007-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Uongo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم الكذب
007-Mlango Wa Kuharamishwa Uongo
قال الله تَعَالَى :
وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ ﴿٣٦﴾
Na wala usifuate usiyo na elimu nayo. [Al-Israa: 36]
مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾
Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 18]
Hadiyth – 1
وعن ابن مسعود رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى البِرِّ ، وإنَّ البِرَّ يَهْدِي إِلَى الجَنَّةِ ، وإنَّ الرَّجُلَ لَيَصْدُقُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقاً . وإنَّ الكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الفُجُورِ ، وإنَّ الفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ ، وإنَّ الرَّجُلَ لَيَكْذِبُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ كَذَّاباً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika ukweli unamuongoza mtu katika wema na wema unampeleka mtu Peponi. Na hakika mtu huendelea kusema ukweli mpaka akaitwa mkweli mbele ya Allaah. Na hakika uwongo unampeleka mtu katika uchafu na uchafu unampeleka mtu Motoni. Na mtu huendelea kusema uwongo mpaka akaandikwa kuwa ni muongo mbele ya Allaah." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( أرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ ، كَانَ مُنَافِقاً خَالِصاً ، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ ، كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْ نِفاقٍ حَتَّى يَدَعَهَا : إِذَا أؤْتُمِنَ خانَ ، وَإِذَا حَدَّثَ كَذَبَ ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ ، وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu yeyote akiwa na mambo manne atakuwa mnafiki hasa, na ataekuwa na moja katika hayo manne atakuwa na sifa moja ya unafiki mpaka aliache: Kama akiaminiwa anaondoa uaminifu; na akizungumza anaongopa; na anapotoa ahadi hivunja; na anapogombana anaiacha haki na kuwa jeuri." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( مَنْ تَحَلَّمَ بِحُلْمٍ لَمْ يَرَهُ ، كُلِّفَ أنْ يَعْقِدَ بَيْنَ شَعِيرَتَيْن وَلَنْ يَفْعَلَ ، وَمَنِ اسْتَمَعَ إِلَى حَديثِ قَوْمٍ وَهُمْ لَهُ كَارِهُونَ ، صُبَّ في أُذُنَيْهِ الآنُكُ يَوْمَ القِيَامَةِ ، وَمَنْ صَوَّرَ صُورَةً عُذِّبَ وَكُلِّفَ أنْ يَنْفُخَ فِيهَا الرُّوحَ وَلَيْسَ بنافِخٍ )) . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kubuni ndoto mbaya ambayo hakuona, atalazimishwa Siku ya Qiyaamah kufunga fundo baina ya mbegu za shayiri na hataweza. Na mwenye kusikiliza mazungumzo ya watu na wao wanachukia hilo, atamiminiwa risasi iliyo yeyushwa masikioni mwake Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kuchora picha ataadhibiwa na kukalifishwa kupuliza ndani yake uhai na hataweza kufanya hivyo." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( أَفْرَى الفِرَى أنْ يُرِيَ الرَّجُلُ عَيْنَيْهِ مَا لَمْ تَرَيَا )) . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwake Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Uongo ulio mkubwa zaidi ni kwa mtu kudai kuwa ameona kitu kwa macho yake ambacho hakukiona." [Al-Bukhaariy]. Na maana yake ni kusema: "Kuona kitu ambacho hukuona."
