05-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kumtaja Allaah Asubuhi na Jioni
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الذكر عِنْدَ الصباح والمساء
05-Mlango Wa Kumtaja Allaah Asubuhi na Jioni
قال الله تَعَالَى :
وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ ﴿٢٠٥﴾
Na mdhukuru Rabb wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na kwa ulimi bila sauti kubwa asubuhi na jioni, na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika. [Al-A'raaf: 205]
وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا ۖ ﴿١٣٠﴾
Na sabihi ukimhimidi Rabb wako kabla ya kuchomoza jua, na kabla ya kuchwa kwake. [Twaahaa: 130]
وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ﴿٥٥﴾
Na sabbih na mhimidi Rabb wako jioni na asubuhi. [Gaafir: 55]
فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّـهُ أَن تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ ﴿٣٦﴾
Katika nyumba ambazo Allaah Ameidhinisha litukuzwe na litajwe humo Jina Lake, wanamsabihi humo asubuhi na jioni.
رِجَالٌ لَّا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ ۙ يَخَافُونَ يَوْمًا تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَارُ ﴿٣٧﴾
Wanaume ambao haiwashughulishi tijara wala uuzaji na kumdhukuru Allaah na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah wanakhofu Siku zitakapopinduka humo nyoyo na macho. [An-Nuwr: 36-37]
إِنَّا سَخَّرْنَا الْجِبَالَ مَعَهُ يُسَبِّحْنَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِشْرَاقِ ﴿١٨﴾
Hakika Sisi Tulitiisha milima iwe pamoja naye ikisabbih jioni na baada ya kuchomoza jua. [Swaad: 18]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ قَالَ حِيْنَ يُصْبِحُ وَحينَ يُمْسِي : سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ ، مِئَةَ مَرَّةٍ ، لَمْ يَأتِ أَحَدٌ يَوْمَ القِيَامَةِ بِأفْضَلَ مِمَّا جَاءَ بِهِ ، إِلاَّ أحَدٌ قَالَ مِثْلَ مَا قَالَ أَوْ زَادَ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusema asubuhi na jioni Subhaana Allaahi wa Bihamdihi mara mia moja, hatakuja na jambo (amali) bora yeyote Siku ya Qiyaamah isipokuwa yule aliyesema mfano wake au aliyezidisha." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : جَاءَ رجلٌ إِلَى النبيّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا رسولَ الله مَا لَقِيْتُ مِنْ عَقْرَبٍ لَدَغَتْنِي البَارِحَةَ ! قَالَ : (( أمَا لَوْ قُلْتَ حِيْنَ أمْسَيْتَ : أعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ : لَمْ تَضُرَّك )) . رواه مسلم .
Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Niliumwa na nge jana usiku hivyo kupata maumivu makubwa." Akasema: "Ama kama ungelisema pindi kunapoingia usiku A'uwdhu bikalimaati LLaahit Taammaati min sharri maa Khalaq (Ninajilinda kwa maneno timilifu ya Allaah kutokana na shari ya Ulivyo viumba), hivyo nge hangekudhuru." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم ، أنَّه كَانَ يقولُ إِذَا أصْبَحَ : (( اللَّهُمَّ بِكَ أصْبَحْنَا ، وَبِكَ أمْسَيْنَا ، وَبِكَ نَحْيَا ، وَبِكَ نَمُوتُ ، وَإلَيْكَ النُّشُورُ )) . وإذا أمسَى قَالَ : (( اللَّهُمَّ بِكَ أمْسَيْنَا ، وبِكَ نَحْيَا ، وَبِكَ نَمُوتُ . وَإلْيَكَ النُّشُورُ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema kunapo pambazuka: "Allaahumma bika aswbahna wa bika amsayna wa bika nahyaa wa bika namuwt wa ilaykan nushuwr (Ee Rabb Wangu! Kwa fadhila Zako ndio tunafika asubuhi na Kwako ndio tunafika jioni na kwa neema Yako ndio tunabaki hai na Kwako ndio tunakufa, na Kwako ndio marejeo yetu)." Na anapofikiwa na jioni akisema: "Allaahumma bika amsayna wa bika nahyaa wa bika namuwtu wa ilaykan nushuwr (Ee Rabb Wangu! Kwa fadhila Zako ndio tunafika jioni, na kwa neema Yako ndio tunabaki hai na Kwako ndio tunakufa, na Kwako ndio marejeo yetu)." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ أَبَا بكرٍ الصديق رضي اللهُ عنه قَالَ : يَا رسول الله مُرْني بِكَلِمَاتٍ أقُولُهُنَّ إِذَا أصْبَحْتُ وإذا أمْسَيْتُ ، قَالَ : (( قُلْ : اللَّهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاواتِ والأرْضِ عَالِمَ الغَيْبِ والشَّهَادَةِ ؛ رَبَّ كُلِّ شَيْءٍ وَمَلِيكَهُ ، أَشْهَدُ أنْ لا إلَهَ إِلاَّ أنْتَ ، أعُوذُ بِكَ مِنْ شَّرِّ نَفْسِي وَشَرِّ الشَّيْطَانِ وَشِرْكِهِ )) قَالَ : (( قُلْهَا إِذَا أصْبَحْتَ ، وإذَا أمْسَيْتَ ، وإذَا أخَذْتَ مَضْجَعَكَ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Abu Bakr As-Swiddiq (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Niamuru mimi kwa maneno (ya duaa) ambayo nitayasoma wakati wa asubuhi na jioni." Akasema: "Sema: Allaahumma Faatwiras Samaawaati wal ardhwi 'Aalimal ghaybi wash-shahaadati Rabba kulli shay'in wa maliykahu Ashhadu an laa illaaha illa Anta A'uwdhu Bika min sharri nafsiy wa sharrish Shaytwaan wa shirkih (Ee Rabb Wangu! Muumbaji wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa yaliyofichikana na yaliyo dhahiri. Rabb na Mwenye kumiliki kila kitu. Nashuhudia ya kwamba hapana muabuduwa wa haki ila Wewe. Ninajilinda Kwako kutokana na shari ya nafsi yangu na shari ya shetani na anavyoitia katika kumshirikisha Allaah)." Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Yaseme hayo asubuhi na jioni na unapokwenda kitandani (kwa ajili ya kulala)." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 5
وعن ابن مسعودٍ رضي اللهُ عنه قَالَ : كَانَ نبيُّ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا أَمْسَى قَالَ : (( أَمْسَيْنَا وأمْسَى المُلْكُ للهِ ، والحَمْدُ للهِ ، لا إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَريكَ لَهُ )) قَالَ الراوي : أَرَاهُ قَالَ فِيهِنَّ : (( لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدير ، رَبِّ أسْألُكَ خَيْرَ مَا في هذِهِ اللَّيْلَةِ وَخَيْرَ مَا بَعْدَهَا ، وَأعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا في هذِهِ اللَّيْلَةِ وَشَرِّ مَا بَعْدَهَا ، رَبِّ أعُوذُ بِكَ مِنَ الكَسَلِ ، وَسُوءِ الكِبَرِ ، رَبِّ أعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابٍ في النَّارِ ، وَعَذَابٍ في القَبْرِ )) ، وَإذَا أصْبَحَ قَالَ ذَلِكَ أيضاً (( أصْبَحْنَا وأصْبَحَ المُلْكُ للهِ )) . رواه مسلم .
Amesema Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa inapoingia jioni (usiku) akisema: "Amsaynaa wa amsaal Mulku Lillaahi wal HamduliLLaahi, Laa ilaaha illaAllaahu wahdahu laa Shariyka lahu (Tumeingiliwa na jioni na kuingia usiku katika ufalme wa Allaah na sifa zote njema anastahiki Allaah. Hapana Rabb wa kuabudiwa isipokuwa Allaah Peke Yake hana mshirika kabisa)." Amesema mpokezi: "Naona kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ndani yake: "Lahul Mulku wa lahul Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay'in Qadiyr. Rabbi As'aluka khayra maa fiy hadhihil laylah wa khayra maa ba'dahaa wa a'uwdhu Bika min sharri maa fiy hadhihil laylah wa sharri maa ba'dahaa, Rabbi a'uwdhu Bika minal kasalwa suuil kibari, Rabbi a'uwdhu Bika min 'adhaabin fii naar wa 'adhaabin fil qabr (Ufalme ni Wake na sifa njema anastahiki Yeye na Yeye tu Ndiye aliye juu ya kila jambo, Mwenye Uwezo mkubwa sana. Rabb wangu nakuomba kheri iliyopo ndani ya usiku huu na kheri ya baada yake. Na ninajilinda Kwako na shari ya yaliyomo ndani ya usiku huu na shari ya baada yake. Rabbi, ninajilinda Kwako na uvivu na ouvu wa uzee, ninajilinda Kwako na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburini)." Na kunapo pambazuka akisema hayo pia: "Aswbahnaa wa aswbahal Mulku LiLLaahi (Kupambazuka kwetu na kupambazuka katika ufalme wa Allaah)." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن عبد الله بن خُبَيْب - بضم الخاء المعجمة - رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ لي رَسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( اقْرَأْ : قُلْ هُوَ اللهُ أحَدٌ ، والمُعَوِّذَتَيْنِ حِيْنَ تُمْسِي وَحِينَ تُصْبحُ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ تَكْفيكَ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Khubayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Soma: Qul Huwa Allaahu Ahad na kinga mbili (Suratul Falaq na Suratun Naas) kunapoingia jioni na kunapo pambazuka mara tatu, zitakutosheleza lwa kila kitu (zitakuwa ni ngao kwako dhidi ya kila kitu kiovu)." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 7
وعن عثمان بن عفان رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ عَبْدٍ يَقُولُ في صَبَاحِ كُلِّ يَوْمٍ وَمَسَاءِ كُلِّ لَيْلَةٍ : بِسْمِ اللهِ الَّذِي لا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ في الأرْضِ وَلاَ في السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ العَلِيمُ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، إِلاَّ لَمْ يَضُرَّهُ شَيْءٌ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana mja yeyote atakayesema kila siku asubuhi na jioni: BismiLLaahi lladhiy laa yadhuwrru ma'a ismuhu shay'un fil ardhi wa laa fis samaa'i wa Huwas Samiy'ul 'Aliym (Kwa jina la Allaah ambaye kwamba kwa baraka ya Jina Lake, hakitanidhuru kitu chochote ardhini na mbinguni, Naye ni Mwenye husikia Mjuzi) mara tatu ila hatadhurika na chochote." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]