01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Duaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل الدعاء

 01-Mlango Wa Fadhila za Duaa

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ ﴿٦٠﴾

Na Rabb wenu Amesema: Niombeni, Nitakuitikieni. [Gaafir: 60]

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾

Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka. [Al-A'raaf: 55]

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ  ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza Waja Wangu kuhusu Mimi, basi (waambie) Mimi Niko Karibu (kwa ujuzi). Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. [Al-Baqarah: 186]

أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ  ﴿٦٢﴾

Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea uovu. [An-Naml: 62]

 

Hadiyth – 1

وعن النعمان بن بشيرٍ رضي الله عنهما ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الدُّعَاءُ هُوَ العِبَادَةُ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'ahumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Duaa ni Ibaadah." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : كَانَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم يَسْتَحِبُّ الجَوَامِعَ مِنَ الدُّعَاءِ ، وَيَدَعُ مَا سِوَى ذَلِكَ . رواه أَبُو داود بإسناد جيدٍ .

'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akipenda sana duaa zilizokamilika na kuacha nyinginezo. [Abu Daawuwd kwa Isnaad nzuri]

 

Hadiyth – 3

وعن أنس رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : كَانَ أكثرُ دعاءِ النبيّ صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ آتِنَا في الدُّنْيَا حَسَنَةً ، وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً ، وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

زاد مسلم في روايتهِ قَالَ : وَكَانَ أَنَسٌ إِذَا أرادَ أنْ يَدْعُوَ بِدَعْوَةٍ دَعَا بِهَا ، وَإِذَا أرادَ أنْ يَدْعُوَ بِدُعَاءٍ دَعَا بِهَا فِيهِ .

Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Duaa aliyokuwa akiiomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sana ni: "(Rabb Wetu! Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukunge na adhabu ya moto) [Al-Baqarah: 201]." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Ameongeza Muslim katika riwaayah yake, akasema: "Na Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa anapotaka kuomba dua hutumia dua hiyo. Na akitaka kuomba dua yoyote hujumlisha dua hii ndani yake." 

 

Hadiyth – 4

وعن ابن مسعودٍ رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ الهُدَى ، والتُّقَى ، والعَفَافَ ، والغِنَى )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Allaahumma inniy as'alukal hudaa wat tuqaa wal 'afaafa wal ghinaa (Ee Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba unipatie uongofu, na uchaji Mungu (taqwa), na utohara na utajiri (kwa kuupa nyongo ulimwengu)." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن طارق بن أَشْيَمَ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : كَانَ الرَّجُلُ إِذَا أسْلَمَ عَلَّمَهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم الصَّلاَةَ ثُمَّ أمَرَهُ أنْ يَدْعُوَ بِهؤلاَءِ الكَلِمَاتِ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ، وَارْحَمْنِي ، وَاهْدِني ، وَعَافِني ، وَارْزُقْنِي )) . رواه مسلم .

وفي روايةٍ له عن طارق: أنَّه سمع النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، وأتاهُ رَجُلٌ فَقَالَ : يَا رسول اللهِ ، كَيْفَ أقُولُ حِيْنَ أسْأَلُ رَبِّي ؟ قَالَ : (( قُلْ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ، وَارْحَمْنِي ، وَعَافِني ، وارْزُقْنِي ، فإنَّ هؤلاَءِ تَجْمَعُ لَكَ دُنْيَاكَ وَآخِرَتَكَ )) .

Amesema Twariq bin Ashyam: Ilikuwa mtu anaposilimu, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) humfundisha Swalaah, kisha humuamuru aombe kwa maneno haya: "Allaahumma Ghfirliy warhamniy wahdiniy wa 'aafiniy warzuqniy (Rabb Wangu! Nisamehe, na Unirehemu, na Uniruzuku)." [Muslim]

Na katika riwaayah yake nyingine kutoka kwa Twaariq: kuwa alimsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomjia mtu na kumuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Niseme vipi ninapomuomba Rabb wangu." Akaniambia: "Sema Allaahumma Ghfirliy warhamniy wa 'aafiniy warzuqniy (Mola Wangu! Nisamehe, na Unirehemu, na Uniponyeshe na Uniruzuku), kwani maombi haya yanajumlisha mabo yako ya dunia na Aakherah."