Hadiyth – 5
وعن سَمُرَةَ بنِ جُنْدُبٍ رضي الله عنه قَالَ : كَانَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم مِمَّا يُكْثِرُ أنْ يَقُولَ لأَصْحَابِهِ : (( هَلْ رَأَى أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنْ رُؤْيَا ؟ )) فَيَقُصُّ عَلَيْهِ مَنْ شَاءَ اللهُ أنْ يَقُصَّ، وإنَّهُ قَالَ لنا ذَات غَدَاةٍ : (( إنَّهُ أَتَانِيَ اللَّيْلَةَ آتِيَانِ ، وإنَّهُمَا قَالا لِي : انْطَلِقْ ، وإنِّي انْطَلَقتُ مَعَهُمَا ، وإنَّا أَتَيْنَا عَلَى رَجُلٍ مُضْطَجِعٍ ، وَإِذَا آخَرُ قائِمٌ عَلَيْهِ بِصَخْرَةٍ ، وَإِذَا هُوَ يَهْوِي بِالصَّخْرَةِ لِرَأْسِهِ ، فَيَثْلَغُ رَأسَهُ ، فَيَتَدَهْدَهُ الحَجَرُ هَا هُنَا ، فَيَتْبَعُ الحَجَرَ فَيَأخُذُهُ فَلاَ يَرْجِعُ إِلَيْهِ حَتَّى يَصِحَّ رَأسُهُ كَما كَانَ ، ثُمَّ يَعُودُ عَلَيْهِ ، فَيَفْعَلُ بِهِ مِثْلَ مَا فَعَلَ المَرَّةَ الأوْلَى ! )) قَالَ: (( قُلْتُ لهما : سُبْحانَ اللهِ ! مَا هَذَان ؟ قَالا لي : انْطَلِقِ انْطَلِقْ ، فَانْطَلَقْنَا ، فَأَتَيْنَا عَلَى رَجُلٍ مُسْتَلْقٍ لِقَفَاهُ ، وَإِذَا آخَرُ قَائِمٌ عَلَيْهِ بِكَلُّوبٍ مِنْ حَديدٍ ، وَإِذَا هُوَ يَأتِي أحَدَ شِقَّيْ وَجْهِهِ فَيُشَرْشِرُ شِدْقَهُ إِلَى قَفَاهُ ، ومِنْخَرَهُ إِلَى قَفَاهُ ، وعَيْنَهُ إِلَى قَفَاهُ ، ثُمَّ يَتَحَوَّلُ إِلَى الجانبِ الآخَرِ ، فَيَفْعَلُ بِهِ مِثْلَ مَا فَعَلَ بالجَانِبِ الأوَّلِ ، فَمَا يَفْرَغُ مِنْ ذَلِكَ الجانبِ حَتَّى يَصِحَّ ذَلِكَ الجانبُ كما كَانَ ، ثُمَّ يَعُودُ عَلَيْهِ فَيَفْعَلُ مِثْلَ مَا فَعَلَ فِي المرَّةِ الأُوْلَى )) قَالَ : (( قُلْتُ : سُبْحَانَ اللهِ ! مَا هذانِ ؟ قالا لي : انْطَلِقِ انْطَلِقْ ، فَانْطَلَقْنَا ، فَأَتَيْنَا عَلَى مِثْلِ التَّنُّورِ )) فَأَحْسِبُ أنَّهُ قَالَ : (( فإذا فِيهِ لَغَطٌ ، وأصْواتٌ ، فَاطَّلَعْنَا فِيهِ فإذا فِيهِ رِجَالٌ وَنِساءٌ عُرَاةٌ ، وَإِذَا هُمْ يَأتِيِهمْ لَهَبٌ مِنْ أسْفَلَ مِنْهُمْ ، فإذا أتاهُمْ ذَلِكَ اللَّهَبُ ضَوْضَوْا . قُلْتُ : مَا هَؤلاءِ ؟ قَالا لِي : انْطَلِقِ انْطَلِقْ ، فَانْطَلَقْنَا ، فَأَتَيْنَا عَلَى نَهْرٍ )) حَسِبْتُ أنَّهُ كَانَ يَقُولُ : (( أَحْمَرُ مِثْلُ الدَّمِ ، وَإِذَا في النَّهْرِ رَجُلٌ سابحٌ يَسْبَحُ ، وَإِذَا عَلَى شَطِّ النَّهْرِ رَجُلٌ قَدْ جَمَعَ عِنْدَهُ حِجَارَةً كثيرةً ، وَإِذَا ذَلِكَ السَّابحُ يَسْبَحُ ، مَا يَسْبَحُ ، ثُمَّ يَأتِي ذَلِكَ الَّذِي قَدْ جَمَعَ عِنْدَهُ الحِجَارَةَ ، فَيَفْغَرُ لَهُ فاهُ، فَيُلْقِمُهُ حَجَراً، فَينْطَلِقُ فَيَسْبَحُ ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَيْهِ، كُلَّمَا رَجَعَ إِلَيْهِ ، فَغَرَ لَهُ فَاهُ ، فَألْقَمَهُ حَجَراً ، قُلْتُ لهُما : مَا هذانِ ؟ قالاَ لِي : انْطَلِقِ انْطَلِقْ ، فَانْطَلَقْنَا ، فَأَتَيْنَا عَلَى رَجُلٍ كَريهِ المرْآةِ ، أَوْ كَأكْرَهِ مَا أنتَ رَاءٍ رجُلاً مَرْأىً ، فإذا هُوَ عِنْدَهُ نَارٌ يَحُشُّهَا وَيَسْعَى حَوْلَهَا . قُلْتُ لَهُمَا : مَا هَذَا ؟ قالاَ لي : انْطَلِقِ انْطَلِقْ ، فَانْطَلَقْنَا ، فَأتَيْنَا عَلَى رَوْضَةٍ مُعْتَمَّةٍ فِيهَا مِنْ كُلِّ نَوْرِ الرَّبيعِ ، وَإِذَا بَيْنَ ظَهْرَي الرَّوْضَةِ رَجُلٌ طَويلٌ لا أَكادُ أَرَى رَأسَهُ طُولاً في السَّماءِ ، وَإِذَا حَوْلَ الرَّجُلِ مِنْ أَكْثَرِ وِلدانٍ رَأيْتُهُمْ قَطُّ ، قُلْتُ : مَا هَذَا ؟ وَمَا هؤلاءِ ؟ قالا لي : انْطَلقِ انْطَلقْ ، فَانْطَلَقْنَا ، فَأَتَيْنَا إِلَى دَوْحَةٍ عَظيمةٍ لَمْ أَرَ دَوْحَةً قَطُّ أعْظمَ مِنْهَا ، وَلاَ أحْسَنَ ! قالا لي : ارْقَ فِيهَا ، فارْتَقَيْنَا فِيهَا إِلَى مَدينَةٍ مَبْنِيَّةٍ بِلَبنٍ ذَهَبٍ وَلَبنٍ فِضَّةٍ ، فَأَتَيْنَا بَابَ المَدِينَةِ فَاسْتَفْتَحْنَا ، فَفُتِحَ لَنَا فَدَخَلْنَاها ، فَتَلَقَّانَا رِجالٌ شَطْرٌ مِنْ خَلْقِهِمْ كأَحْسَنِ مَا أنت راءٍ ! وَشَطْرٌ مِنْهُمْ كأقْبَحِ مَا أنتَ راءٍ ! قالا لَهُمْ : اذْهَبُوا فَقَعُوا في ذَلِكَ النَّهْرِ ، وَإِذَا هُوَ نَهْرٌ مُعْتَرِضٌ يَجْرِي كأنَّ ماءهُ المَحْضُ في البَيَاضِ ، فَذَهَبُوا فَوَقَعُوا فِيهِ . ثُمَّ رَجَعُوا إلَيْنَا قَدْ ذَهَبَ ذَلِكَ السُّوءُ عَنْهُمْ ، فَصَارُوا في أحْسَنِ صُورَةٍ )) قَالَ : (( قالا لِي : هذِهِ جَنَّةُ عَدْنٍ ، وهذاك مَنْزِلُكَ ، فسَمَا بَصَري صُعُداً ، فإذا قَصْرٌ مِثْلُ الرَّبَابَةِ البَيضاءِ ، قالا لي : هذاكَ مَنْزلكَ ؟ قلتُ لهما : باركَ اللهُ فيكُما ، فذَراني فأدخُلَه . قالا لي : أمَّا الآنَ فَلاَ ، وأنتَ دَاخِلُهُ ، قُلْتُ لَهُمَا : فَإنِّي رَأيتُ مُنْذُ اللَّيْلَة عَجَباً ؟ فما هَذَا الَّذِي رأيتُ ؟ قالا لي : أمَا إنَّا سَنُخْبِرُكَ : أَمَّا الرَّجُلُ الأوَّلُ الَّذِي أَتَيْتَ عَلَيْهِ يُثْلَغُ رَأسُهُ بالحَجَرِ ، فإنَّهُ الرَّجُلُ يَأخُذُ القُرآنَ فَيَرفُضُهُ ، ويَنَامُ عَنِ الصَّلاةِ المَكتُوبَةِ . وأمَّا الرَّجُلُ الَّذِي أتَيْتَ عَلَيْهِ يُشَرْشَرُ شِدْقُهُ إِلَى قَفَاهُ ، ومِنْخَرُهُ إِلَى قَفَاهُ ، وَعَيْنُهُ إِلَى قَفَاهُ ، فإنَّهُ الرَّجُلُ يَغْدُو مِنْ بَيْتِهِ فَيَكْذِبُ الكِذْبَةَ تَبْلُغُ الآفاقَ . وأمَّا الرِّجَالُ والنِّسَاءُ العُراةُ الَّذِينَ هُمْ في مثْلِ بناءِ التَّنُّورِ ، فَإنَّهُمُ الزُّنَاةُ والزَّواني ، وأما الرجلُ الذي أتيتَ عَليهِ يَسْبَحُ في النهرِ ، ويلقم الحجارةَ ، فإنَّهُ آكلُ الربا ، وأمَّا الرَّجُلُ الكَريهُ المرآةِ الَّذِي عِنْدَ النَّارِ يَحُشُّهَا وَيَسْعَى حَوْلَهَا ، فإنَّهُ مالكٌ خازِنُ جَهَنَّمَ ، وأمَّا الرَّجُلُ الطَّويلُ الَّذِي في الرَّوْضَةِ ، فإنَّهُ إبراهيم صلى الله عليه وسلم ، وأمَّا الولدان