02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kumdhukuru Allaah Ta'aalaa kwa Kusimama, Kukaa, Kujilaza na katika Hadathi, Janaba, Hedhi Isipokuwa Kusoma Qur-aan Ambayo Haifai Kusomwa kwa Mwenye Janaba na Hedhi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب ذكر الله تَعَالَى قائماً أَوْ قاعداً ومضطجعاً
ومحدثاً وجنباً وحائضاً إِلاَّ القرآن فَلاَ يحل لجنب وَلاَ حائض
02-Mlango Wa Kumdhukuru Allaah Ta'aalaa kwa Kusimama, Kukaa, Kujilaza na katika Hadathi, Janaba, Hedhi Isipokuwa Kusoma Qur-aan Ambayo Haifai Kusomwa kwa Mwenye Janaba na Hedhi
قال الله تَعَالَى :
إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾
الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ ﴿١٩١﴾
Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio) kwa wenye akili. Ambao wanamdhukuru Allaah wakiwa wima, au wamekaa au wamejinyoosha [Aal-'Imraan: 190-191]
Hadiyth – 1
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : كَانَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم يَذْكُرُ اللهَ عَلَى كُلِّ أَحْيَانِهِ . رواهُ مسلم .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akimtaja (akimdhukuru) Allaah Ta'aalaa kila wakati." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن ابن عباسٍ رَضِيَ اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَوْ أنَّ أَحَدَكُمْ إِذَا أتَى أهْلَهُ قَالَ : بِسْمِ الله ، اللَّهُمَّ جَنِّبْنَا الشَّيْطَانَ ، وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا ، فَقُضِيَ بَيْنَهُمَا وَلَدٌ ، لَمْ يَضُرَّهُ )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau mmoja wenu atamwingilia mkewe akasema: "BismiLLaahi Allaahumma Jannibnaa ash-shaytwaana wa Jannibish shaytwaana Maa Razaqtana (Kwa jina la Allaah, ee Rabb wangu! Tuepushe na shetani na umuepushie shetani kile utakacho Turuzuku). Watakapojaaliwa kupata mtoto basi hatadhuriwa (na shetani)." [Al-Bukhaariy na Muslim]