangu. Nami niko pamoja naye anaponikumbuka; Anaponikumbuka nafsini mwake, Nitamkumbuka Nafsini Mwangu, na anaponikumbuka penye wengi, Nitamkumbuka penye wengi bora zaidi yao." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 29
وعن أَبي هريرة رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( سَبَقَ المُفَرِّدُونَ )) قالوا : وَمَا المُفَرِّدُونَ ؟ يَا رسولَ الله قَالَ: (( الذَّاكِرُونََ اللهَ كثيراً والذَّاكِرَاتِ )) . رواه مسلم.
وَرُوي : (( المُفَرِّدُونَ )) بتشديد الراءِ وتخفيفها والمشهُورُ الَّذِي قَالَهُ الجمهُورُ : التَّشْديدُ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wameongoza Mufarriduwn." Wakauliza: "Na Mufarriduwn ni kina nani, ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Wanaume wenye kumdhukuru Allaah kwa wingi na wanawake." [Muslim].
Imepokewa al-Mufarriduwn kwa kuweka shaddah katika herufi "ra" na bila ya shaddah na iliyo mashuhuri ni ile iliyopokewa na Jamhuwr: "Kuweka shaddah."
Hadiyth – 30
وعن جابر رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( أفْضَلُ الذِّكْرِ : لا إلهَ إِلاَّ اللهُ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Bora ya dhikri ni kusema Laa ilaaha illaAllaah." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 31
وعن عبد الله بن بسر رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ رجلاً قَالَ : يَا رسولَ الله ، إنَّ شَرَائِعَ الإسْلامِ قَدْ كَثُرَتْ عَليَّ ، فَأَخْبِرْنِي بِشَيءٍ أَتَشَبثُ بِهِ قَالَ : (( لا يَزالُ لِسَانُكَ رَطباً مِنْ ذِكْرِ الله )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Busr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa kuna mtu alisema: "Ee Rasuli wa Allaah! hakika sheria za Kiislamu zimekuwa nyingi juu yangu, nijulishe kitu (chepesi na rahisi) ambacho nitakishika barabara." Akasema: "Uwache ulimi wako uwe majimaji (ujishughulishe sana) katika kumdhukuru Allaah." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 32
وعن جابر رَضِيَ اللهُ عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( من قَالَ : سُبْحان الله وبِحمدِهِ ، غُرِسَتْ لَهُ نَخْلَةٌ في الجَنَّةِ )) . رواه الترمذي، وقال : (( حديث حسن )).
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusema Subhaana Allaahi wa Bihamdihi, huotesha mtende Peponi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 33
وعن ابن مسعود رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لَقِيْتُ إبْرَاهِيمَ لَيلَةَ أُسْرِيَ بِي ، فَقَالَ : يَا مُحَمّدُ أقْرِىءْ أُمَّتَكَ مِنِّي السَّلاَمَ ، وَأَخْبِرْهُمْ أنَّ الجَنَّةَ طَيَّبَةُ التُّرْبَةِ ، عَذْبَةُ الماءِ ، وأنَّهَا قِيعَانٌ وأنَّ غِرَاسَهَا : سُبْحَانَ اللهِ ، والحَمْدُ للهِ ، وَلاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ ، واللهُ أكْبَرُ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilikutana na Ibraahiym ('Alayhis salaam) usiku wa Israa', naye akaniambia: "Ee Muhammad! Watolee salamu Ummah wako kutoka kwangu na uwape habari kuwa Pepo ina mchanga mzuri na maji yake ni matamu na hakika ni pana sana (yenye nafasi muruwa) na kuwa mimea yake ni Subhaana Allaah wal HamduliLLaah wa Laa ilaaha illaaAllaahu wa Allaahu Akabar." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 34