الَّذِينَ حَوْلَهُ ، فكلُّ مَوْلُودٍ ماتَ عَلَى الفِطْرَةِ )) وفي رواية البَرْقانِيِّ : (( وُلِدَ عَلَى الفِطْرَةِ )) فَقَالَ بعض المُسلمينَ : يَا رسولَ الله ، وأولادُ المُشركينَ فقالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( وأولادُ المشركينَ ، وأما القومُ الذينَ كانُوا شَطْرٌ مِنْهُمْ حَسَنٌ ، وشَطْرٌ مِنْهُمْ قَبيحٌ ، فإنَّهُمْ قَومٌ خَلَطُوا عَمَلاً صَالِحاً وآخَرَ سَيِّئاً ، تَجاوَزَ الله عنهم )) . رواه البخاري .
وفي روايةٍ لَهُ : (( رَأيْتُ اللَّيْلَةَ رَجُلَيْنِ أتيَانِي فأخْرَجَانِي إِلَى أرْضٍ مُقَدَّسَةٍ )) ثُمَّ ذَكَرَهُ وقال : (( فَانْطَلَقْنَا إِلَى نَقْبٍ مثلِ التَّنُّورِ ، أعْلاهُ ضَيِّقٌ وَأسْفَلُهُ واسِعٌ ؛ يَتَوَقَّدُ تَحْتَهُ ناراً ، فإذا ارْتَفَعَتِ ارْتَفَعُوا حَتَّى كَادُوا أنْ يَخْرُجُوا ، وَإِذَا خَمَدَتْ ! رَجَعُوا فِيهَا ، وفيها رِجالٌ ونِساءٌ عراةٌ )) . وفيها : (( حَتَّى أتَيْنَا عَلَى نَهْرٍ مِنْ دَمٍ )) ولم يشكَّ (( فِيهِ رَجُلٌ قائِمٌ عَلَى وَسَطِ النَّهْرِ وعلى شطِّ النَّهرِ رجلٌ ، وبينَ يديهِ حِجارةٌ ، فأقبلَ الرجلُ الذي في النَّهرِ ، فَإذَا أرَادَ أَنْ يَخْرُجَ رَمَى الرَّجُلُ بِحَجَرٍ في فِيهِ ، فَرَدَّهُ حَيثُ كَانَ ، فَجَعَلَ كُلَّمَا جَاءَ لِيَخْرُجَ جَعَلَ يَرْمِي في فِيهِ بِحَجَرٍ ، فَيْرَجِعْ كما كَانَ )) . وفيها : (( فَصَعِدَا بي الشَّجَرَةَ ، فَأدْخَلاَنِي دَاراً لَمْ أرَ قَطُّ أحْسَنَ مِنْهَا ، فيهَا رِجَالٌ شُيُوخٌ وَشَبَابٌ )) . وفيها : (( الَّذِي رَأيْتَهُ يُشَقُّ شِدْقُهُ فَكَذَّابٌ ، يُحَدِّثُ بِالكِذْبَةِ فَتُحْمَلُ عَنْهُ حَتَّى تَبْلُغَ الآفَاقَ ، فَيُصْنَعُ بِهِ مَا رَأَيْتَ إِلَى يَومِ القِيَامَةِ )) ، وَفِيهَا : (( الَّذِي رَأيْتَهُ يُشْدَخُ رَأسُهُ فَرَجُلٌ عَلَّمَهُ اللهُ القُرْآنَ ، فَنَامَ عَنْهُ بِاللَّيْلِ ، وَلَمْ يَعْمَلْ فِيهِ بالنَّهارِ ، فَيُفْعَلُ بِهِ إِلَى يَوْمِ القِيَامَةِ ، والدَّارُ الأولَى الَّتي دَخَلْتَ دَارُ عَامَّةِ المُؤمِنِينَ ، وأمَّا هذِهِ الدَّارُ فَدَارُ الشُّهَداءِ ، وأنا جِبْرِيلُ ، وهذا مِيكائيلُ ، فَارْفَعْ رَأْسَكَ ، فَرَفَعْتُ رَأسِي ، فإذَا فَوْقِي مِثْلُ السَّحابِ ، قالا : ذاكَ مَنْزِلُكَ ، قُلْتُ : دَعَانِي أدْخُلُ مَنْزِلي ، قالا : إنَّهُ بَقِيَ لَكَ عُمُرٌ لَمْ تَسْتَكْمِلْهُ ، فَلَوِ اسْتَكْمَلْتَهُ أتَيْتَ مَنْزِلَكَ )) . رواه البخاري .