 

Hadiyth – 6

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ مُصَرِّفَ القُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبنَا عَلَى طَاعَتِكَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaahumma muswarrifal quluwbi swarrif quluwbanaa 'alaa twaa'atika (Rabb Wangu! Mwenye kuongoza mioyo, Iongoze mioyo yetu katika twaa Yakoo)." [Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( تَعَوَّذُوا بِاللهِ مِنْ جَهْدِ البَلاَءِ ، وَدَرَكِ الشَّقَاءِ ، وَسُوءِ القَضَاءِ ، وَشَمَاتَةِ الأَعْدَاءِ )) متفق عَلَيْهِ .

وفي روايةٍ قَالَ سفيان : أَشُكُّ أنِّي زِدْتُ واحدةً مِنْهَا .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Takeni ulinzi kutoka kwa Allaah na balaa la mtihani, na kupatwa na maisha mabaya (Aahkerah), na hukumu mbaya na furaha ya maadui." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah: Sufyaan Amesema: "Nina shaka kuwa mimi nimezidisha moja kati ya hayo mambo." 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( اللَّهُمَّ أصْلِحْ لِي دِيني الَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أمْرِي ، وأصْلِحْ لِي دُنْيَايَ الَّتي فِيهَا مَعَاشِي ، وأصْلِحْ لِي آخِرتِي الَّتي فِيهَا مَعَادي ، وَاجْعَلِ الحَيَاةَ زِيَادَةً لِي في كُلِّ خَيْرٍ ، وَاجْعَلِ المَوتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ )) . رواه مسلم .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Allaahumma aswlih liy Diyniy ladhiy huwa 'iswmatiu amriy wa aswlih liy dunyaayal latiy fiyhaa ma'ashiy wa aswlih liy aakhiratiyl latiy fiyhaa ma'aadiy waj'alil hayaata ziyaadatan liy fiy kuli khayr waj'alil mawta raahatan liy min kuli sharr (Rabb Wangu! Nitengenezee Dini yangu ambayo ndiyo yenye kulinda mambo yangu, na Nitengenezee mimi dunia yangu ambayo ndiyomsingi wa maisha yangu, na Nitengenezee Aakherah yangu ambayo ndiyo marejeo yangu. Na yajaalie maisha yangu yawe marefu katika kufanya mambo mema na umauti wangu Ujaalie ni raha kwangu dhidi ya kila maovu." [Muslim]

 

Hadiyth – 9

وعن علي رضي الله عنه قَالَ: قَالَ لي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قُلْ : اللَّهُمَّ اهْدِني ، وسَدِّدْنِي )) .

وفي رواية : (( اللَّهمَّ إنِّي أسْألُكَ الهُدَى والسَّدَادَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Sema: Allaahumma ihdiniy wa saddidniy (Rabb Wangu! Niongoze na Unifanye mimi kusimama wima)."

Na katika riwaayah nyingine: "Allaahumma inniy as'alukal hudaa wa sadaad (Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba uongofu na kuwa wima)." [Muslim]

 

Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ العَجْزِ ، وَالكَسَلِ ، وَالجُبْنِ ، والهَرَمِ ، والبُخْلِ ، وأعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ القَبْرِ ، وأعوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ المَحْيَا وَالمَمَاتِ )) .

وفي رواية : (( وَضَلَعِ الدَّيْنِ ، وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ )) . رواه مسلم .

Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Allaahumma inniy a'uwdhu Bika minal 'ajzi wal kasali wal jubni wal harami wal bukhli wa a'uwdhu Bika min 'adhaabil qabri wa a'uwdhu Bika min fitnatil mahyaa wal mamaat (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na unyonge na uvivu, na uzembe na uzee na ubakhili. Na ninajilinda Kwako na adhabu ya kaburini, na ninajilinda Kwako na fitna ya uhai na kifo)."

