017-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Kuapa Kwa Amana

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ

 

Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

017- Kuapa Kwa Amana

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Haifai kuapa kwa amana.  Ni kwa Hadiyth ya Buraydah (Radhwiya Allaah ‘anhu), amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 "‏ مَنْ حَلَفَ بِالأَمَانَةِ فَلَيْسَ مِنَّا ‏"

 

“Mwenye kuapa kwa amana, basi si katika sisi”.  [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3253), Ibn Hibaan (1318) na Al-Bayhaqiy (10/30)].

 

Kwa maana si katika wenye kufuata njia yetu, bali ni mwenye kujishabihisha na wengineo, na hii ni tabia ya Ahlul Kitaab.  Huenda amekusudia kwalo makamio juu yake.  [‘Awn Al-Ma’abuwd (9/79 na 80)].

 

Ikiwa ataongeza Jina la Allaah kwenye tamko la amana akasema:  “Naapa kwa Amana ya Allaah”, baadhi ya ‘Ulamaa wamesema itazingatiwa ni kiapo chenye kuwajibisha kafara, kwa kuwa Amana ya Allaah ni Sifa kati ya Sifa Zake, hivyo inajuzu kuapa hivyo!!

 

Lakini hapa kuna angalizo.  Tunasema hakuna dalili thibitishi kuwa Amana ni Sifa kati ya Sifa za Allaah, bali ni Amri kati ya Amri Zake, na Faradhi kati ya Faradhi Zake.  Kwa ajili hiyo, wamekatazwa watu kuapia kwalo kwa sababu hilo ni kufanya sawa kati yake na kati ya Majina ya Allaah Ta’aalaa na Sifa Zake. [Ma’aalim As-Sunan cha Al-Khattwaabiy].

 

Isitoshe, imethibiti katazo la kuapa kwa amana.  Hivyo, rai sahihi ni kuwa, haijuzu kabisa kuapa kwa neno hilo.  Na hii ni kauli ya Mahanafiy.  Na Ibn ‘Abdul Barri na wengineo wameinasibisha kwa Ash-Shaafi’iy.  [Al-Badaai’u (3/6), Al-Mughniy (11/207) na At-Tamhiyd (14/372)].

 

                                               

Share