Amesema Samurah bin Jundub (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwauliza sana Swahaaba zake: "Yupo yeyote miongoni mwenu aliyeona ndoto?" Yule ambaye aliona ndoto alikuwa anahadithia yale ambayo Allaah amemtaka ahadithie. Na hakika alituambia mchana mmoja: "Hakika walikuja kwangu watu wawili jana usiku na wakaniambia: 'Twende pamoja.' Nami nikaenda pamoja nao mpaka tukafika kwa mtu aliyekuwa amelala chini, na mwengine amesimama juu yake akiwa na jiwe kubwa mkononi mwake. Alikuwa akimpiga kichwani mwake nalo, hivyo kukanyaga kichwa chake. Baada ya jiwe kubwa kumponda linabingirika masafa kidogo kutoka kwake. Yule mpondaji akalifuata na kulichukua na akarudi ile hali yake ya awali (kama kilivyo kuwa mwanzo). kisha anarudia kumponda na anamfanya kama alivyo mfanya mara ya kwanza." Akasema: "Nikawauliza: Ametakasika Allaah! Hawa ni kina nani?" Wakaniambia: "Twende, twende." Tukaondoka na kufika kwa mtu aliyekuwa amelala chini, na mwengine amesimama juu yake akiwa na kulabu ya chuma (ncha yake ikiwa imechongoka na ina makali) mkononi mwake. Naye alikuwa akija upande wake mmoja na kuukata mdomo wake mpaka shingoni mwake, na kisha kurarua pua yake mpaka shingoni mwake na kulifumua jicho lake mpaka shingoni mwake. Kisha anageuza upande wake mwengine na kufanya kama alivyofanya upande ule wa awali. Hamalizi upande huu wa pili mpaka ule upande wa kwanza urudi kama ulivyokuwa, kisha anarudia tena na kufanya kama alivyofanya awali. Akasema: "Nikasema: Ametakasika Allaah! Hawa ni kina nani?": Wakaniambia: "Twende zetu, twende zetu." Nasi tukaondoka mpaka tukakifikia kitu kilicho fanana na tanuri, nami nikadhania kuwa alisema: "Humo ndani ghafla tukasikia yakitoka makelele na sauti." Nasi tukaangalia tukawaona wanaume na wanawake waliokuwa uchi na mwako wa moto ulikuwa ukiwajilia kutoka chini. Na unapowafikia huo mwako basi walikuwa wanalia. Nikawauliza: "Hawa ni kina nani?" Wakaniambia: "Twende twende." Nasi tuliondoka mpaka tukafika mtoni. Nilidhania kuwa alikuwa amesema kitu: "Maji ya mto huo yalikuwa mekundu mfano wa damu na humo ndani kulikuwa na mwongeleaji. Ukingoni mwa mto huo alisimama mtu na mlima wa mawe. Mwongeleaji alipokuwa anakuja upande wake alikuwa anampiga na jiwe, hivyo kuukanyaga uso wake, na kunfanya kurudi. Anaaza kuongelea tena, na anapo karibia ukingo wa mto mara nyengine tena, yule mtu aliyesimama ukingoni anampiga tena na jiwe ambalo linauponda uso wake." Niliwauliza: "Hawa ni kina nani?" Wakasema: "Twende, twende." Tukaondoka mpaka tukafika kwa mtu mwenye sura mbaya kabisa, ambaye kwa sura hizo alikuwa haangaliki akiwa karibu na moto mkali, naye alikuwa anauzunguka. Nikauliza: "Huyu ni nani?" Wakaniambia: "Twende, twende." Tuliondoka na kufiki katika bustani