Na katika riwaayah yake nyingine: "Wa dhala'id dayni wa ghalabatir rijaal (Na najilinda Kwako kutokana na uzito wa deni na kushindwa na watu)." [Muslim]

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي بكر الصديق رضي الله عنه : أنَّه قَالَ لرسُولِ الله صلى الله عليه وسلم : عَلِّمْنِي دُعَاءً أَدْعُو بِهِ في صَلاَتِي ، قَالَ : (( قُلْ : اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمتُ نَفْسِي ظُلْماً كَثِيراً ، وَلاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ ، فَاغْفِرْ لي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ ، وارْحَمْنِي ، إنَّكَ أنْتَ الغَفُورُ الرَّحِيمُ )) متفق عَلَيْهِ .

وفي روايةٍ : (( وفي بيتي )) وَرُوِيَ : (( ظلماً كثيراً )) ورُوِي : (( كبيراً )) بالثاء المثلثة وبالباء الموحدة ؛ فينبغي أنْ يجمع بينهما فيقال : كثيراً كبيراً .

Imepokewa kutoka kwa Abu Bakar As-Swiddiyq kuwa alimwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Nifundishe duaa ntakayoomba katika Swalaah yangu." Akasema: "Sema: Allaahumma inniy dhalamtu nafsiy dhulman kathiyrannwalaa yaghfirudh dhunuba illaa Anta Faghfirliy Maghfiratan min 'Indika warhamniy Innaka Antal Ghafuurur Rahiym (Rabb Wangu! Hakika nimejidhulumu dhulma nyingi, na hakuna anayesamehe dhambi isipokuwa Wewe. Nisamehe msamaha wa kutoka Kwako tu, na unirehemu, hakika Yako ni Mwingi wa Kusamehe na Kuhurumia)." [Al-Bukhaariy, Muslim. At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

Na katika riwaayah: "Na katika nyumba yangu." Na imepokewa: "Dhulman kathiyran (dhulma nyingi)." Na imepokewa: "Kabiyran (kubwa), kwa tha na kwa ba, hivyo zinatakiwa zijumlishe kwa kusema: "Kathiyran kabiyran."

 

Hadiyth – 12

وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم : أنَّه كَانَ يدْعُو بِهذا الدُّعَاءِ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي وَجَهْلِي ، وإسرافِي في أمْرِي ، وَمَا أنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنّي ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي جِدِّي وَهَزْلِي ؛ وَخَطَئِي وَعَمْدِي ؛ وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أخَّرْتُ ، وَمَا أسْرَرْتُ وَمَا أعْلَنْتُ ، وَمَا أنتَ أعْلَمُ بِهِ مِنِّي ، أنْتَ المُقَدِّمُ ، وأنْتَ المُؤَخِّرُ ، وأنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba kwa duaa hii: "Allaahumma Ghfirliy khatwiyatiy wa jahliy wa israafiy fiy amriy wa maa Anta a'alamu bihi miniiy, Allaahumma Ghfirliy jiddiy wa hazliy wa khata'iy wa 'amdiy wa kullu dhaalika 'indiy. Allaahumma Ghfirliy maa qaddamtu wa maa akhkhartu wa maa asrartu wa maa a'lantu wa maa Anta a'alamu miniy Antal Muqaddimu wa Antal Muakhkhiru wa Anta 'alaa kulli Shaiyin Qadiyr (Rabb Wangu! Nighufurie makosa yangu na ujinga wangu. Na israfu yangu kwangu katika mambo yangu yote na lile ambalo Wewe Unalijua zaidi kuliko mimi. Rabb Wangu! Nighufirie makosa yangu niliyoyafanya kwa makusudi, kwa ujinga na kwa mzaha wangu na yote hayo niliyonayo. Ee Rabb Wangu! Nighufurie nilichokichelewesha, nilicho kifanya kwa siri na nilicho kifanya kwa bayana. Wewe Ndiye Unayetanguliza, na Wewe Ndiye Unayechelewesha na Wewe ni Muweza wa kila kitu)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 13

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم  كَانَ يقول في دُعَائِهِ : (( اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَمِلْتُ ومنْ شَرِّ مَا لَمْ أعْمَلْ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema katika duaa yake: "Allaahumma inniy a'uwdhubika min sharri maa 'amiltu wa min sharri maa lam a'amal (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na shari ya niliyoyafanya na kwa shari ya yale ambayo sijayatenda)." [Muslim]

 