وعن أَبي الدرداءِ رَضِيَ اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ألا أُنَبِّئُكُمْ بِخَيْرِ أعْمالِكُمْ ، وأزْكَاهَا عِنْدَ مَلِيكِكُمْ ، وأرْفَعِهَا في دَرَجَاتِكُمْ ، وَخَيرٍ لَكُمْ مِنْ إنْفَاقِ الذَّهَبِ والفِضَّةِ ، وَخَيْرٍ لَكُمْ مِنْ أن تَلْقَوا عَدُوَّكُمْ فَتَضْرِبُوا أعْنَاقَهُمْ وَيَضْرِبُوا أعْنَاقَكُمْ ؟ )) قَالَوا : بَلَى ، قَالَ : (( ذِكر الله تَعَالَى )) . رواه الترمذي ، قَالَ الحاكم أَبُو عبد الله : (( إسناده صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Je, siwaambii nyinyi amali bora kwenu, ambayo ni safi kabisa mbele ya mfalme wenu na yenye kunyanyua daraja yenu na ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha na ni bora kwenu kuliko kukutana na adui zenu na kuwakata shingo zao na wao kukata shingo zenu?" Wakasema: "Ndio." Akasema: "umdhukuru Allaah Ta'aalaa." [At-Tirmidhiy, na akasema Al-Haakim Abu 'Abdillaah kuwa Isnaad yake ni Swahiyh]
Hadiyth – 35
وعن سعد بن أَبي وقاص رَضِيَ اللهُ عنه ، أنَّه دخل مَعَ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ، عَلَى امْرأةٍ وَبَيْنَ يَدَيْها نَوىً – أَوْ حَصَىً – تُسَبِّحُ بِهِ فَقَالَ : (( أُخْبِرُكِ بما هُوَ أيْسَرُ عَلَيْكِ مِنْ هَذَا - أَوْ أفْضَلُ - )) فَقَالَ : (( سُبْحَانَ الله عَدَدَ مَا خَلَقَ في السَّمَاءِ ، وسُبْحَانَ الله عَدَدَ مَا خَلَقَ في الأرْضِ ، وسُبْحَانَ الله عَدَدَ مَا بَيْنَ ذَلِكَ ، وسُبحَانَ الله عَدَدَ مَا هز خَالِقٌ ، واللهُ أكْبَرُ مِثْلَ ذَلِكَ ، والحَمْدُ للهِ مِثْلَ ذَلِكَ ؛ وَلاَ إلَهَ إِلاَّ اللهُ مِثْلَ ذَلِكَ ، وَلاَ حَولَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللهِ مِثْلَ ذَلِكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Sa'ad bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa walikwenda pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mwanamke ambaye mbele yake kulikuwa na rundo la kokwa za tende au vijiwe, ambazo alikuwa akitumia kusabihi navyo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Je, nikuambie jambo ambalo ni jepesi kwako kuliko hili au ni bora zaidi?" Akasema: "Subhaana Allaahi kwa idadi ya alivyo viumba katika ardhi na Subhaana Allaahi kwa idadi ya vilivyoko baina yake. Na Subhaana Allaahi kwa idadi ya Alivyoviumba na Atakavyo viumba. Na Allaahu Akbar mfano wa hizo na AlhamduliLLaah mfano wa kama hizo na Laa ilaaha illaAllaahu mfano wa idadi hiyo na Laa Hawla walaa Quwwaata illaa BiLLaahi mfano wa hizo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 36
وعن أَبي موسى رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ لي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ألا أدُلُّكَ عَلَى كَنْزٍ مِنْ كُنُوزِ الجَنَّةِ ؟ )) فقلت : بلى يَا رسولَ الله قَالَ : (( لا حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ )) متفق عَلَيْهِ .
Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Aliniambia mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Sikujulishi wewe hazina miongoni mwa hazina za Peponi?" Nikasema: "Nieleze, ee Rasuli wa Allaah! Akasema: "Laa Hawla walaa Quwwataa illaa BiLLaahi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawud na At-Tirmidhiy]