ambalo lilikuwa na maua aina yote ya majira ya kuchipua. Katikati ya bustani hilo kulikuwa na mtu aliyekuwa mrefu sana mpaka sikuweza kuona kichwa chake ambacho kilikuwa ni kama kinagusa mbingu, na huku amezungukwa na watoto wengi sana amabo sikuona mfano wake kabla ya hapo. Nikawauliza: "Huyu ni mtu gani? Na hawa watoto ni kina nani?" Wakaniambia: "Twende, twende." Tukaondoka mpaka tukafika katika mti mkubwa wala sijaona mti aina yake kwa ukubwa na uzuri. wakaniambia : "Panda juu." Tulipanda mpaka tukafika katika mji uliojengwa na matofali ya dhahabu na fedha yaliyo pangwa moja baada ya jengine. Tulifika katika mlango wa mji, tukafunguliwa, nasi tukaingia na kuwaona watu nusu ya miili yao ikiwa mizuri sana sijawahi kuona uzuri kama huo na nusu ya pili mbaya sana na wala sijaona ubaya wa mtu kama huo. Wakaniambia: "Nendeni mukaingie katika mto ule." Mto wenyewe ulikuwa ukipita katikati ya mji na maji yake yalikuwa safi na meupe. Waliingia ndani ya mto huo na walipotoka ile sehemu yote ya mwili iliyokuwa mbaya ilitoweka na wakawa wazuri kabisa. Akasema: "Wakaniambia: Hii ndio Pepo ya Edeni na ile ndiyo nyumba yako." Nilinyanyua macho yangu juu na kuona kasri nyeupe kama kipande cha kiwingu. Wakaniambia: "Hii ndiyo sehemu yako." Niliwaambia: "Allaah Awabariki nyote wawili! Niacheni niingie." Wakasema: "Sio sasa, lakini utaingia bila shaka yoyote siku moja." Nikawaambia: "Hakika nimeona maajabu mengi usiku wa leo. Haya niliyoyaona ni mambo gani?" Wakaniambia: "Ama sasa tutakueleza yote yaliyopita: "Ama yule mtu wa kwanza ambaye alikuwa akipondwa kichwa chake na jiwe kubwa, hakika ni mtu aliyehifadhi Qur-aan na kisha kuisahau na kuipuuza na alikuwa hatekelezi Swalaah za Faradhi. Na ama yule mtu aliyekuwa na kulabu ya chuma mkononi mwake, naye alikuwa akiukata mdomo wake mpaka shingoni mwake, na kisha kurarua pua yake mpaka shingoni mwake na kulifumua jicho lake mpaka shingoni mwake, hakika yeye ni mtu aliyekuwa akitoka asubuhi mapema na kueneza uongo ambao unaenea ulimwengu mzima. Na ama wale wanaume au wanawake. Na ama yule tuliyempata akiogelea na akirushiwa mawe, ni mlaji wa riba. Na ama kwa yule mtu mwenye sura mbaya, ambaye alikuwa haangaliki na aliyekuwa akiuzunguka moto ni Maalik, mlindaji wa Moto. Na ama yule mtu mrefu sana katika bustani ni Ibraahiym ('Alayhis salaam) na wale watoto waliomzunguka ni wale watoto walioaga dunia katika Fitrah (maumbile na Uislamu)."