Hadiyth – 14

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ مِن دعاءِ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ زَوالِ نِعْمَتِكَ، وتَحَوُّلِ عَافِيَتِكَ، وفُجَاءةِ نِقْمَتِكَ ، وَجَميعِ سَخَطِكَ )) . رواه مسلم .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Ni miongoni mwa duaa za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Allaahumma inniy a'uwdhu bika min zawaali ni'matika wa tahawwuli 'aafiyatika wa fujaati niqmatika wa jamiy'i sakhatwika (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na kukoma kwa neema Zako na kubadilika kwa usalamaWako na kuja haraka kwa ghadhabu Yako na hasira Yako yote)." [Muslim]

 

Hadiyth – 15

وعن زيد بن أرقم رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ العَجْزِ وَالكَسَلِ ، والبُخْلِ والهَرَمِ ، وَعَذابِ القَبْرِ ، اللَّهُمَّ آتِ نَفْسِي تَقْوَاهَا ، وَزَكِّها أنْتَ خَيْرُ مَنْ زَكَّاهَا ، أنْتَ وَلِيُّهَا وَمَوْلاَهَا ، اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عِلْمٍ لا يَنْفَعُ؛ وَمِنْ قَلْبٍ لا يَخْشَعُ ، وَمِنْ نَفْسٍ لاَ تَشْبَعُ ؛ وَمِنْ دَعْوَةٍ لا يُسْتَجابُ لَهَا )) .رواه مسلم .

Amesema Zayd bin Arqam (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Allaahumma inniy a'uwdhu bika minal 'ajzi wal kasal wal bukhli wal harami wa 'Adhaabil qabr. Allaahumma aati nafsiy taqwaahaa wa zakkihaa Anta khayra man zakkaahaa Anta waliyyuhaa wa mawlaahaa. Allaahumma inniy a'uwdhu bika min 'ilmin laa yanfa'u wa min qalbin laa yakhsha'u wa min nafsin laa tashba'u wa min da'watin laa yustajaabu lahaa (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na unyonge na uvivu, na ubakhili na uzee na adhabu ya kaburini. Rabb Wangu! Ipatie nafsi yangu Taqwa na Uitakase kwani Wewe ni mbora wa kuitakasa, Wewe Ndiye Mlinzi na Bwana (Mola) Wake. Rabb Wangu! Hakika ninajilinda na elimu isiyo na manufaa na kwa moyo usioogopa na nafsi isiyo shiba na duaa isiyojibiwa)." [Muslim]

 

Hadiyth – 16

وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول : (( اللَّهُمَّ لَكَ أسْلَمْتُ ، وَبِكَ آمَنْتُ ، وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ ، وإلَيْكَ أنَبْتُ ، وَبِكَ خَاصَمْتُ ، وإلَيْكَ حَاكَمْتُ . فَاغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ ، وَمَا أَخَّرْتُ ، وَمَا أَسْرَرْتُ ، وَمَا أعْلَنْتُ ، أنتَ المُقَدِّمُ ، وأَنْتَ المُؤَخِّرُ ، لا إلهَ إِلاَّ أنْتَ )) .

زَادَ بَعْضُ الرُّوَاةِ : (( وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Allaahumma laka aslamtu wa bika aamantu wa 'alayka tawakkaltu wa ilayka haakamtu faghfirliy maa qaddamtu wa maa akhkhartu wa maa asrartu wa maa a'lantu Antal Muqaddim wa Antal Muakhkhiru Laa ilaaha illaa Anta (Rabb Wangu! Kwako nimenyenyekea, na nimekutegemea Wewe, na nimerudi Kwako na Kwako nataka usaidizi na Kwako ninataka hukumu. Hivyo, nisamehe madhambi yangu niliyoyatanguliza na nitakayo yafanya (baadae), na yale niliyo yafanya kwa siri na kwa dhahiri. Wewe Ndiye wa Mwanzo na Wewe Ndiye wa Mwisho. Hapana muabudiwa wa haki ila Wewe)."

