04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila ya Vikundi vya Dhikri na Kupendeza Kujilazimisha Nayo na Kukatazwa Kujiondosha Bila ya Udhuru
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل حِلَقِ الذكر
والندب إِلَى ملازمتها والنهي عن مفارقتها لغير عذر
04-Mlango Wa Fadhila ya Vikundi vya Dhikri na Kupendeza Kujilazimisha Nayo na Kukatazwa Kujiondosha Bila ya Udhuru
قال الله تَعَالَى :
وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ ﴿٢٨﴾
Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke [Al-Kahf: 28]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ للهِ تَعَالَى مَلائِكَةً يَطُوفُونَ في الطُّرُقِ يَلْتَمِسُونَ أهْلَ الذِّكْرِ ، فإذا وَجَدُوا قَوْمَاً يَذْكُرُونَ اللهَ عزوجل ، تَنَادَوْا : هَلُمُّوا إِلَى حَاجَتِكُمْ ، فَيَحُفُّونَهُمْ بِأَجْنِحَتِهِم إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا ، فَيَسْألُهُمْ رَبُّهُمْ – وَهُوَ أعْلَم - : مَا يقولُ عِبَادي ؟ قَالَ : يقولون : يُسَبِّحُونَكَ ، ويُكبِّرُونَكَ ، وَيَحْمَدُونَكَ ، ويُمَجِّدُونَكَ ، فيقول : هَلْ رَأَوْنِي ؟ فيقولونَ : لا واللهِ مَا رَأَوْكَ . فيقولُ : كَيْفَ لَوْ رَأوْني ؟! قَالَ : يقُولُونَ : لَوْ رَأوْكَ كَانُوا أَشَدَّ لَكَ عِبَادَةً ، وَأَشَدَّ لَكَ تَمْجِيداً ، وأكْثَرَ لَكَ تَسْبِيحاً . فَيقُولُ : فماذا يَسْألونَ ؟ قَالَ : يقُولُونَ : يَسْألُونَكَ الجَنَّةَ . قَالَ : يقولُ : وَهل رَأَوْها ؟ قَالَ : يقولون : لا واللهِ يَا رَبِّ مَا رَأَوْهَا . قَالَ : يقول : فَكيفَ لَوْ رَأوْهَا ؟ قَالَ : يقولون : لَوْ أنَّهُمْ رَأوْهَا كَانُوا أشَدَّ عَلَيْهَا حِرْصاً ، وأشدَّ لَهَا طَلَباً ، وأعْظَمَ فِيهَا رَغْبَةً . قَالَ : فَمِمَّ يَتَعَوَّذُونَ ؟ قَالَ : يقولون : يَتَعَوَّذُونَ مِنَ النَّارِ ؛ قَالَ : فيقولُ : وَهَلْ رَأوْهَا ؟ قَالَ : يقولون : لا واللهِ مَا رَأوْهَا . فيقولُ : كَيْفَ لَوْ رَأوْهَا ؟! قَالَ : يقولون : لَوْ رَأوْهَا كانوا أشَدَّ مِنْهَا فِرَاراً ، وأشَدَّ لَهَا مَخَافَةً . قَالَ : فيقولُ : فَأُشْهِدُكُمْ أنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُم ، قَالَ : يقولُ مَلَكٌ مِنَ المَلاَئِكَةِ : فِيهم فُلاَنٌ لَيْسَ مِنْهُمْ ، إنَّمَا جَاءَ لِحَاجَةٍ ، قَالَ : هُمُ الجُلَسَاءُ لا يَشْقَى بِهِمْ جَلِيسُهُمْ )) . متفق عَلَيْهِ .وفي رواية لمسلمٍ عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إن للهِ مَلاَئِكَةً سَيَّارَةً فُضُلا يَتَتَبُّعُونَ مَجَالِسَ الذِّكْرِ ، فَإذَا وَجَدُوا مَجْلِساً فِيهِ ذِكْرٌ ، قَعَدُوا مَعَهُمْ ، وَحَفَّ بَعْضُهُمْ بَعْضاً بِأجْنِحَتِهِمْ حَتَّى يَمْلَؤُوا مَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ السَّماءِ الدُّنْيَا ، فإذَا تَفَرَّقُوا عَرَجُوا وَصَعدُوا إِلَى السَّمَاءِ ، فَيَسْأَلُهُمْ اللهُ عزوجل - وَهُوَ أعْلَمُ - : مِنْ أيْنَ جِئْتُمْ ؟ فَيَقُولُونَ : جِئْنَا مِنْ عِنْدِ عِبادٍ لَكَ في الأرْضِ : يُسَبِّحُونَكَ ، ويُكبِّرُونَكَ ، وَيُهَلِّلُونَكَ ، وَيَحْمَدُونَكَ ، وَيَسْألُونَكَ . قَالَ : وَمَاذا يَسْألُونِي ؟ قالوا : يَسْألُونَكَ جَنَّتَكَ . قَالَ : وَهَلْ رَأَوْا جَنَّتِي ؟ قالوا : لا ، أَيْ رَبِّ . قَالَ : فكيْفَ لَوْ رَأَوْا جَنَّتي ؟! قالوا : ويستجيرونكَ . قَالَ : ومِمَّ يَسْتَجِيرُونِي ؟ قالوا : مِنْ نَارِكَ يَا رَبِّ . قَالَ : وَهَلْ رَأوْا نَاري ؟ قالوا : لا ، قَالَ : فَكَيْفَ لَوْ رَأَوْا نَارِي ؟! قالوا : وَيَسْتَغفِرُونكَ ؟ فيقولُ : قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ ، وَأَعْطَيْتُهُمْ مَا سَألُوا ، وَأجَرْتُهُمْ مِمَّا اسْتَجَارُوا . قَالَ : فيقولون : ربِّ فيهمْ فُلانٌ عَبْدٌ خَطَّاءٌ إنَّمَا مَرَّ ، فَجَلَسَ مَعَهُمْ . فيقُولُ : ولهُ غَفَرْتُ ، هُمُ القَومُ لاَ يَشْقَى بِهِمْ جَلِيسُهُمْ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Anao Malaaikah wanaozunguka majiani, wanawafafuta wanao dhikiri (wanao mtukuza Allaah). Wanapowakuta watu wanamtaja Allaah, wanaita: 'Njooni! Kwenye kile mnachokihitaji.' Watazunguka kwa mbawa zao mpaka kufikia uwingu wa dunia. Rabb wao Atawauliza, hali Anajua zaidi yao: 'Wanasema nini waja Wangu?' Malaaikah watajibu: 'Wanasema: Wanakusabihi na wana kutukuza (kwa kusema Allaahu Akbar) na wanakuhimidi na wanakutukuza.' Kisha Allaah Atawauliza: 'Je, wameniona?' Watajibu: 'Hapana Wa-Allaahi! Hawajakuona.' Atauliza: 'Vipi kama wangeli niona?' Watasema: 'Kama wangeli kuona wangeli kuabudu zaidi, wangeli kutukuza zaidi, na wangeli kutakasa kwa wingi zaidi.' Atauliza: 'Wananimba nini?' Watajibu: 'Wanakuomba Pepo.' Atauliza: 'Je, wameiona?' Watasema: 'Hapana Wa-Allaahi! Ee Rabb hawakuiona.' Atawauliza: 'Vipi kama wangeona?' Watasema: 'Kama wangaliiona wangalikuwa na pupa nayo zaidi, wangeli itaka zaidi, na wangalikuwa na mapenzi nayo makubwa zaidi.' Atauliza: 'Wanajilinda na nini?' Watasema: 'Na moto.' Atauliza: Je, wameuona?' Watajibu: 'Hapana Wa-Allaahi! Hawakuuona.' Atasema: 'Vipi kama wangeuona?' Watasema: 'Kama wangeliuona wangeli kimbia zaidi, na wangeli uogopa zaidi.' Atasema: 'Hapo Allaah atawaambia nini washuhudisha kuwa mimi Nimewasamehe.' Atasema Malaaikah miongoni mwa Malaaikah: 'Kati yao kuna fulani, sio miongoni mwao. Bali alikuja kwa mahitaji (mengine).' Allaah Atasema: 'Hao ndio wenye kikao, na anyekaa nao, kwa ajili yao, hawi na maisha mabaya.' [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Muslim: Kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Anacho kikosi cha Malaaikah wanaotembelea wakitafuta vikao vya dhikri. Wanapopata kikao cha dhikri, wanakaa pamoja nao, na kufunika baadhi yao kwa wengine kwa mbawa zao na baina ya uwingu wa dunia. Pindi wanapoondoka na kuelekea mbinguni. Allaah 