Na katika riwaayah ya Al-Barqaaniy: "Waliozaliwa katika Fitrah." Wakasema baadhi ya Waislamu: "Ee Rasuli wa Allaah! na watoto wa wazazi mushirikina (watakuaje)?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Na hata watoto wa mushrikina. Na ama wale watu ambao upande mmoja ulikuwa mzuri na mwengine mbaya, ni wale watu waliofanya amali njema na mbaya, ambao wamesamehewa na allaah." [Al-Bukhaariy]
Na katika riwaayah yake nyengine: "Niliwaona usiku watu wawili ambao walikuja kwangu na kunipeleka katika ardhi tukufu." Na akataja kama ilivyo hapo juu. Na akasema: "Tukafika katika shimo liliokuwa katika ardhi kama tanuri, juu (mdomoni mwake) lilikuwa jembamba na chini pana. Ndani yake kulikuwa na moto, mwako wa moto unapopanda juu walikuwa wakinyanyuliwa mpaka karibu kutupwa nje ya hilo tanuri na mwako unapofifia basi hurudishwa chini ya tanuri. Na ndani yake kulikuwa na wanaume na wanawake waliokuwa uchi." Kisha tukaja mpaka katika mto wa damu na hapana shaka katika hili. Ndani ya mto huo kulikuwa na mtu amesimama katikati yake na mwengine alikuwa amesimama ukingoni mwake akiwa na mlima wa mawe mbele yake. Yule aliyekuwa katikati alikuwa anataka kutoka nje ya mto, na yule aliyekuwa ukingoni alikuwa akimrushia mawe, hivyo kumfanya arudi alikotoka. Jambo hili lilikuwa likifanyika kila wakati yule mtu alipotaka kutoka nje ya mto. Kisha wakapanda nami mti na kuniingiza katika nyumba ambayo sijawahi kuiona mfano wake kwa uzuri. Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na wazee na vijana. Riwaayah inaendelea: Nikaambiwa: Akikatwa mashavu yake ni mtu ambaye anaeneza uongo ambao unasambaa ulimwengu mzima, naye ataadhibiwa hivyo mpaka siku ya Qiyaamah." Na ndani yake: "Na yule uliyomuona akivyogwa na jabali kwenye kichwa ni mtu aliyefundishwa na Allaah Qur-aan, lakini akawa analala usiku, kuisahau na hakuifanyia kazi mchana. Atafanywa hivyo mpaka Siku ya Qiyaamah. Na ile nyumba ya mwanzo uliyoingia ni nyumba ya Waumini wa kawaida na ama nyumba hii ni ya mashahidi. Na mimi ni Jibriyl na huyu ni Mikail. Tafadhali nyanyua macho yako sasa, nami nikainua macho yangu juu, nikaona kitu mfano wa mawingu. Wakaniambia: "Hii ndiyo nyumba yako." Nikasema: "Niacheni niingie nyumba yangu." Wakasema: "Hakika bado una miaka ambayo hujakamilisha, na pindi utakapokamilisha miaka hiyo iliyobaki utaingia katika nyumba yako." [Al-Bukhaariy]