Wameongeza baadhi ya wapokezi: "Walaa Hawla walaa Quwwata illaa BiLLaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 17

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ النبيّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يدعو بِهؤُلاءِ الكَلِمَاتِ : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ النَّارِ ، وَعَذَابِ النَّارِ ، وَمِنْ شَرِّ الغِنَى وَالفَقْرِ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) ؛ وهذا لفظ أَبي داود .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Allaahumma inniy a'uwdhu bika min fitnatin naari wa 'adhaabin naari wa min sharril ghinaa wal faqr (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na fitna ya Moto na adhabu ya Moto na shari ya utajiri na ufakiri)." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh, na hii ni lafdhi ya Abu Daawuwd]

 

Hadiyth – 18

وعن زياد بن عِلاَقَةَ عن عمه ، وَهُوَ قُطْبَةُ بنُ مالِكٍ رَضِيَ اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ النبيّ صلى الله عليه وسلم يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنْ مُنْكَرَاتِ الأخْلاَقِ ، وَالأعْمَالِ ، والأهْواءِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwake Ziyaad bin 'Ilaaqah kutoka kwa ami yake, naye Qutbah bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alisema: Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu a'alyhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Allaahumma a'uwdhu bika min munkaraatil akhlaaq wal a'maal wal ahwaai (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na utovu wa tabia na amali mbaya na hawaa (matamanio)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 19

وعن شَكَلِ بن حُمَيدٍ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قلتُ : يَا رسولَ الله ، علِّمْنِي دعاءً ، قَالَ : (( قُلْ : اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ سَمْعِي ، وَمِنْ شَرِّ بَصَرِي ، وَمِنْ شَرِّ لِسَانِي ، وَمِنْ شَرِّ قَلْبِي ، وَمِنْ شَرِّ مَنِيِّي )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Shakal bin Humayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Ee Rasuli wa Allaah: "Nifundishe duaa." Akasema: Sema: "Allaahumma inniy a'uwdhu Bika min sharri sam'iy wa min sharri baswariy wa min sharri lisaaniy wa min sharri qalbiy wa sharri manniyyiy (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na uovu wa masikizi yangu, na uovu wa uoni wangu na uovu wa ulimi wangu, na uovu wa moyo wangu na uovu wa sehemu zangu za siri (utupu))." [Abu Daawud na At-Timidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 20

وعن أنس رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ البَرَصِ ، والجُنُونِ ، والجُذَامِ ، وَسَيِّيءِ الأسْقَامِ )) . رواه أَبُو داود بإسناد صحيحٍ .

Imepokewa kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Allaahumma inniy a'uwdhu Bika minal barasw wal junuwn wal jidhaam wa sayyiil asqaam (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na ukoma, na umajununi, na ugonjwa wa ngozi na maradhi mengine mabaya)." [Abu Daawuwd kwa isnaad Swahiyh]

 

Hadiyth – 21

وعن أَبي هريرة رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنَ الجُوعِ ، فَإنَّهُ بِئْسَ الضَّجِيعُ ، وأعوذُ بِكَ منَ الخِيَانَةِ ، فَإنَّهَا بِئْسَتِ البِطَانَةُ )) . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba: "Allaahumma inniy a'uwdhu Bika minal juw'i fainnahu bisal dhajiy'u wa a'uwdhu Bika minal khiyaanati fainnahaa bisatil bitwaanah (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na njaa, kwani huyo ni rafiki mbaya na ninajilinda Kwako na hiyana, kwani ni tabia mbaya ya ndani ya mwili)." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]

 

Hadiyth – 22

وعن عليّ رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ مُكَاتباً جاءهُ فَقَالَ : إنِّي عَجِزْتُ عَنْ كِتَابَتِي فَأعِنِّي ، قَالَ : ألا أُعَلِّمُكَ كَلِماتٍ عَلَّمَنِيهنَّ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، لَوْ كَانَ عَلَيْكَ مِثْلُ جَبَلٍ دَيْناً أدَّاهُ اللهُ عَنْكَ ؟ قُلْ : (( اللَّهُمَّ اكْفِني بِحَلاَلِكَ عَنْ حَرَامِكَ ، وَأغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِواكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mtumwa (aliyeandikiana na bwana wake kuununua uhuru wake kwa kuandikiana mkataba wa hela atakazo toa) alikuja kwake na kumwambia: "Hakika nimeshindwa kulipa sehemu ya hela za mkataba tulizo kubaliana, hivyo nisaidie." Alimwambia: "Je, sikufundishi maneno ambayo alinifundisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? lau una deni mfano wa jabali Allaah Atakuondoshea. Sema: Allaahumma kfiniy bihalaalika 'an haraamika wa ghniniy bifadhlika 'amman siwaaka (Rabb Wangu! Nitosheleze mimi na halali kutoka Kwako kutokana na haramu (usinifanye kutegemea haramu) na Nipatie utajiri (na kinai) kwa fadhila Zako ambayo itanifanya nisimtegemee mwengine yeyote mbali na Wewe)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 23