'Azza wa Jalla atawauliza japokuwa Anajua zaidi: 'Je, munatoka wapi?' Watajibu: 'Sisi tunatoka kwa waja Wako walio ardhini, na Wanakusabihi, na wanaleta takbiri na tahlili na Wanakuhimidi na Kukuomba.' Atauliza: 'Na Wananiomba nini?' Watajibu: 'Wanakuomba Pepo.' Atauliza: 'Na je, wameiona Pepo Yangu?' Watasema: 'Hapana ee Rabb.' Atauliza: 'Vipi kama wangeliiona Pepo Yangu?' Watasema: 'Na wanataka ulinzi kutoka Kwako.' Atauliza: 'Na wanajilinda na nini?' Watajibu: 'Na Moto Wako, ee Rabb.' Atauliza: 'Na je, wameuona Moto Wangu?' Watajibu: 'Hapana.' Atauliza: 'Vipi kama wangaliuona Moto Wangu?' Watasema: 'Na wanataka msamaha kutoka Kwako.' Atasema: 'Hakika Nimewasamehe na Nimewapatia walichoomba na Nimewalinda kwa walichotaka ulinzi kwacho.' Akasema: Watasema Malaaikah: 'Rabb wetu! Kati yao kuna fulani ambaye ni mja mwenye kufanya madhambi. Hakika yeye alikuwa anapita, akakaa nao.' Atasema: 'Na yeye pia Nimemsamehe. Wao watu ambao hawawi na maisha mabaya."
Hadiyth – 2
وعنه وعن أَبي سعيدٍ رضي الله عنهما ، قالا : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لا يَقْعُدُ قَومٌ يَذكُرُونَ اللهَ عزوجل إِلاَّ حَفَّتْهُمُ المَلائِكَةُ وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ وَنَزَلَتْ عَلَيْهِمْ السَّكِينَةُ ؛ وَذَكَرَهُمُ اللهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hawakai watu kumdhukuru Allaah isipokuwa huzungukwa na Malaaikah, na hufunikwa na rehma (kutoka kwa Allaah), na huteremkiwa na utulivu na Allaah huwataja kwa walioko Naye." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي واقدٍ الحارث بن عوف رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم بَيْنَمَا هُوَ جَالِسٌ في المَسْجِدِ ، والنَّاسُ مَعَهُ ، إذْ أقْبَلَ ثَلاثَةُ نَفَرٍ ، فأقْبَلَ اثْنَانِ إِلَى رسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَذَهَبَ واحِدٌ ؛ فَوَقَفَا عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم . فأمَّا أحَدُهُما فَرَأَى فُرْجةً في الحَلْقَةِ فَجَلَسَ فِيهَا ، وَأمَّا الآخرُ فَجَلَسَ خَلْفَهُمْ ، وأمَّا الثَّالثُ فأدْبَرَ ذاهِباً . فَلَمَّا فَرَغَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( ألاَ أُخْبِرُكُمْ عَنِ النَّفَرِ الثَّلاَثَةِ : أَمَّا أَحَدُهُمْ فَأوَى إِلَى اللهِ فآوَاهُ اللهُ إِلَيْهِ . وَأمَّا الآخَرُ فاسْتَحْيَى فَاسْتَحْيَى اللهُ مِنْهُ ، وأمّا الآخَرُ ، فَأعْرَضَ ، فَأَعْرَضَ اللهُ عَنْهُ )) . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Waaqid Al-Haarith bin 'Awf (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa amekaa Msikitini na watu wakiwa pamoja naye, mara wakaja watu watatu. Wawili (kati ya hao watatu) walikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na watatu wao akaenda zake, wakasimama mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ama mmoja wao aliona nafasi katika kiako, akaenda akaaa hapo na yule mwingine alikaa nyuma ya kikao hicho. Ama yule watatu aligeuka na kwenda zake. Alipomaliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mazungumzo yake alisema: "Siwajulishi nyinyi kuhusu hawa watu watatu: Ama mmoja wao, alikuja kwa Allaah, Naye Akamjia (kwa kumfunika na kumuweka chini ya ulinzi Wake). Na ama yule wa pili aliona haya na hivyo Allaah kumuonea haya. Na ama yule wa mwisho, aligeuka na kwenda zake, na hivyo Allaah akageuka kutoka Kwake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه قَالَ : خرج معاوية رضي الله عنه عَلَى حَلْقَةٍ في المَسْجِدِ ، فَقَالَ : مَا أجْلَسَكُمْ ؟ قالوا : جَلَسْنَا نَذْكُرُ اللهَ . قَالَ : آللهِ مَا أجْلَسَكُمْ إِلاَّ ذاك ؟ قالوا : مَا أجْلَسَنَا إِلاَّ ذَاكَ ، قَالَ : أما إنِّي لَمْ اسْتَحْلِفْكُمْ تُهْمَةً لَكُمْ ، وَمَا كَانَ أحَدٌ بِمَنْزِلَتِي مِنْ رَسولِ الله صلى الله عليه وسلم أَقَلَّ عَنْهُ حَديثاً مِنِّي : إنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم خَرَجَ عَلَى حَلْقَةٍ مِنْ أصْحَابِهِ فَقَالَ : (( مَا أجْلَسَكُمْ ؟ )) قالوا : جَلَسْنَا نَذْكُرُ الله وَنَحْمَدُهُ عَلَى مَا هَدَانَا للإسْلاَمِ ؛ وَمَنَّ بِهِ عَلَيْنَا . قَالَ : (( آللهِ مَا أجْلَسَكُمْ إِلاَّ ذَاكَ ؟ )) قالوا : واللهِ مَا أجْلَسَنَا إِلاَّ ذَاكَ . قَالَ : (( أمَا إنِّي لَمْ أسْتَحْلِفْكُمْ تُهْمَةً لَكُمْ ، ولكِنَّهُ أتَانِي جِبرِيلُ فَأخْبَرَنِي أنَّ الله يُبَاهِي بِكُمُ المَلاَئِكَةَ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy kuwa amesema: Siku moja Mu'aawiyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alizuru Msikiti na kuona Halaqah (duara ya wasomaji). Akauliza: "Ni kipi kilichowafanya nyinyi mkae?" Wakajibu: "Tumekaa ili kumdhukuru Allaah." Akauliza: "Kwa Allaah, hamkukaa ila kwa sababu hiyo." Wakajibu: "Hatukukaa isipokuwa kwa hilo." Akasema: "Ama mimi sikuwaambia muape kwa kuwatuhumu. Na hakuna yeyote katika daraja yangu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kupokea Hadiyth chache sana kuliko mimi. Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja katika Halaqah ya Swahaaba zake na kuwauliza: 'Ni kipi kilicho wafanya muwe katika kikao?' Wakajibu: 'Tumekaa ili tumdhukuru Allaah na kumhimidi kwa kutuongoa (kutuingiza) katika Uislamu na kutupatia neema hiyo.' Akauliza: Kwa Allaah, hamkukaa ila kwa sababu hiyo." Wakajibu: "Hatukukaa isipokuwa kwa hilo." Akasema: "Ama kwa hakika! MImi sijawafanya muape kwa kuwatuhumu (au kuwa na shaka) nyinyi, lakini amekuja kwangu Jibriyl na kunipasha habari kuwa Allaah Amefurahi sana na kuwasifu nyinyi mbele ya Malaaikah Zake." [Muslim]