02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kuwaombea Wasio Kuwepo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل الدعاء بظهر الغيب

02-Mlango Wa Fadhila za Kuwaombea Wasio Kuwepo

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ ﴿١٠﴾

Na wale waliokuja baada yao wanasema: Rabb wetu! Tughufurie pamoja na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan. [Al-Hashr: 10]

وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ ﴿١٩﴾

Na omba Maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. [Muhammad: 19]

رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾

Rabb wetu! Nighufurie mimi na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu. [Ibraahiym: 41]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي الدرداء رضي اللهُ عنه : أنَّه سَمِعَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( مَا مِنْ عَبْدٍ مُسْلمٍ يدعُو لأَخِيهِ بِظَهْرِ الغَيْبِ إِلاَّ قَالَ المَلَكُ : وَلَكَ بِمِثْلٍ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna mja yeyote Muislamu anamuombea ndugu yake asiye kuwepo isipokuwa Malaaikah anasema, nawe ana mfano wa hayo." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي الدرداء رضي اللهُ عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول : (( دَعْوَةُ المَرْءِ المُسْلِمِ لأَخيهِ بِظَهْرِ الغَيْبِ مُسْتَجَابَةٌ ، عِنْدَ رَأسِهِ مَلَكٌ مُوَكَّلٌ كُلَّمَا دَعَا لأَخِيهِ بِخَيْرٍ قَالَ المَلَكُ المُوَكَّلُ بِهِ : آمِينَ ، وَلَكَ بِمِثْلٍ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Duaa ya mtu Muislamu kwa nduguye asiye kuwepo inakubaliwa kwani Malaaikah anawakilishwa kuwa naye, kila anapomuombea ndugu yake kwa kheri husema yule Malaaikah aliyewakilishwa kwake: Aamiyn (iwe hivyo), nawe upate mfano wa hayo (unayomuombea ndugu yako)." [Muslim]

 

 

Share