وعن عِمْرَانَ بن الحُصَينِ رضي الله عنهما : أنَّ النبيّ صلى الله عليه وسلم عَلَّمَ أبَاهُ حُصَيْناً كَلِمَتَيْنِ يَدْعُو بهما : (( اللَّهُمَّ ألْهِمْني رُشْدِي ، وأعِذْنِي مِنْ شَرِّ نَفْسي )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Imraan bin Al-Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimfundisha baba yao, Huswayn maneno mawili ambayo alikuwa akiomba kwa kuyatumia: "Allaahumma alhimniy rushdiy wa a'idhniy min sharri nafsi (Rabb Wangu! Nipatie uongofu na Unilinde na shari ya nafsi yangu)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 24

وعن أَبي الفضل العباس بن عبد المطلب رضي الله عنه قَالَ : قُلْتُ : يَا رسول الله عَلِّمْني شَيْئاً أسْألُهُ الله تَعَالَى، قَالَ : (( سَلوا الله العَافِيَةَ )) فَمَكَثْتُ أَيَّاماً، ثُمَّ جِئْتُ فَقُلتُ : يَا رسولَ الله عَلِّمْنِي شَيْئاً أسْألُهُ الله تَعَالَى ، قَالَ لي : (( يَا عَبَّاسُ ، يَا عَمَّ رسول اللهِ ، سَلُوا الله العَافِيَةَ في الدُّنيَا والآخِرَةِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema Abil Fadhl Al-'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Nifundishe duaa ambayo nitamuomba nayo Allaah Ta'aalaa." Akasema: "Mtake Allaah siha nzuri." Nikakaa kwa siku kadhaa, kisha nikaja na kumwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Nifundishe duaa ambayo nitamuomba nayo Allaah Ta'aalaa." Akaniambia: "Ee 'Abbaas, ee ami ya Rasuli wa Allaah! Muombe Allaah afya nzuri duniani na Aakhirah." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 25

وعن شَهْرِ بن حَوشَبٍ ، قَالَ : قُلْتُ لأُمِّ سَلَمة رَضِيَ اللهُ عنها ، يَا أمَّ المؤمِنينَ ، مَا كَانَ أكثْرُ دعاءِ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ، إِذَا كَانَ عِنْدَكِ ؟ قالت : كَانَ أكْثَرُ دُعائِهِ : (( يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Amesema Shahr bin Hawshab: Nilimuuliza Umm Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Ee Mama wa Waumini! Ni duaa gani aliyokuwa akiomba sana Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa kwako?" Akasema: "Miongoni mwa duaa aliyokuwa akiomba sana ni Yaa muqallibal quluwbi thabbit qalbiy 'alaa Diynik (Ee Mwenye kugeuza mioyo uthibitishe moyo wangu katika Dini Yako)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 26

وعن أَبي الدرداءِ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( كَانَ مِنْ دُعاءِ دَاوُدَ : اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ حُبَّكَ ، وَحُبَّ مَنْ يُحِبُّكَ ، وَالعَمَلَ الَّذِي يُبَلِّغُنِي حُبَّكَ ، اللَّهُمَّ اجْعَلْ حُبَّكَ أحَبَّ إلَيَّ مِنْ نَفْسِي ، وأهْلِي ، وَمِنَ الماءِ البارِدِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abid Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ilikuwa miongoni mwa duaa za Daawuwd: Allaahumma inniy asalika hubbaka wa hubba man yuhibbuka wal 'amalal ladhiy yuballighuniy hubbaka. Allaahumma j'al hubbaka ahabba ilayya min nafsiy wa ahliy wa minal maail baarid (Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba mapenzi Yako, na mapenzi ya wale Unao wapenda na amali ambayo itanifikisha kwa mapenzi Yako. Rabb Wangu! Yafanye mapenzi yangu Kwako ni mahububu zaidi kwangu kuliko nafsi yangu, na familia yangu na maji baridi)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 27

وعن أنس رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ألِظُّوا بـ ( يَاذا الجَلاَلِ والإكْرامِ ) )) . رواه الترمذي ، ورواه النسائي من رواية ربيعة بن عامِرٍ الصحابي ، قَالَ الحاكم : (( حديث صحيح الإسناد )) .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jilazimisheni na mukariri sana maneno ya Yaadhal Jalaali wal Ikraam (Umetukuka Ee Mwenye Enzi na Mwenye Kustahiki Kuheshimika)." [At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy kwa riwaayaah ya Rabi'ah bin 'Aamir, ambaye ni Swahaaba. Amesema Al-Haakim: Isnaad yake ni Swahiyh]

 

Hadiyth – 28

وعن أَبي أُمَامَةَ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : دعا رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، بدُعاءٍ كَثيرٍ ، لَمْ نَحْفَظْ مِنْهُ شَيْئاً ؛ قُلْنَا : يَا رسول الله ، دَعَوْتَ بِدُعاءٍ كَثِيرٍ لَمْ نَحْفَظْ مِنْهُ شَيْئاً ، فَقَالَ : (( ألا أدُلُّكُمْ عَلَى مَا يَجْمَعُ ذَلِكَ كُلَّهُ ؟ تقول : اللَّهُمَّ إنِّي أسَألُكَ مِنْ خَيْر مَا سَأَلَكَ مِنْهُ نَبِيُّكَ محمَّدٌ صلى الله عليه وسلم ؛ وأعوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا استَعَاذَ مِنْهُ نَبِيُّكَ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم، وأنتَ المُسْتَعانُ ، وَعَليْكَ البَلاَغُ ، وَلاَ حَولَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Amesema abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba duaa nyingi sana ambazo hatukuweza kuzihifadhi, hivyo tukamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Umeomba duaa nyingi ambazo hatukuhifadhi humo chochote." Akasema: "Siwaonyeshi nyinyi duaa ambayo itajumlisha hizo zote? Semeni: Allaahumma inniy asaluka min khayri maa saalaka minhu Nabiyyuka Muhammadun (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) wa a'uwdhu bika min sharri masta'adha minhu Nabiyyuka Muhammadun (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) wa Antal Musta'aanu wa 'alaykal balaaghu walaa hawla walaa quwwata illaa BiLLaahi (Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba alicho kuomba Nabiy Wako Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na ninajilinda Kwako na uovu alioomba ulinzi kwayo Nabiy Wako Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Na Wewe tu Ndiye Msaidizi wa pekee wa kuombwa msaada na Kwako ndio tunatarajia kuitikiwa maombi yetu. Na hapana hila wala nguvu isipokuwa kupitia kwa Allaah)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 29

وعن ابن مسعود رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : كَانَ من دعاءِ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ مُوجِبَاتِ رَحْمَتِكَ، وَعَزَائِمَ مَغْفِرَتِكَ، والسَّلامَةَ مِنْ كُلِّ إثْمٍ، والغَنِيمَةَ مِنْ كُلِّ بِرٍّ ، والفَوْزَ بالجَنَّةِ ، والنَّجَاةَ مِنَ النَّارِ )) . رواه الحاكم أَبُو عبد الله ، وقال : (( حديث صحيح عَلَى شرط مسلمٍ )) .

Amesema Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Miongoni mwa duaa za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni: Allaahumma inniy asaluka muujibaati Rahmatika wa 'azaaima Maghfiratika was Salaamata min kulli birrin wal fawza bil jannati wan najaata minan naar (Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba unipatie Rehema Zako Maghfira Yako na Unipatie ngawira kwa kukutii kwa kila jambo na kufuzu kupata pepo na Kuniokoa na Moto)." [Al-Haakim Abu 'Abdillaah, na akasema hii ni Hadiyth Swahiyh kulingana na mashartiyaliyowekwa na Muslim]

 

 

 

 

 

 

Share